WASIFU WA MJI
SURA YA KWANZA
1.0. HISTORIA YA MKOA WA DODOMA NA WILAYA ZAKE
1.1. UTANGULIZI
Jina la Dodoma lilizaliwa hata kabla ya Mji wenyewe. Zipo hadithi nyingi
zinazoeleza jinsi jina hilo lilivyopatikana, lakini hadithi inayokubaliwa na wengi
ni hii: Tembo alikuja kunywa maji katika Kijito cha Kikuyu na akakwama
matopeni. Baadhi ya wenyeji waliomwona walipiga mayowe na kusema
“yadodomela” ambayo kwa lugha ya Kigogo maana yake ‘amezama’. Na tangu
wakati huo mahala hapo pakawa panajulikana kama Idodomya pale mahali
alipozama yule tembo.
Haijulikani kwa uhakika lini jina lilianza kutumiwa. Kwa kukisia huenda eon
hilo lilianza kutumika tokea mwaka 1860. Msafiri wa Kizungu H. M. Stanley
ambaye alipitia sehemu hiyo mnamo mwaka 1874 aliliita Dodoma. Lakini
hakuna kumbukumbu ya kimaandishi ya zamani zaidi kuhusu jina hilo
lilivyopatikana.
Miaka mingi iliyopita, wakati wa kipindi cha wahamiaji wa Kiafrika, wakazi wa
Dodoma ambao ni wafugaji waliweka makazi yao katika eneo linalojulikana sasa
kama Mkoa wa Dodoma. Katika kulinda mifugo yao, wakazi hawa waliishi kwa
kutawanyika na hasa ukizingatia kuwa walikuwa wachache mno kwa Idadi.
Mbali na shughuli za ufugaji, walijishughulisha pia na Kilimo cha kujikimu,
kutengeneza ala za muziki na usukaji wa vikapu: waliweza pia kuanzisha
usindikaji mdogo wa kutengeneza Chumvi, Nta na Samli:
`
Pamoja na kufanya kazi huko, kikwazo kikubwa kwa wakazi hawa kilikuwa ni
hali ya hewa. Mvua zinaponyesha vizuri wanapata chakula cha kutosha lakini
mvua zinapokuwa haba, hali ya chakula inakuwa ngumu sana. Mwaka 1890
Utawala wa Kijerumani uliingia mkoani Dodoma. Na miaka 18 baadaye yaani
mwaka 1912, eneo la Dodoma likawa eneo la Utawala wa Wilaya.
2
Mji wa Dodoma ukiwa makazi ya kudumu ulianzishwa mnamo mwaka 1910 kwa
ujio wa reli Kuu ya Kati. Reli Kuu ya Kati ambayo ndiyo hasa ilisababisha
kuwepo na kukua kwa Mji wa Dodoma ulitanguliwa na msafara wa Binadamu
uliotokana na biashara dhalimu ya Utumwa. Msafara huo ulikuwa kiungo kati ya
Bara na Pwani.
1.2. Mkoa wa Dodoma:
Kabla ya Tanganyika kupata Uhuru wake tarehe 09 Desemba 1961, Mkoa wa
Dodoma ulikuwa ni sehemu ya Jimbo la Kati (Central Province). Mwaka 1963,
Jimbo la kati liligawanywa na kupatikana Mikoa ya Dodoma na Singida. Mkoa
wa Dodoma ulianzaishwa kwa Tangazo la Serikali Na.450 la tarehe 27 Septemba,
1963.
Asilimia kubwa ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma ni Wabantu na kwa uchache
Wanilotiki. Makabila yanayopatikana Dodoma ni Wagogo, Wakaguru, Watiriko,
Wahehe, Wataturu, Wamasai na Wasukuma. Makabila mengine ni Warangi,
Wasandawe na Wabarbaig.
Mwaka 1962 Mkoa wa Dodoma ulikuwa na Wilaya tatu za kiutawala ambazo ni
Dodoma, Kondoa na Mpwapwa. Mabadiliko ya kwanza yalifanyika mwaka 1973
ambapo Wilaya ya Dodoma iligawanywa na kuwa Wilaya mbili za Dodoma Mjini
na Dodoma Vijijini pia mwaka 1995 Wilaya ya Mpwapwa iligawanywa na kuwa
Wilaya mbili za Mpwapwa na Kongwa.
Aidha mwaka 2005 Wilaya ya Dodoma Vijijini nayo iligawanywa na kuwa
Wilaya mbili za Bahi na Chamwino. Hivi karibuni mwaka 2010, Wilaya ya
Kondoa imegawanywa na kupata Wilaya za Kondoa na Chemba;
Hivi sasa Mkoa wa Dodoma una Wilaya sita Tarafa 28 kata 190 na Vijiji 512.
Mgawanyo wake Kiwilaya ni kama inavyooneshwa katika Jedwali lifuatalo
3
Jedawali Na. 1: Mgawanyo wa Maeneo ya Kiutawala:
Na. Wilaya Ukubwa wa
Eneo Sq. km.
Tarafa Kata Vijiji
1 Bahi 5,448 4 21 56
2 Chamwino 8,056 5 32 77
3 Kondoa 13,210 8 48 190
4 Mpwapwa 7,379 4 30 77
5 Dodoma Mjini 2,769 4 37 38
6 Kongwa 4,041 3 22 74
JUMLA 40,903 28 190 512
1.3. Wilaya ya Mpwapwa:
Wilaya ya Mpwapwa ilianzishwa mnamo mwaka 1929 ikiunganishwa na Wilaya
ya Kongwa.Wilaya hii ilitambulika Kiserikali mwaka 1952 kwa Tangazo la
Serikali Na.312 la tarehe 17 Oktoba, 1952.
Neno Mpwapwa limetokana na neno la asili la lugha ya Kigogo “MHAMVWA”
Likiwa na maana ya korongo lililokuwa linatiririsha maji mwaka mzima
lililotokea Kikombo kuelekea kusini yaani Mji mpya hadi kwa mshangoo.
Korongo hili limekatisha katikati ya Mpwapwa Mjini.
Wenyeji walitamka MHAMVWA kwa urahisi lakini Wakoloni walipofika
walishindwa kulitamka neno hilo MHAMVWA badala yake walitamka
Mpwapwa, hivyo wananchi/wenyeji nao pia walilizoea neno hilo la Mpwapwa
likazoeleka hadi hivi leo. Hivyo asili ya neno Mpwapwa ni MHAMVWA.
Makabila ya wenyeji wa Mpwapwa ni Wagogo, Wahehe, Wabena, Watiriko,
Wakaguru na makabila ya nje ya Mkoa wa Dodoma. Makabila haya
yanajishughulisha na kilimo na ufugaji.
Kihistoria, kabla ya Ukoloni Wilaya ya Mpwapwa wananchi waliishi Kiujamaa
wakiongozwa na Machifu katika kazi za Kiutawala na maendeleo.
Ofisi ya Halmashauri ilikuwa ikiitwa Bomani ambapo Mpwapwa na Kongwa
ilikua wilaya moja, kipindi hicho Maafisa Utumishi walikuwa wakiitwa
Bwanashauri na walikua wakiitika kwa Mkuu wa Wilaya na Machifu nao
walikuwa chini ya Bwanashauri.
4
Machifu walikuwa na mkutano wao ambao ulikuwa unaitwa Wihangulize
(makusanyiko) na agenda yao kuu ilikuwa kupanga mikakati ya ukusanyaji
mapato na vyanzo vya mapato ilikuwa ni kodi ya mifugo, kodi ya kichwa ,kodi
inayotokana na uharibifu wa mazingira pia kulikuwa na Sheria Ndogo ambapo
mtu akikutwa ameharibu mazingira anachapwa viboko.
Kipindi hicho vilindoni ilikuwa ni sehemu ya kuhifadhia chakula ambapo kila
Mwananchi alitakiwa kupeleka chakula kuhifadhiwa kwa ajili ya akiba kwa
matumizi ya kipindi cha njaa.
Mwaka 1947 Kongwa ilitambulika kama Wilaya Ndogo,na hii ilitokana na kilimo
cha karanga kushamiri. Makabila makuu yanayoishi Wilayani Mpwapwa ni
Wagogo, Wahehe, Wakaguru na Watiriko. Kuna makabila machache ya jamii ya
kifugaji kama Wamang’ati na Wamasai ambao wanaishi maeneo ya kusini mwa
Wilaya maeneo ya bwawa la Mtera na mto Ruaha.
Aidha kabila la Wahehe wapo Wilayani Mpwapwa kutokana na historia kuwa
walikuja huku wakati wa ukoloni wakitafuta maeneo mazuri ya kulima. Wilaya ya
Mpwapwa ina ukubwa wa kilometa zamraba 7,379 ikiwa na wakazi wapatao
253,602. Kiutawala Wilaya inaTarafa 4, Kata 30, Vijiji 77 na Vitongoji 490.
1.4. Wilaya ya Kondoa
Wilaya ya Kondoa ni Miongoni mwa Wilaya zilizoanzishwa kabla ya Uhuru chini
ya utawala wa Kijerumani na baadaye Mwingereza. Utawala wa Mwingereza
ulipokea Wilaya kutoka kwa Utawala wa Mjerumani mwaka 1916. Mwingereza
alisaidiwa na Machifu waliokuwa wakitumika kama watawala na pia Mahakimu.
Wilaya ilianzishwa kwa Tangazo la Serikali Na. 21 la tarehe 01 Machi, 1926.
Wakati Tanganyika ikiwa chini ya Utawala wa Ujerumani, Kondoa Irangi ilikuwa
miongoni mwa Tarafa zilizokuwa zinaunda Tanganyika ikiwa imegawanyika
katika kanda za Irangi, Uburunge na Usandawe.
Ilipofika mwaka 1966 Wilaya ya Kondoa ilikuwa miongoni mwa Wilaya 3
zilizounda Mkoa wa Dodoma ikiwa na tarafa 8, Kata 32 na Vijiji 154. Serikali ya
Tanganyika ilirithi mfumo wa Serikali za Mitaa kutoka kwa wakoloni na
kuzitumia kama nyenzo ya kuleta maendeleo kwa misingi ya kidemokrasia.
5
Halmashauri ya Kondoa ilikuwa miongoni mwa serikali za mitaa zilizoundwa
chini ya sura ya 72 ya mwaka 1926 ikijulikana kama Kondoa Council. Machifu
waliendelea kufanya kazi za utawala na Mahakama hadi utawala wa machifu
ulipositishwa mwaka 1963 kwa sheria na 13 ya 1962. Wilaya iliongozwa na
Mkuu wa Wilaya akisaidiana na Afisa wa Wilaya.
Tarehe 30 Juni, 1972, serikali ilifuta Halmashauri za Wilaya. Utaratibu wa
madaraka mikoani ulianzishwa ambapo mamlaka kutoka Wizarani ilipelekwa kwa
Maafisa wake katika Ofisi za Mikoani. Lengo la madaraka mikoani lilikuwa
kusukuma kwa kasi maendeleo vijijini. Ni katika kipindi hicho cha madaraka
Mikoani ambapo kulikuwa na utekelezaji wa mpango wa vijiji vya ujamaa kati ya
mwaka 1972 – 1975. Pia mpango wa elimu kwa wote (Universal Primay
Education) ulianzishwa. Kipindi hicho Wilaya ziliongozwa na Mkurugenzi wa
Maendeleo wa Wilaya akisaidiwa na Bodi ya Maendeleo ya Wilaya ambapo kwa
sasa anajulikana kama Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya.
Kutokana na dosari zilizotokana na mfumo wa kama vile kutowashirikisha
wananchi katika taratibu za maamuzi Serikali za Mitaa zilirejeshwa tena mwaka
1984 kwa lengo la kuwawezesha wananchi kujiamulia mambo yao pasipo
kutegemea Serikali Kuu kuwafanyia kila kitu. Hivyo Halmashauri za Wilaya
zilianzishwa kwa sheria Na. 7 ya mwaka 1982.
Mwaka 1997, Wilaya ilikuwa sehemu ya Sekretariati ya Mkoa baada ya
kuanzishwa kwa Sheria Na 19 ya mwaka 1997 – ikiwa na jukumu la kuiwezesha
Halmshauri ya Wilaya kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, ubora na viwango
vinavyokubalika.
Mwaka 2010, Wilaya iligawanywa na kupatikana Wilaya Mpya ya Chemba
ambayo bado haijaanza ili kusogeza huduma za jamii karibu zaidi na wananchi.
Pia katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 zilianzishwa Kata mpya 13,Vijijini 13
na Mitaa 11 hivyo kufanya Wilaya ya Kondoa kuwa na Tarafa 8, Kata 48 na Vijiji
190 na Mitaa 11. Aidha, majimbo mawili ya uchaguzi ya Kondoa Kusini na
Kondoa Kaskazini yalianzishwa mwaka 1985.
6
1.5. Wilaya ya Dodoma Mjini:
Wilaya ya Dodoma Mjini ilianzishwa mwaka 1950 kwa Tangazo la Serikali Na.
117 la tarehe 22 Septemba, 1950 kabla ya Uhuru na mwaka 1955 ilipopewa
hadhi ya “Council”. Kabla ya kupewa hadhi ya Halmashauri kulikuwa na Baraza
la Watemi chini ya Sheria Cap 72 ya “Native Authorities” Eneo la Dodoma
liligawanywa katika Temi (Chiefdom) 14 chini ya Mwenyekiti wao Mtemi
Mazengo. Eneo la Dodoma lilikuwa chini ya Mtemi Biringi, wasaidizi wa Mtemi
waliitwa Wapemba Moto (Sub-Chiefs). Wapembamoto wa Dodoma walikuwa
Masima na Mamba. Chini yao walikuwepo Wazenga Tumbi na Walugaluga.
Katika maeneo ya Mjini kulikuwa na Mkuu wa Wilaya akisaidiwa na Liwali na
Akida. Viongozi hawa walikuwa na Mamlaka ya Utawala na kusimamia Sheria.
Mabadiliko mengi yalianza kutoka mwaka 1973 baada ya Mji wa Dodoma
kutangazwa rasmi kuwa Makao Makuu ya Serikali chini ya kifungu cha Sheria
320 ya mwaka 1973. Mwaka huo Wilaya ya Dodoma Mjini iligawanywa na kuwa
Wilaya mbili za Dodoma Mjini na Dodoma Vijijini. Ilipofika mwaka 1980
Wilaya ya Dodoma Mjini ilipandishwa hadhi na kuwa Halmashauri ya Manispaa.
1.6. Wilaya ya Kongwa:
Wilaya ya Kongwa ilianza kujulikana katika ramani ya Dunia mwaka 1913
ambapo Shirika la Kidini kutoka Canada ambalo lilijulikana kama Church
Missionary Society - CMS walipoanza ujenzi wa Chuo cha Ualimu na Theolojia
mwaka 1909 katika Kijiji cha Mlanga.
Kongwa ilipata umaarufu baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia ambapo shirika
moja la Kilimo la Uingereza lilijulikana kama Overseas Food Cooperation
kuanzisha utafiti wa Kilimo cha Karanga mwaka 1947 kwa madhumuni ya
kufufua uchumi wa Kingereza uliokuwa umeathiriwa na Vita Kuu hiyo.
Baada ya miaka miwili yaani 1949 Wilaya hii ilifutwa kutokana na kushindwa
kwa Mradi wa Karanga ambao ulisababishwa na ukosefu wa Mvua kwa miaka
mitatu mfululizo na Shirika la Overseas Food Corporation kufunga shughuli zake.
7
Kabla ya Uhuru, Wilaya ya Kongwa ilikuwa inaongozwa na Watemi au Machifu
wa Makabila ambao ndio walikuwa wanatawala katika maeneo mbalimbli kwa
kurithishana:
• Mtemi Nyamanji alitawala eneo la Pandambili
• Mtemi Mahinyila alitawala eneo la Kongwa
• Mtemi Kasawa alitawala eneo la Mlali
• Mtemi Simango alitawala eneo la Sagara
Mara baada ya Uhuru, mfumo wa Machifu ulibadilika na kuwa wa mfumo wa
Kidemokrasia ambalpo Jamii husika huchagua kiongozi wamtakaye.
Tarehe 23 Juni, 1995 Serikali ilitoa Tangazo la Serikali kuipatia hadhi Kongwa
kwa mara nyingine kuwa Wilaya kamili. Kabla ya hapo Kongwa ilikuwa sehemu
ya Wilaya ya Mpwapwa. Mipaka yake ilitangazwa kwenye Gazeti la Serikali la
tarehe 08 Novemba, 1996 – Tangazo la Serikali Na. 349. Wilaya ina ukubwa wa
kilometa za mraba 4,041. Kiutawala imegawanyika katika Tarafa 3, Kata 22,
Vijiji 74 na Vitongoji 281. Wilaya inajumla ya kaya 50,877 zenye wakazi
wapatao 302,221.
Wenyeji/wakazi wa Wilaya hii ni Wagogo, Wakaguru, Warangi na
Makabilamengine ambayo yalihamia toka sehemu mbalimbali za Tanzania mfano
Wabena, Wanguu, Wangoni, Wakamba na Wamasai ambao walikuja kwa ajili ya
shughuli za kilimo na ufugaji.
1.7. Wilaya ya Chamwino:
Wilaya ya Chamwino ni miongoni mwa Wilaya changa zilizoanzishwa mwaka
2007 kutipia Tangazo la Serikali Na. 190 la tarehe 30 Agusti, 2007 baada ya
iliyokuwa Wilaya ya Dodoma Vijijini kugawanywa.
Wilaya mama ya Dodoma Vijijini ilianzishwa mwaka 1973 kutokana na
kugawanywa kwa Wilaya ya Dodoma na kupatikana kwa Wilaya ya Dodoma
Mjini na Dodoma Vijijini.
Kabla ya Uhuru eneo hili lilikuwa likikaliwa na wenyeji wa kabila la Wagogo
chini ya mabaraza ya Utawala wa Machifu kama ifuatavyo:
• Eneo la Mvumi - Mtemi Mazengo Chalula
• Eneo la Mwitikira - Mtemi Ndoje Muwelewele
• Eneo la Msanga - Mtemi Kolongo Holoholo
8
• Eneo la Buigiri - Mtemi Ndalu Magundu
• Eneo la Makang’wa - Mtemi Tuppa Mbuko
• Eneo la Itiso - Mtemi Hobe Meda
Baada ya Uhuru, Uongozi wa Kichifu ulifutwa rasmi mwaka1963 na kuwekwa
Utawala wa Wakuu wa Wilaya wakisaidiwa na Mabwanashauri. Wenyeji/wakazi
wa Wilaya ya Chamwino ni Wagogo, Wasandawe, Wanguu na Warangi. Pia yapo
makabila mengine yaliyohamia ya Wasukuma na Wamasai ambao wamekuja kwa
shughuli za kilimo na ufugaji.
Shughuli kuu za kiuchumi zinazofanywa na wakazi wa Wilaya hii ni pamoja na
ufugaji wa Ngombe, Mbuzi, Kondoo na Punda. Kwa upande wa kilimo mazao
yanayolimwa ni pamoja na mazao ya chakula ya Mtama, Mahindi na Uwele.
Mazao ya biashara ni Zabibu, Alizeti, Nyonyo na Karanga.
Wilaya ya Chamwino ina ukubwa wa kilometa za mraba 8,056. Kiutawala ina
Majimbo mawili ya Uchaguzi, Tarafa 5, Kata 32, Vijiji 77 na Vitongoji 732.
Wilaya ina jumla ya Kaya 88,282 zenye wakazi wapatao 308,770.
1.8. Wilaya ya Bahi:
Wilaya ya Bahi ni miongoni mwa Wilaya sita za Mkoa wa Dodoma iliyoanzishwa
mwaka 2007 kupitia Tangazo la Serikali Na. 190 la tarehe 31 Augusti, 2007
baada ya kugawanywa kwa iliyokuwa Wilaya ya Dodoma Vijijini na kuwa
Wilaya mbili za Bahi na Chamwino.
Kabla ya Uhuru Wilaya hii ilikuwa ikitawaliwa na Mabaraza ya Machifu
wakisaidiwa na Wapembamoto maeneo ya utawala yalikuwa:
• Eneo la Kinyambwa - Mtemi Makasi Magaga
• Eneo la Luata - Mtemi Nalo Kusila
• Eneo la Bahi - Mtemi Ilotwa Makunzo
• Eneo la Nondwa - Mtemi Mgogo Mamba
Baada ya Uhuru, eneo la Wilaya ya Bahi lilikuwa sehemu ya Wilaya ya Dodoma
kabla ya kugawanywa kwa Wilaya hiyo na kupata Wilaya za Dodoma Mjini na
Dodoma Vijijini mwaka 1973. Ilipofika mwaka 2006 Wilaya ya Dodoma Vijijini
iligawanywa na kupatikana Wilaya ya Bahi.
9
Wilaya hii ya Bahi ina ukubwa wa kilomita za mraba 5,948. Kiutawala Wilaya
inaTarafa 4, Kata 21 Vijiji 56 na Vitongoji 539. Wilaya ina jumla ya kaya 43,310
zenye wakazi wapatao 238,951.
Wenyeji/wakazi wa Wilaya hii ni Wagogo na Makabila mengine ya Wasukuma
na Wamasai ambao walikuja kwa ajili ya shughuli za ufugaji na kilimo.
10
SURA YA PILI
2.0. HALI YA UONGOZI NA UTAWALA
2.1. Uongozi kabla ya Uhuru:
Kabla ya ujio wa Wakoloni, eneo la Ugogo linalojulikana kama Dodoma kwa
sasa lilikuwa likikaliwa na makabila matatu. Kaskazini ya Dodoma wenyeji
waliokuwa wakikaa humo walikuwa ni Wang’omvia. Kabila la pili walikuwa
Wamankala ambao waliishi sehemu yote ya Dodoma Magharibi kuizunguka
mbuga ya Surungayi. Kabila la tatu ni Wayanzi ambalo waliishi sehemu ya
Ugogo ya Manyoni juu.
Baada ya hapo makabila mengine yalianza kuhamia na kuchanganyikana. Wageni
hao baada ya kukaa na wenyeji kwa muda mrefu waliacha desturi za kwao
walikotoka na kubadili majina na kufuata mazoea mapya na kuiga desturi za
wenyeji waliowakuta.
Wakazi waliohamia Ugogo walianza kustawi kwa ukulima na ufugaji wa
wanyama. Baadhi ya makabila kama Wamasai, Wahehe, Wanyamwezi wakaanza
kuwanyemelea na kuwashambulia, Hapo ndipo vita vya makabila vikaanza. Vita
hivi viliendelea kwa miaka mingi.
Wakati Wagogo walipoanza kuwa na Umoja zaidi kwa ajili ya kujiunga ili
washindane na maadui zao, na kuleta mambo ya Ustawi zaidi kuliko
walivyokuwa mwanzo; Wajerumani wakafika na kuwapiga vita Waafrika, na
kujenga Boma lao huko Bagamoyo. Mwanzo Wagogo walikuwa hawana umoja
kamili kwa sababu hawakujuana.
Vita hivyo viliendelea hata Wadachi wakawashinda Waafrika, wakajenga Boma
lao la kwanza Bagamoyo walipotoka huko huko wakapiga vita sehemu hizi za
Dodoma, Wakajenga Boma lao la kwanza Ugogo Mhamvwa (Mpwapwa) na
Kilimatinde. Baadaye wakawaweka Maakida (Makarani wa kudi) kuwa viongozi
wao kwa mambo ya Serikali.
11
Baada ya kujengwa maboma mawili ya kwanza Mpwapwa na Kilimatinde,
likajengwa tena Boma la Dodoma Ugogo katikati na lilifunguliwa mwaka 1912.
Mwaka 1914 vita kuu ya kwanza ilianza baina ya Waingereza na Wadachi na
kumalizika mwaka 1919 ambapo Waingereza walishinda na kuanza kutawala.
Ndipo utawala wa Waingereza ulipofikiria kuwapa uwezo wenyeji kwa kuanzisha
mabaraza ya utawala wa wenyeji.
Hivyo katika Wilaya ya Dodoma yaliundwa mabaraza kumi na nne, Boma la
Kilimatinde (ambalo sasa ni Manyoni) yaliundwa Mabaraza kumi na Boma la
Mpwapwa yakaundwa mabaraza kumi na manne. Jumla ya Mabaraza katika eneo
la Dodoma yalikuwa thelathini na nane (38). Watemi walipowekwa wale
waliobaki wakawa wajumbe ambao waliitwa Wapembamoto. Watemi walipewa
makarani wa Baraza na Matarishi.
2.2. Uongozi baada ya Uhuru:
Vuguvugu la kudai Uhuru katika Mkoa wa Dodoma lina historia ndefu iliyoanzia
mwaka 1939 kilipoanzishwa Chama cha Wafanyakazi cha Wapishi na Maboi
(African Cooks, Washerman and House Servant Association) Historia inaonesha
kufanyika kwa mkutano mkuu wa mwaka wa African Association mwaka 1945
uliohimiza kuanzishwa kwa matawi ya African Association iliyokuja kuwa
chimbuko la Tanganyika African Association (TAA) na baadaye Tanganyika
African National Union (TANU). Maelezo haya yanadhihirisha ushiriki wa
Dodoma kama sehemu anzilishi ya vuguvugu la kupigania Uhuru wa nchi yetu.
Tawi la kwanza la TANU kwa Mkoa wa Dodoma lilifunguliwa mwaka 1955
katika eneo la Barabara ya Nane - Mji Mpya.
Viongozi waanzilishi wa TANU kwa Mkoa wa Dodoma walikuwa. Ndugu
Mahadi K. Makuka, Omary Suleiman, Mzee Kayanda, Mama Kalunde, Abdallah
Mkamba, Said Suleimani, Idd Waziri, Khalfar Khamisi, Bakari Yengeyange,
Swed Athmani na Ramadhani Alli.
Mwaka huo huo wa 1955 ulifanyika uchaguzi wa Jimbo la kati lililohusisha
Mikoa ya Dodoma na Singida. Viongozi waliochaguliwa walikuwa Ndugu,
Alorande Kanyamala, Abdallah Mkamba, Job Lusinde, Omary Selemani na
Haruna Taratibu kabla ya Uhuru.
12
Nchi ya Tanganyika (kwa sasa Tanzania bara) ilikuwa na Majimbo manane (8)
ya Kiutawala Dodoma ndiyo iliyokuwa Makao Makuu ya Jimbo la Kati (Central
province). Baada ya Uhuru, mwaka 1962 Jimbo la kati liligawanywa katika
majimbo mawili ambayo ni Dodoma na Singida na kuitwa Mikoa.
Tokea wakati huo, (1962) Mkoa wa Dodoma umeongozwa na Wakuu wa Mikoa
14 kama ifuatavyo.
Jedwali Na. 2: Orodha ya Wakuu wa Mkoa walioongoza Mkoa wa Dodoma
NA. JINA LA MKUU WA MKOA MWAKA WA KUINGIA MWAKA WA
KUTOKA
1 Bw. John Mwakangale 1962 1967
2 Bw. Wallece Kihampa 1967 1970
3 Bw. John Mhavile 1970 1972
4 Bw. Ibrahim Kajembo 1972 1975
5 Bw. Laurence Mtazama Gama 1975 1979
7 Bw. Christopher Liundi 1980 1985
8 Bibi Anna Abdallah 1985 1987
9 Bw. Athuman Shaidi Kabongo 1987 1993
10 Bw. William Jonathan Kusila 1993 1995
11 Bw. Isidore Leka Shirima 1995 2003
12 Bw. Mussa Ali Nkhangaa 2003 2006
13 Bw. William Vangimembe Lukuvi 2006 2009
14 Eng. Dr. James Alex Msekela 2009 Hadi sasa
2.3. Muundo wa Mkoa ulivyobadilika kuanzia mwaka 1961
• Mwaka 1961 hadi 1962 Mkoa wa Dodoma ulikuwa sehemu ya Jimbo la
Kati Makao Makuu yake yakiwa Dodoma.
• Mwaka 1962 Mkoa wa Dodoma ulianza rasmi ukiongozwa na Mkuu wa
Mkoa akisaidiwa na Katibu wa Mkoa
• Mwaka 1964 mfumo wa utawala wa kutumia Machifu (Watemi) ulifutwa
rasmi na Serikali.
13
• Mwaka 1972 mfumo wa Utawala ulibadilika kwa kuanzisha Madaraka
Mikoani. Katika Mfumo huu, Mikoa ilianzisha Kurugenzi za Maendeleo
za Mikoa na katika Wilaya zilianzishwa Kurugenzi za Maendeleo za
Wilaya. Mkuu wa Mkoa alikuwa ni msimamizi wa Utawala na Maendeleo
akisaidiwa na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Mkoa na Wakuu wa Idara.
Chini yao walikuwepo Wakuu wa Wilaya wakisaidiwa na Wakurugenzi
wa Maendeleo wa Wilaya pamoja na Wakuu wa Idara ngazi ya Wilaya.
Mamlaka za Serikali za Mitaa zilivunjwa.
• Mwaka 1984 Mamlaka za Serikali za Mitaa zilirejeshwa na kuanzishwa
kwa Halmashauri za Miji na Wilaya. Lengo lilikuwa ni kuwapa Madaraka
zaidi wananchi kuamua maendeleo yao. Sheria Na.7 ya mwaka 1982
ilianzishwa Halmashauri za Wilaya na Sheria Na.8 ya mwaka 1982
ilianzisha Halmashuri za Miji.
• Mwaka 1997 Kurugenzi za Mikoa zilifutwa na kuanzishwa Sekretarieti za
Mikoa kwa Sheria Na.19 ya mwaka 1997. Mabadiliko haya yalifanya
Sekretarieti za Mikoa kuwa ni Idara za Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu – TAMISEMI.
2.4. UCHUMI WA MKOA
Kwa ujumla Mkoa wa Dodoma unategemea kilimo na ufugaji ambao unafanyika
katika ngazi ya kaya. Kuna kiwango kidogo cha usindikaji wa mazao ya kilimo na
mifugo.
Kilimo chetu ni cha uzalishaji mdogo ambao unatokana na uhaba wa mvua. Pia
kilimo hiki kwa kiwango kikubwa kinafanyika kwa kutumia jembe la mkono.
Mazao yanayolimwa ni pamoja na Mtama, Uwele, Mahindi, Karanga, Alizeti,
Ufuta na mazao ya jamii ya mikunde.
Mnamo miaka ya 1970 na 1980 mazao ya Zabibu na Mpunga nayo yalianza
kulimwa kama mazao ya biashara.
Kiuchumi Mkoa wa Dodoma ni wa tatu kwa kuwa na mifugo mingi. Ufugaji wa
kuku na Nguruwe nao umeshamiri kwa biashara.
Shughuli nyingine ni mazao ya misitu ufugaji nyuki, uvuvi na madini.
14
Idadi ya wakazi
Idadi ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma imekuwa ikiongezeka kabla na baada ya
Uhuru: Sensa ya kwanza kufanyika kabla ya Uhuru ilifanyika mwaka 1948
ambapo eneo la Dodoma lilikuwa na wakazi wapatao 9,144. Sensa nyingine
ilifanyika miaka minne baadaye yaani mwaka 1952 ambayo ilionyesha kuwa
Dodoma ilikuwa na wakazi Waafrika 9,373, Wahindi 2113, Wazungu 360,
Waarabu 311 na Wasomali 58. Jumla yao ilikuwa 12,219.
Baada ya Uhuru hadi sasa nchi yetu imefanya Sensa ya watu na makazi mara nne:
Sensa zote hizo zimeonyesha kuongezeka kwa kasi kwa wakazi wa Mkoa wa
Dodoma kama inavyoonyeshwa katika jedwali Na.1.
Jedwali Na.3: WAKAZI WA MKOA WA DODOMA 1967 – 2002
MWAKA IDADI YA WAKAZI
1967 709,380
1978 972,005
1988 1,235,328
2002 1,698,996
Pato la Mkoa:
Pato la Mkoa limekuwa likiongezeka mwaka hadi mwaka, mwaka 1991 pato la
Mkoa (GDP) lilikuwa Sh.34.4 Millioni; mwaka 2001 pato la Mkoa lilifikia
Sh.262.955 millioni na mwaka 2010 pato hili limefikia Sh.1,027,508.
Pato la mtu (Per capital) kwa mwaka nalo limekuwa likiongezeka. Mwaka 1991
pato la mtu lilikuwa Sh.92,800 miaka kumi baadaye (2001) pato la mtu lilifikia
Sh.185,599 Hivi sasa 2010 pato hilo ni Sh.486,564.
Pamoja na ukosefu wa mazao ya kudumu ya biashara, inakadiriwa kuwa asilimia
60 hadi 70 ya mapato hayo hutokana na mazao asili ya chakula kama vile
Mahindi, Mtama, Maharage, Uwele, mpunga, mazao ya mbegu za mafuta, mifugo
inachangia asilimia 35 ya pato la Mkoa.
15
SURA YA TATU
3.0. MAFANIKIO YALIYO PATIKANA
3.1. MAJUKUMU NA MALENGO YA MKOA
Kwa mujibu wa Mpango Mkakati wa Mkoa wa mwaka 2011/2012 hadi
2014/2015. Dira ya Mkoa ni kutoa huduma za kiutawala na kitaalamu kwa
Mamlaka ya Serikali za Mitaa pamoja na wadau wengine kwa ajili ya
Maendeleo endelevu. Ili kuhakikisha kuwa lengo hilo linafikiwa, Mkoa
umejiwekea malengo yafuatayo:
• Kusimamia na kudumisha amani na usalama wa Wananchi na mali zao
bila ubaguzi wa aina yeyote.
• Kujenga uwezo kwa watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa ili waweze
kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
• Kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa na wadau wengine kutoa
huduma zilizo bora kwa wananchi.
• Kuwa kiungo cha mawasiliano kati ya Sekretarieti ya Mkoa na Ofisi
ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa; Wizara
mbalimbali; Mamlaka ya Serikali za Mitaa na wadau wengine.
• Kusimamia masuala mtambuka kama vile kuondoa Umasikini,
Utawala Bora, janga la UKIMWI, Mazingira, Maafa, masuala ya
Jinsia na Makundi Maalum.
• Kuainisha vivutio vya uwekezaji na vipaumbele katika kukuza
uzalishaji katika kilimo kupitia dhana ya KILIMO KWANZA kwa
kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu. TAMISEMI, Wizara, Mamlaka
ya Serikali za Mitaa na Wadau.
• Kuongeza uwezo wa utoaji huduma bora za TIBA na KINGA katika
Hospitali ya Mkoa.
16
3.2. MAENDELEO YA KISEKTA
3.2.1. SEKTA YA AFYA
UTANGULIZI
Huduma za Afya Mkoani Dodoma zimekuwa zikitolewa kabla ya Uhuru na baada ya
uhuru. Zimetolewa kwa kiwango cha kuridhisha kulingana na uwezo wa nchi kulingana
na wakati. Upatikanaji wa huduma za afya kwa karibu kwa wananchi umekuwa
ukiongezeka kulingana na uwezo wa nchi. Hali kadhalika afya ya wananchi imekuwa
ikiboreshwa taratibu kutokana na changamoto zinazojitokeza katika nyakati mbalimbali.
Mji wa Dodoma ulianza kujengwa na wakoloni wa Kijerumani mwaka 1912 ambapo wao
waliamua Dodoma iwe makao makuu yao sababu upo katikati na sababu za kiusalama.
Huduma za Afya kabla ya Wakoloni :
Huduma za Tiba asili zilitolewa na waganga wa Jadi ambao walitoa huduma za tiba kwa
kutumia mitishamba (mizizi, majani, miti na gamba) pia walitoa huduma za kinga kwa
kutabiri au kuagua kuchanja chale / dawa. Huduma za wazazi zilitolewa na wakunga wa
jadi.
Huduma za Afya baada ya Wakoloni kuingia:
Wakoloni walipoingia walikuja wamisionari kueneza dini lakini pia walitoa huduma za
Afya kwa wazungu na waafrika wachache waliokuwa karibu yao. Taratibu wakaanza
kuzipanua na kujenga vituo hatimaye Zahanati zilizotoa huduma za Afya kwa mfumo wa
kisayansi. Vituo mbalimbali vilianzishwa na Wamisionari hawa kama ifuatavyo:-
Hospitali ya Mvumi:
Hospitali hii ilianza kama kituo/Zahanati kwa Wamisionari mnamo mwaka 1922,
polepole ikapanuka kuwa kituo cha Afya na hatimaye Hospitali ikiendeshwa na Kanisa la
Anglikana. Iliimarika na hatimaye Wilaya ya Dodoma Vijijini kwa wakati huo ikawa
inaitumia kama Hospitali Teule ya wilaya. Kutokana na mabadiliko ya Sera ya Afya ya
kutaka kuimarisha huduma za afya wadau mbalimbali,watu binafsi na madhehebu ya dini
Hospitali walishirikishwa. Hivyo, hospitali hii kwa sasa hupatiwa fedha za kusaidia
kuiendesha, watumishi wanalipiwa mshahara na Serikali na kuna vyuo vya mafunzo
17
vinatoa mafunzo ya uganga, uuguzi na maabara kwa kushirikiana na serikali.Wamisionari
walijenga zahanati zingine za kutolea huduma kama Itiso,Bahi,Mlowa Bwawani na
Chikopelo. Serikali baada ya uhuru ilijenga vituo vya afya 6 zikiwemo Chipanga, Mtitaa,
Handali, Mundemu, Chamwino na Haneti na pia ikajenga zahanati nyingi.Wilaya ya bahi
kwa sasa ina vituo vya afya 6 na zahanati 29. Wilaya ya Chamwino ina vituo vya afya 5
na zahanati 53
Hospitali ya Kongwa:
Hospitali ya Kongwa ilijengwa mwaka 1948 -1949 na wazungu waliojenga Chuo cha
Kimisionari cha St.Philp. Hospitali hii ilitegemewa na wakazi wa Afrika Mashariki
kwani ilikuwa na Madaktari bingwa na majengo megi, pia Chuo cha Afya kilikuwepo
katika Hospitali hiyo. Hospitali hiyo ililenga kutoa huduma kwa masetla pamoja na
wafanyakazi wao wa kampuni ya Overseas Kongwa waliokuwa wanalima karanga katika
eneo hilo.Mwaka 1959 masetla walifunga shughuli za kilimo cha karanga. Mwaka 1961
hospitali ilibadilishwa kuwa Kituo cha Afya. Vituo vya afya Mlali na Mkoka viilijengwa
baada ya Uhuru.Baada ya Wilaya ya Kongwa kuanziashwa mwaka1995 Kituo cha afya
kikabadilishwa kuwa Hospitali ya Wilaya na majengo mbalimbali yakaanza kujengwa na
kuzinduliwa rasmi mwaka 1998 na Rais Benjamin William Mkapa. Wilaya hii kwa sasa
ina Hospitali moja, Vituo vya Afya 3 na Zahanati 42.
Hospitali ya Mpwapwa:
Mwaka 1928 mwezi Mei, Zahanati ya Mpwapwa ilianza rasmi kujengwa na kukamilika
mwaka 1930. Hospitali ya Wilaya Mpwapwa ilianza kujengwa mwaka 1962 mwezi Mei
kwa kuanza na majengo ya wagonjwa wa nje (OPD), Wodi Na. 2,3,4 na 7, Chumba cha
upasuaji, jiko, sehemu ya kufulia, chumba cha stoo na jengo la mionzi (X-Ray). Majengo
mengine yaliendelea kujengwa hatua kwa hatua hadi kufikia hali hii ya sasa.
Hospitali ya Wilaya Mpwapwa ilianza kujengwa mwaka 1962 mwezi Mei kwa kuanza na
majengo ya wagonjwa wa nje (OPD), Wodi Na. 2,3,4 na7, Chumba cha Upasuaji, Jiko,
sehemu ya Kufulia, chumba cha Stoo na Jengo la Mionzi (X-Ray). Majengo mengine
yaliendelea kujengwa hatua kwa hatua hadi kufikia hali hii ya sasa.
Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa ilifunguliwa rasmi 08/05/1963 ikiwa na watumishi 49
ambao kati yao 14 waliajiriwa na Wizara ya Afya makao makuu na 35 waliajiriwa na
Wilaya. Vifaa mbalimbali vililetwa toka Wizarani na vingine vililetwa toka Hospitali ya
18
Overseas Kongwa ambayo ilibadilishwa na kuwa Kituo cha Afya katika mwaka 1961
baada ya wenye mashamba ya karanga kufunga shughuli zao mwaka 1959 na kuondoka.
Aidha, vituo vingine vilivyokuwepo ni vituo vidogo vya matibabu vilivyokuwa katika
maeneo ya wamisionari ambavyo ni Lumuma RC kilichoanzishwa mwaka 1965 na
Kibakwe RC mwaka 1968. Vituo hivyo vilikuwa vikitoa huduma za tiba ndogo ndogo za
wagonjwa wa nje na kutoa rufaa kwa wagonjwa waliokuwa na matatizo makubwa. Baada
ya uhuru serikali ilijenga vituo vya afya Kibakwe na Rudi na zahanati nyingi. Kwa sasa
wilaya ina zahanati 49 na Vituo vya Afya 3. Mkakati wa kujenga zahanati kwa kila kijiji
na kituo cha afya kwa kila kata unatekelezwa.
Wilaya ya Kondoa:
Wilaya hii kwa sasa ina Hospitali moja ambayo ni ya Wilaya, Vituo vya Afya 5 na
zahanati 68.
Wilaya Dodoma Mjini
Wilaya ya Dodoma ina Hospitali 4 Vituo vya Afya 10 na Zahanati 52 kwa sasa.
Hospitali ya Mkoa
Hospitali ya Mkoa ilikamilia kujengwa mwaka 1927 kama kituo cha majeruhi wa kivita.
Ilianza na Majengo ya mawe machache yakaongezeka kidogo kidogo mfano OPD, Jengo
la utawala, maabara (ambayo sasa ni jengo la Meno), chumba cha kuhifadhi maiti
(ambayo sasa ni sub store ya pharmacy), jiko na Ofisi ya Muuguzi Mkuu, wodi No. 5, 6,
7, 8, 9, 10 na wodi 12 (ilijengwa itumike kama Staff Quarter.) Mwaka 1959 ilifanywa
kuwa Hospitali ya Jimbo. Kuanzia mwaka 1976 Wodi zingine ziliongezeka mfano Wodi
1, 2, 3, 4 na mwaka 1979 ilijengwa Wodi ya Daraja la Kwanza ya Wanaume na
Wanawake ambayo sasa ni Wodi ya Watoto Na. 13 na 14. Wodi 16 iliyokuwa ya Watoto
ilibadilishwa ikawa Daraja la Pili na watoto kuhamishiwa Wodi 13 na 14. Mwaka 2000
ilijengwa Wodi ya Daraja la Kwanza.
Wakati wa ukoloni Hospitali ya Grade I kwa wazungu ilikuwa katika ofisi za Stamico
(madini), Jengo moja katika hospitali ya Mkoa (Wodi 10 kwa sasa) lilitumika kama
Daraja la Pili kwa Waasia (Wahindi na Waarabu).
Huduma za Afya ya Mama na mtoto nazo zilitolewa katika jengo la chanjo kwa sasa,
kabla ya hapo lilikuwa Bweni la wanafunzi wa Rural Medical Aid waliokuwa wakisoma
katika Hospitali ya Mkoa. Daktari mwanzilishi wa hospitali hii alikuwa Dr Blackhood
19
(mzungu) ambaye alishirikiana Sr Elizabeth kama Muuguzi mkuu wa hospitali. Alijenga
zahanati nyingi zikiwemo Itiso, Handali na Mwitikira. Moja ya Waafrika wa kwanza
kufanya kazi General Hospital alikuwa Mama Mwashongo Mwinyimkuu ambaye
alijitolea akajenga jengo kwa akina mama (Mwashongo clinic).
Waganga wakuu wengine walioingoza Hospitali hii ni Dr Mtawali, Dr Kheri, Dr Nkinda,
Dr Sadiki, Dr J. Tesha, Dr J. Temba, Dr G. Upunda, Dr Mbogo, Dr M. Massi, Dr J.
Mtimba, Dr F. Mokiti, na anayeiongoza kwa sasa Dr G. Mtey.
Huduma za Afya baada ya Uhuru:
Serikali ilipoingia madarakani ilianzisha sera ya kupambana na Ujinga, Maradhi na
Umasikini. Hapakuwa na sera ya Afya, mipango yote ililenga kupunguza maradhi na vifo
kama sera ya Taifa. Sera rasmi ya Afya ilianza kupatikana mwaka 1990 na ikaboreshwa
mwaka 2007.
Serikali ya awamu ya kwanza iliyoongozwa na Hayati Mwl J. K. Nyerere ilijengwa
zahanati na vituo vingi ili kuwasogezea wananchi huduma za Afya. Kazi ilikuwa rahisi
hasa pale wananchi walipoishi katika Vijiji vya Ujamaa baada ya Azimio la Arusha.
Wananchi wengi walifikiwa na huduma za Afya zikiwemo kinga na Tiba. Hata hivyo
changamoto nyingi pia zilijitokeza ikiwemo ukosefu wa watumishi, madawa, vifaa na
majengo kutotosheleza.
Huduma za kinga mbalimbali zilifanyika ikiwemo utoaji elimu ya Afya kwa wananchi,
na usafi wa mazingira. Kampeni za aina mbalimbali zilifanyika mfano:-
‐ Mtu ni Afya iliyoimarisha usafi wa mazingia na matumizi ya vyoo
‐ Kampeni za Chanjo - UCI, Polio na Surua
‐ Kampeni za Vit A, na dawa za Minyoo
Zote hizo zililenga kupunguza ama kutokomeza magonjwa. Moja ya mafanikio ya
huduma za kinga ni kutokomeza ugonjwa ndui mwaka 1979. Magonjwa ya kuambukiza
mengi yanaendelea kupungua mfano Kipindupindu n.k.
20
Sera ya Mabadiliko ya Utoaji Huduma za Afya:
Kutokana na changamoto zilizokuwa zinajitokeza katika utoaji huduma za afya Wizara
ya afya ilifanya mabadiliko. Huduma zikawa za kuchangia ili kuongeza fedha za
kununulia dawa, mabadiliko haya yalilenga kuboresha huduma za Afya kwa
kuwashirikisha wadau na watu mbalimbali na wananchi. Watu binafsi na taasisi za kidini
zilishirikishwa. Mikakati mbali mbali ilianzishwa kama vyanzo vya mapato ya kuboresha
huduma za Afya. Njia hizo ni pamoja na wafanyakazi kuwa na Bima ya Afya, wananchi
wa kawaida kuchangia kupitia uchangiaji wa papo kwa papo(Cost Sharing) na Mfuko ya
Afya jamii. Mikakati hii imeboresha upatikanaji wa dawa, vifaa na majengo. Mabadiliko
ya utoaji huduma za afya pia yalitilia mkazo ushirikishwaji wa watu binafsi na pia ubia
kati ya serikali na mashirika ya dini.
Hali ya Watumishi wa Afya:
Moja ya tatizo kubwa ni upungufu wa watumishi wa afya ambapo Wizara imejenga vituo
vya mafunzo vya kada mbalimbali kwa lengo la kuongeza watumishi wa Afya kila
mwaka. Kada mbalimbali zinaongezeka taratibu kila mwaka. Hali ya Watumishi kwa
mwaka 2009 ni kama ifuatavyo:-
21
Jedwali Na. 4: Watumishi waAfya Kiwilaya:
Kada
Chamwino Bahi Kondoa Mpwapwa Kongwa Dodoma Manispaa
hita
jika
wali
opo
pung
ufu
hita
jika
wali
opo
pun
guf
u
hita
jika
wali
opo
pungu
fu
hitajika wali
opo
pun
gufu
hita
jika
wali
opo
pung
ufu
hitajika waliopo pungu
fu
M/specialist 1 1 0 1 1 0 1 1 0 1 0 1 1 0 1 1 1 0
MD 1 1 0 1 1 O 3 1 2 2 1 1 3 2 1 115 14 101
AMO 10 6 4 6 3 3 10 6 4 11 11 0 14 8 6 44 25 19
COs 135 57 78 74 28 46 117 52 65 91 47 54 92 54 38 68 52 14
Dentist 2 1 1 1 1 0 1 1 0 1 1 0 1 0 1 6 5 1
NM 115 81 34 116 56 70 121 79 42 103 62 41 139 87 52 161 74 87
PHN 52 24 28 35 4 31 16 13 3 90 15 75 39 5 34 119 77 42
Lab tec 25 6 19 12 6 6 4 1 1 0 16 12 4 19 4 15
Pharmacist/asst 1 1 0 6 2 4 9 0 9 1 1 0 1 1 0 2 3 0
HO/HAs 32 13 19 21 9 12 40 7 33 35 15 20 25 4 21 37 17 20
HS 1 1 0 1 1 0 2 2 0 2 2 0 1 1 0 1 1 0
ACC 6 1 5 6 0 6 2 0 2 2 2 0 1 1 0 1 2 0
Jumla kiwilaya 282 193 188 280 112 178 322 176 160 348 158 192 333 175 159 538 275 299
JUMLA
kimkoa
Hitajika=2,103 Waliopo=1,089(52%) Pungufu=906(48%)
Chanzo:Taarifa za PHC za Wilaya mwaka 2010 na CCHP 2010/2011
22
Kusogeza Huduma karibu na Wananchi
Serikali ya awamu ya nne imeagiza ujenzi wa Zahanati kwa kila kijiji na Kituo cha Afya kwa
kila Kata uwe umekamilika ifikapo mwaka 2015. Hospitali za Mikoa zinaboreshwa kuwa za
Rufaa. Katika Hospitali ya mkoa upanuzi unaendelea ambapo majengo ya ghorofa kwa ajili
ya akina mama na Bima ya Afya yanakaribia kukamilika. Ujenzi wa zahanati na vituo vya
Afya nao unaendelea.
Hali ya vituo vya kutolea huduma za Afya mkoani ni kama ifuatavyo katika jedwali
lifuatalo:-
Jedwali Na. 5: Idadi ya Vituo vya Afya:
Kituo Serikali Madhehebu ya dini Mashirika Binafsi Jumla
Zahanati 240 31 7 15 293
Vituo vya afya 26 6 0 1 33
Hospitali 5 3 0 0 8
Jumla 271 40 7 16 334
Matatizo
• Idadi ya watu inayoongezeka kwa kasi ni changamoto
• Magonjwa mapya yanazuka mfano ebola, mafua ya ndege ukimwi n.k.
• Mfumo wa utoaji huduma za afya haujakidhi mahitaji.
• Upungufu wa fedha za kuendeshea huduma za afya.
• Upungufu wa watumishi,vifaa madawa na majengo
Mafanikio yaliyopatikana
• Idadi ya Zahanati, vituo vya Afya na Hospitali vimeongezeka kufikia 334 (angalia
jedwali hapo juu).
• Chanjo kwa watoto na wazazi imefikia asilimia 90
• Jedwali Na. 6: Kiwango cha Chanjo kwa Watoto na Wazazi 2007 hadi 2010:
MWAKA AINA YA CHANJO
BCG DPTHbHib SURUA
2007 96% 99% 90%
2008 98% 95% 94%
2009 100% 93% 95
2010 94% 93% 93%
Lengo la kitaifa=90%
23
• Vifo vya watoto wachanga vimepungua hali kadhalika vifo vitokanavvyo na uzazi
vimepungua kama ifuatavyo:-
Jedwali Na. 7: Kiwango cha Vifo wa watoto wachanga na Vifo vya Uzazi 2007 hadi
2010:
MWAKA VIFO
VITOKANAVYO
NA UZAZI
VIFO VYA
WATOTO
WACHANGA
VIFO VYA
WATOTO
CHINI YA
MWAKA 1
VIFO VYA
WATOTO CHINI
YA MIAKA 5
2007 168/100,000 LB 8/1000 23/1000 65/1000
2008 124/100,000 LB 11/1000 22/1000 45/1000
2009 122/100,000 LB 9/1000 19/1000 40/1000
2010 127/100,000 LB 10/1000 20/1000 38/1000
• Sababu zilizopelekea kupunguza vifo vya watoto na mama wajawazito ni pamoja na:
‐ Kuboreshwa kwa huduma za rufaa ambapo kila Kituo cha Afya kina gari la
wangonjwa. Huduma za Upasuaji zimeanza kutolewa katika Vituo vya Afya
‐ Kujengwa kwa Chigonela (nyumba za kujingojelezea mama wajawaszi wenye
matatizo katika Vituo vya Afya na Hospital za Wilaya
‐ Kununuliwa kwa vifaa vya kutolea huduma ya uzazi kwenye kila kituo
‐ Watumishi wanaotoa huduma za uzazi kupatiwa mafunzo
‐ Kushirikisha jamii katika masuala ya uzazi/ujauzito
• Kina mama wanaotumia uzazi wa mpango wameongezeka na pia wanaojifungulia
vituoni imeongezeka
Jedwali Na. 8: Kiwango cha Akinamama wanaotumia Uzazi
2007 hadi 2010:
MWAKA ASILIMIA WANAOJIFUNGULIA
VITUONI
2007 57%
2008 65%
2009 67%
2010 69%
Takwimu za kitaifa =53%
• Coverage ya vyoo ni 86% kwa choo cha aina yoyote na 25% vyoo bora
• Milipuko ya magonjwa ya kuambukiza kama kipnidupndu imepungua
• Elimu ya Afya inaendelea kubadili tabia na mienendo ya wananchi,
• Mfumo wa rufaa umeboreshwa.kila kituo cha afya kina gari la wagonjwa kwa sasa
24
• Upatikanaji wa dawa muhimu kadhalika umeimarishwa kwa kutoa makasha ya dawa
muhimu kwa kila kituo cha huduma
Matarajio ya baadaye:
• Kuongeza watumishi wenye ujuzi ili kukidhi mahitaji kwa kila Kituo
• Kukamilisha ujenzi wa Zahanati kwa kila Kijiji na Kituo cha Afya kwa kila kata
• Kununua vifaa tiba, vitendanishi na madawa ya kutosha kwa kila Kituo cha kutolea
huduma za Afya
• Kubuni na kutekeleza mikakati ya kupunguza magonjwa na vifaa yanayoikabili jamii
Attachment: picha mbali mbali
25
JENGO LA OPD LILIVYO SASA BAADA YA UKARABATI
26
MAJENGO YA ZAMANI YA MAWE YALIYOJENGWA MWAKA 1927
27
JENGO LA MAABARA LIMEBORESHWA NA KUWA LA KISASA
28
MAABARA IMEPATIWA VIFAA VYA KISASA
29
JENGO JIPYA LA WAZAZI LINAJENGWA ILI KUPUNGUZA MSONGAMANO
UNAOSABABISHA KULALA WAWILI WAWILI AU ZAIDI
30
MFUKO WA BIMA YA AFYA UNABORESHA HUDUMA KWA WATEJA WAKE
KWA KUJENGEA OPD YA KISASA
WAGONJWA WAKIHUDUMIWA NA MADAKTARI NA WAUGUZI. HUDUMA
ZINAENDELEA KUBORESHWA KWA KUONGEZA WATUMISHI, VIFAA NA
MADAWA
31
HUDUMA ZA USAFI WA MAZINGIRA, CHAKULA NA ULINZI
ZIMEBINAFSISHWA ILI KUIPUNGUZIA MZIGO SEREKALI ILI ZIBORESHWE
32
3.2.2. HOSPITALI YA MIREMBE NA TAASISI YA ISANGA:
1.0. UTANGULIZI:
Huduma kwa wagonjwa wa akili zilianzishwa na Wamisionari wa Kijerumani
toka mji wa Bethel huko Lutindi - Tanga mwaka 1888. Wakati huo wananchi
walio wengi waliamini kwamba, wagonjwa wa akili walipagawa na mashetani
kwa hiyo tiba yao ilifanywa na waganga wa jadi au maombi kwa waumini wa
dini. Imani hizo zipo mpaka leo. Mgonjwa wa kwanza kulazwa katika kituo
cha Lutindi aliitwa Bibi Mkambenga akifuatiliwa na wagonjwa wengine kwa
awamu kwa jinsi wananchi walivyoendelea kuelimika. Baada ya vita kuu ya
kwanza ya dunia, kituo hicho kiliendelea kuhudumia wagonjwa wa akili chini
ya utawala wa Serikali ya kikoloni ya Mwingereza.
1.1. KUJENGWA KWA HOSPITALI YA MIREMBE (1925 - 1926):
Umuhimu wa huduma kwa wagonjwa wa akili ulifanya Serikali ya kikoloni ya
Waingereza ianzishe Hospitali ambayo ingetoa huduma kwa nchi nzima. Mji
wa Dodoma ulichaguliwa kwa kuwa ulikuwa katikati ya nchi na ulifikika kwa
urahisi kwa kutumia reli ya kati na barabara kuu ya kaskazini (The Great
North Road). Mwaka 1925 Hospitali ya Mirembe ilianza kujengwa na
kufunguliwa mapema mwaka 1927 ikiwa na jumla ya wagonjwa 29
waliohamishwa toka kituo cha Lutindi. Tokea wakati huo mpaka sasa
Hospitali ya Mirembe ni maalum Tanzania bara kwa kutoa huduma za Afya ya
Akili na utengemao wa mienendo ya wagonjwa wa akili. Wakati Hospitali
ilipofunguliwa, hapakuwepo wataalamu wazalendo katika fani ya magonjwa
ya akili. Kutokana na hali hii viongozi wa Hospitali kwa kipindi kirefu
walikuwa wageni (Waingereza) ambao waliendesha huduma kwa uzoefu
wakitumia dawa ya aina moja iliyoitwa “Paraldalyde”. Dawa hiyo haikuweza
kumtuliza mgonjwa wa akili inavyostahili na hivyo wagonjwa wengi walikaa
hospitalini kwa muda mrefu na kusababisha msongamano.
1.2. KUJENGWA KWA TAASISI YA ISANGA (1948 – 1950)
Mara baada ya vita vikuu vya pili vya dunia 1945 tatizo la wagonjwa wa akili
wahalifu (Criminal Mental Lunatics) liliongezeka na kusababisha Serikali ya
Kikoloni ya Mwingereza kujenga kituo/gereza la kuhudumia wagonjwa wa
akili wahalifu karibu sana na Gereza Kuu la Isanga. Kituo hicho kilifunguliwa
33
mwaka 1950 na kupewa jina la “Broadmoar” kwa kuwa huduma zake
zilifanana na gereza la jinsi hiyo lililopo nchini Uingereza. Taasisi hii ilianza
na wagonjwa 60 ikiwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ikiendeshwa
kama sehemu ya gereza. Mwaka 1960 Dk. Smart (Mwingereza) aliishauri
Serikali ya kikoloni iboreshe huduma za kituo cha Broadmoar kwa kubadili
umiliki wake ili kiendeshwe kama Hospitali ya Huduma za Afya ya Akili
chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Wazo lake lilikubalika na
mwaka 1961 Broadmoar ilikabidhiwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
iliweka kituo hicho chini ya Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mirembe kwa
kuwa moja ya majukumu yake ni kutoa tiba na utengemao wa afya ya akili.
Kuanzia hapo hadi sasa taasisi ya Isanga imekuwa sehemu ya Hospitali ya
Mirembe ikitoa huduma kwa wagonjwa wa akili wahalifu wanaoletwa hapo
kisheria.
1.3. HOSPITALI YA MIREMBE KABLA YA UHURU (1926 – 1959)
Hospitali ilianza na wagonjwa 29 mwaka 1927 hadi kufikia wagonjwa 616
mwaka 1961. Mganga Mkuu wa kwanza mtaalam wa magonjwa ya akili
aliitwa Dr. Mackay (Mwingereza) ambaye alifanya kazi kwa kipindi cha
miaka 2 tu (1950 – 1951) kisha alipokelewa kazi na Dk. Smart (1951 – 1961)
ambaye ndiye aliyetoa ushauri kwa Serikali ya Kikoloni ya Mwingereza
kukabidhi kituo cha Broadmoar kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Katika kipindi hicho, wagonjwa wa akili wahalifu walikuwa wakifungiwa
katika magereza huku wakilundikana pasipo huduma yoyote ya kiganga.
Walikuwa hawapendwi kwa kuwa walikuwa wasumbufu na kero kwa
wafungwa wenzao na askari waliowalinda. Wengi wao walidhaniwa
wamepagawa au wamepandwa na mashetani na hivyo, walipigwa, walifungwa
kamba hata kunyimwa chakula ili kupunguza nguvu zao za kusumbua.
1.4. HOSPITALI YA MIREMBE BAADA YA UHURU (1961 – 1976)
Kati ya mwaka 1961 na 1976 kulikuwa na ongezeko la wagonjwa kuanzia 616
(1961) hadi wagonjwa 2,555 (1976). Idadi hii ya wagonjwa ilikuwa inatisha
na hali hiyo ilileta madhara makubwa kwa wagonjwa, familia zao na taifa kwa
ujumla kwa sababu zifuatazo:
34
(i) Ilikuwa gharama kubwa kuwasafirisha wagonjwa kutoka
wanakoishi hadi Mirembe
(ii) Baada ya kulazwa hospitalini, wagonjwa hawakuwa na fursa ya
kuwasiliana na ndugu zao
(iii) Kutokana na msongamano, upungufu wa wataalamu na ufinyu
katika upatikanaji wa dawa, wagonjwa wengi walikosa huduma
inayostahili na kuchukua muda mrefu pasipo kupona au kupata
nafuu. Baadhi yao walipata maambukizi ya maradhi mapya
yaliyosababisha vifo.
Mwaka 1961 – 1965 Dk. Sell (Daktari Bingwa wa magonjwa ya akili) –
Mwingereza alichukua nafasi ya Dr. Smart kama Mganga Mkuu wa Hospitali.
Katika kipindi hicho, kuliwa na mabadiliko ya utoaji huduma za dawa
kwakuwa dawa mpya aina ya “Iargactil na serenace” zilianza kupatikana na
kutumika na shughuli za kazi za mikono (Occupational therapy) kwa
wagonjwa ziliaza. Mwaka 1965 – 1969 Dr. Williams (Mhindi) alichukua
nafasi ya Dk. Sell kama Mganga Mkuu wa hospitali. Huyu alianzisha huduma
kwa wagonjwa wenye kifafa kwa kutumia dawa mpya ya “zerontine na
ethosuximole” huku akiendeleza shughuli za kazi za mikono yaani kilimo cha
bustani za mboga na ufugaji wa nguruwe.
Mwaka 1967 kituo cha marekebisho ya wagonjwa wa akili wa muda mrefu
(Mirembe Annex) kilifunguliwa kwa madhumuni ya kuwahudumia wagonjwa
wa akili ambao wamepoteza mawasiliano na ndugu/jamaa au wanahitaji
kusindikizwa kwenda nyumbani kwao na wahudumu wahospitali au
wanahitaji matibabu ya muda mrefu. Mwaka 1969, Dr. Pendaeli (Daktari
Bingwa wa magonjwa ya akili) alikuwa daktari wa kwanza Mtanzania
mzalendo kushika nafasi ya juu ya uongozi na utaalamu katika Hospitali ya
Mirembe. Aliripoti toka masomoni Uingereza na kuchukua nafasi ya Dk.
Williams kama Mganga Mkuu wa hospitali. Huyu aliimarisha tiba
zilizokuwepo ikiwa ni pamoja na shughuli za kazi za mikono.
35
1.5. MABADILIKO YA UONGOZI KATIKA HOSPITALI YA MIREMBE:
Yamekuwepo mabadiliko mbalimbali ya Uongozi kastika Hospitali ya
Mirembe kwa vipindi tofauti kama ifuatavyo: Mwaka 1972 - 1976 Dk.
Rugeiyamu, 1976 – 1978 Dk. Mziray, 1978 – 1986 Dk. Ngonyani, 1989 –
1995 Dk. P. B. Mtey na 1995 – Januari 30, 2011 Dk. J. E. Nkya. Aliyepo sasa
ni Dk. E. Mndeme (Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili).
1.6. MABADILIKO YA HUDUMA ZA AFYA YA AKILI:
Mwaka 1970 Wizara ya Afya ikishirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO)
ilianzisha Programu ya Kitaifa ya Afya ya Akili (National Mental Health
Program) kwa kutoa mafunzo na kufungua vitengo vya afya ya akili katika
hospitali za Mikoa. Hatua hii ilipunguza msongamano wa wagonjwa katika
Hospitali ya Mirembe na kuimarisha huduma kwa wagonjwa. Mwaka 1973
kilianzishwa Chuo cha Uuuguzi wa Afya ya Akili Mirembe (Mirembe
Psychiatric School of Nursing) ambacho kimekuwa kikitoa mafunzo maalumu
ya uuguzi kwa wagonjwa wa akili kwa waugunzi walio kazini kama mafunzo
ya kujiendeleza. Wauguzi hawa wanapohitimu wanategemewa kuimarisha
huduma kwa wagonjwa wa akili kwenye vitengo vilivyoanzishwa katika
hospitali zao. Mpango huu umesaidia wagonjwa wengi kuhudumiwa karibu na
nyumbani kwao na wale waliokuwa wamekaa muda mrefu katika hospitali ya
Mirembe walirudishwa nyumbani kwao ili waendelee na matibabu katika
vituo vilivyopo karibu. Mabadiliko katika huduma za Afya ya Akili
tunayafafanua kama ifuatavyo
(i) Hospitali ya Mirembe:
Kwa sasa, Hospitali hii ina vitanda vinavyotumika 500.
Inahudumia wagonjwa wa akili raia ambao wengi wao hupokelewa
kama wagonjwa wa rufaa toka Hospitali za Wilaya na Hospitali za
Mikoa Tanzania nzima. Baadhi ya wagonjwa huletwa na jamaa zao
pasipo kupitia kwenye kituo chochote cha tiba. Kwa sasa, hudma
za magonjwa ya akili zimeoanishwa na huduma za Afya ya Msingi
katika hospitali ya mirembe kwa kuimarisha huduma za matibabu
kwa magonjwa ya kawaida ya kimwili. Huduma hizi zinajumuisha
wagonjwa wa nje (OPD), wagonjwa wa ndani (IPD), huduma za
uchunguzi wa Maabara Eksirei, EEG na Ultra-sound. Pia, Hospitali
36
inatoa ushauri nasaha na kupima kwa hiyari magonjwa ya
kuambukiza kama UKIMWI na magonjwa ya NGONO, huduma za
CTC (Care and Treatement Centre) kwa waadhirika wa UKIMWI,
kupima na tiba kwa wagonjwa wa Kifua Kikuu. Wastani wa siku
za kulazwa wagonjwa wa akili ni siku 60.
(ii) Taasisi ya Isanga:
Kituo kilikabidhiwa kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na
kubadilishwa jina kutoka “Broadmoar” kuwa “Isanga Institution”
mwaka 1961 kama sehemu ya Hospitali ya Mirembe. Kwa sasa
kituo hiki ni Idara ya “Forensic Psychiatry” ya Hospitali ya
Mirembe. Magereza au Jeshi la Polisi kwa ajili ya matibabu au
uchunguzi wa afya ya akili wakati alipofanya uhalifu au matibabu
na utengemao wa Afya ya Akili kwa muda mrefu usiopungua
miaka mitatu. Muda wa kulazwa na kupata matibabu katiika kituo
hiki kisheria ni miaka 3.
(iii) Mirembe Annex:
Kituo hiki hutunza wagonjwa wa akili waliopona au waliopata
nafuu lakini hawakumbuki nyumbani kwao au wanahitaji
wasindikizwe na Muuguzi au jamaa/ndugu zao kurudi
nyumbani.hapa wanaendelea na matibabu wakati wanaposubiri
taratibu za kuwarudisha nyumbani. Kituo hiki kina uwezo wa
vitanda 50. Wastani wa muda wa kukaa wagonjwa katika kituo hiki
ni kati ya miezi 3. Kwa sasa huduma za kituo hiki zimehamishiwa
katika Hospitali ya Huduma za Afya ya Akili Mirembe kutokana
na tatizo la upungufu wa watumishi.
(iv) Kijiji cha Hombolo:
Kituo hiki kipo katika Kijiji cha Hombolo kilichopo Km. 50 nje ya
Mji wa Dodoma. Hapa, wagonjwa wa akili waliopona au waliopata
nafuu lakini wenye matatizo ya kijamii ya kutokukubalika
nyumbani kwao kutokana na uhalifu waliofanya wakati wakiwa
wagonjwa, hupewa mafunzo ya kazi za kilimo na ufugaji
kuwaandaa kujitegemea. Hakuna muda maalum wa kukaa katika
37
kituo hiki. Aidha, mgonjwa anapokuwa tayari huruhusiwa
kuondoka kituoni na kuanzisha makazi yake kwa kujitegemea.
(v) Chuo cha Uuguzi Mirembe:
Chuo kilianzishwa Julai 1973, madhumuni ya kuazishwa Chuo hiki
ni kutoa mafunzo ya Uuguzi wa Afya ya Akili, ambapo hapo awali
mafunzo hayo yalitolewa nje ya nchi. Toka 1973 mpaka 2007
mfumo wa mafunzo umekuwa ukibadilika. Awali mafunzo
yalikuwa ni ya Uuguzi daraja la “B” lakini sasa ni daraja la “A”
kwa ngazi ya Stashahada na Stashahda ya juu kwa muda wa miaka
2 kila ngazi. Mwaka 2008 chuo kilipokea wanafunzi watarajali wa
kwanza wa mpango wa MMAM. Pia chuo ni kituo cha mafunzo ya
kujiendeleza Kanda ya kati yenye Mikoa miwili Dodoma na
Singida. Tangu chuo kianzishwe idadi ya wanafunzi wahitimu
imeongezeka toka 17 hadi 1,311. Kwa mwaka 2010/2011 chuo
kina wanafunzi wa aina mbili ya Stashahada na Stashahada ya juu.
Stashahada:
(a) Wanafunzi wa stashahada ya Uuguzi na uuguzi wa Afya ya
Akili – mafunzo ya kujiendeleza (In service) mafunzo ya miaka
2, jumla yao ni 93
(b) Wanafunzi watarajali wa mpango wa MMAM mwaka wa pili
na wa kwanza jumla yao ni 67
Stashahada ya juu:
Uuguzi wa Afya ya Akili (Advanced Diploma) – mafunzo ya
miaka 2 jumla yao ni 9. Jumla ya wanafunzi wote hadi May 2011
ni 160 (Wanawake kwa wanaume)
Wanafunzi hawa hufundishwa darasani na kufanya mazoezi katika
Hospitali ya Mirembe, Hospitali Kuu ya Mkoa na Kituo cha Afya
cha Manispaa ya Dodoma. Pia wanafunzi huenda kufanya mazoezi
katika vijiji vya karibu, hutembelea vituo vya watoto wenye
mtindio wa ubongo, makazi ya wazee, na wale wasiojiweza kwa
kujifunza zaidi.
38
7.0. HUDUMA KWA WAGONJWA WOTE:
Takwimu za miaka mitano (5) zinaonyesha kwamba jumla ya wagonjwa 160,509
walihudhuria na kupata huduma mbalimbali za afya kama ifuatavyo:
Jedwali na.9 Huduma za Wagonjwa kwa kipindi cha miaka mitano 2006 - 2010:
S/N AINA YA
WAGONJWA
2006 2007 2008 2009 2010 JUMLA
1 Wagonjwa wa akili raia
(civil psychiatric in
patients)
2,334 2,439 2,447 2,540 2,158 11,698
2 Wagonjwa wa akili
wahalifu (forencic pts.)
331 236 146 163 150 1,101
3 Wagonjwa wa
kawasida (physical
inpatients)
897 893 896 1,334 1,340 6,030
4 Wagonjwa wan je wa
akili (OPD pasych. Pts)
4,861 5,103 8,354 7,640 6,456 35,642
5 Wagonjwa wan je wa
kawaida (OPD physical
patients)
14,070 14,138 18,907 19,843 25,346 104,977
JUMLA 66,249 68,740 30,750 24,578 35,432 160,509
7.2. HUDUMA ZA WAGONJWA WA AKILI:
Mchanganuo wa huduma kwa wagonjwa wa akili kwa kipindi cha miaka mitano (5)
iliyopita yaani (Julai 2006 – Desemba 2010) ni kama ifuatavyo:
Jedwali Na. 10 Huduma kwa Wagonjwa wa Akili kwa kipindi cha miaka mitano
Julai 2006 – Desemba 2010
S/N WAGONJWA 2006 2007 2008 2009 2010 JUMLA
1 Schizophrenia 2,019 886 1,584 1,598 1,288 8,019
2 PSUD 372 154 333 346 336 1,709
3 Epilepsy 302 175 356 362 318 1,672
4 OBS 112 162 89 106 112 637
5 Senile Dem. 25 11 13 21 14 91
6 Mania 3 38 55 60 56 240
7 Depression 5 12 13 32 24 98
8 Mental Ret. 7 5 2 9 6 32
9 Neurois 0 0 1 4 4 11
10 Pers. Disord 0 0 1 2 - 6
JUMLA 2,845 1,443 2,447 2,540 2,158 12,512
39
Changamoto
• Tatizo linaloonekana kuwa kubwa kwa jamii kwa sasa ni utumiaji wa
dawa za kulevya. Kwa kipindi cha miaka mitano jumla ya wagonjwa
1,709 walipokelewa wakiwa waathirika wa dawa za kulevya (drugs
addicts). Wengi wao wakiwa vijana wa kiume (wenye umri kati ya
miaka 15 na 35) ambayo ndiyo nguvu kazi ya Taifa
• Jamii ya Watanzania walio wengi wana ufinyu wa ufahamu wa
magonjwa ya akili. Wagonjwa wengi hucheleweshwa nyumbani
wakipelekwa kwa waganga wa jadi au makanisani na misikitini
kuombewa. Hili linachangia usugu wa ugonjwa.
• Wagonjwa wa akili wanatelekezwa na ndugu/jamaa zao pasipo msaada
wowote.
40
3.2.3. SEKTA YA ELIMU
UTANGULIZI
Historia ya Harakati za maendeleo ya sekta ya elimu Mkoani Dodoma imegawanyika
katika vipindi vitatu (3) kabla ya Uhuru, wakati wa Uhuru na baada ya Uhuru katika
maeneo makuu manne (4) Elimu ya msingi, Elimu ya Sekondari, Elimu ya watu
wazima na Elimu ya vyuo. Elimu iliyokuwa ikitolewa ilitofautiana kuzingatia vipindi
mahitaji na mfumo wa utawala, mahitaji ya kisiasa na kiuchumi katika vipindi husika.
(i) ELIMU YA MSINGI KABLA YA UHURU - MWAKA 1920 - 1960
Shule ya kwanza kubainika kuwepo mkoani Dodoma ni ile iliyoanzishwa na
Mmisionari wa Shirika la CMS Bwana W. Cole. Shule hiyo ilianzishwa huko Handali
mnamo mwaka 1926, ikiwa na walimu 2 ambao ni Bwana W. Cole akishirikiana na
Mkewe.
Mwaka 1927, wazawa wawili waliongezwa ili kusaidia kuwafundisha wanafunzi wa
wakati huo. Walimu hawa walikuwa Petro Lusinde na John Mwakawele ambao
walikuwa au walitumika kama wakalimani wa lugha ya Kienyeji Kigogo, na
Kiingereza, lugha ambayo ilitumika kutolea mafundisho shuleni. Mnamo mwaka
1928, Mmisionari wa shirika la CMS kutoka Ujerumani Bwana Sprelingle (Speranje)
alifanya ziara ya kumtembelea Bwana W. Cole akianzia Dar es Salaam, na kusafiri
kwa gari moshi hadi Kikombo, ambako alishuka hapo na kuanza kumtafuta mwenyeji
wake.
Kutoka Kikombo alitembea kwa miguu hadi Handali (mahali shule ilipo), umbali
ambao aliamini kuwa haitakuwa rahisi kuihudumia shule hiyo. Bwana Speranje
alishauri shule hiyo ihamishwe/ipelekwe mahali ambapo itakuwa ni rahisi kupata
huduma. Mwaka huo 1928, mwishoni yalifanyika maandalizi ya kuihamisha shule
hiyo kutoka Handali na kuileta hapa Dodoma Mjini maeneo ya Kikuyu.
Dhana ya kupata walimu wa dini ya Kikristo na watumishi wa Serikali kwa kada ya
chini, iliwasukuma wamisionari wa dini ya Kikristo kwa madhehebu ya Waanglikana
na Wakatoliki kuanzisha shule za Msingi maeneo mbalimbali katika Mkoa wa
Dodoma.
41
Jedwali Na. 11 idadi ya Shule za Msingi zilizokuwepo kabla ya Uhuru 1920 – 1960
WILAYA
IDADI YA SHULE
SHULE ZA
SERIKALI
SHULE ZISIZO
ZA SERIKALI
MAELEZO
Dodoma (M) - 23 Mmiliki R.C
Kondoa 3 25 Mmiliki R.C.
Mpwapwa 3 17
Dodoma (V) 1 - Wamisionari wa CMS
Jumla 6 66
Chanzo: Na. I: Mahojiano na Mhashamu Askofu Mathias J. Isuja
Mahojiano na Mwl. Ernest Kongola
MAFANIKIO:
1. Shule za msingi zilizoendeshwa na madhehebu ya dini ziliongezeka kwa haraka.
2. Wasomi wa awali kutoka Mkoa wa Dodoma walianza kuonekana katika utumishi
wa Serikali ya Mkoloni, miongoni mwao ni pamoja na Mwl. Ernest Kongola na
John Lusinde.
CHANGAMOTO:
(1) Idadi ya shule ilikuwa ni ndogo mno kulingana na mahitaji na idadi ya watu wa
wakati huo. Elimu ilikuwa ikitolewa katika hali ya ubaguzi wa rangi au
madhehebu ya Dini
(2) Malengo ya elimu iliyotolewa yalikuwa ni kuandaa watumishi wa kada ya chini
na wala si kuwafanya wanafunzi kujitegemea.
(3) Ukosefu wa kumbukumbu bayana wa nyaraka zinazohusu Elimu kabla ya Uhuru.
Shule ya awali kabisa iliyoanzishwa huko Handali mwaka 1926 iwekewe
kumbukumbu ya kihistoria.
42
(ii) ELIMU YA MSINGI WAKATI WA UHURU - MIAKA YA 1961 - 1970
Baada ya kupata Uhuru 1961, Mkoa wa Dodoma uliendeleza kwa kasi ujenzi
wa shule za Msingi ili kukabiliana na mahitaji ya Elimu na pia kubaini kuwa
Elimu ndio ufunguo wa maisha.
Serikali ya Tanganyika/Tanzania katika kipindi hicho haikuwa na uwezo
mkubwa wa ki-uchumi ili kukidhi haja za wananchi wake katika nyanja
mbalimbali. Kupitia Sera ya Ujamaa na Kujitegemea na hasa baada ya Azimio
la Arusha – 1967, shule zote zilizokuwa zinamilikiwa na asasi binafsi
zilitaifishwa na kuwa mali ya Serikali. Jedwali lifuatalo linaonesha idadi ya
shule hizo.
Jedwali Na. 12 idadi ya Shule za Msingi zilizotaifishwa baada ya Uhuru
1961 - 1970
WILAYA
IDADI YA SHULE
SHULE ZILIZOTAIFISHWA
Dodoma 24
Kondoa 28
Mpwapwa 30
Dodoma (V) 33
Jumla 109
Chanzo: Mhashamu Askofu Mathias J. Isuja na Mwl. Ernest Kongola.
MAFANIKIO:
1. Kulikuwa na mafanikio kidogo katika kipindi hiki kwa upande wa shule za
Msingi, kwani shule hizo zinazoonekana kwenye jedwali ni zile zilizokuwa
zinamilikiwa na Asasi binafsi katika kipindi cha miaka ya 1920 – 1960. Hata
hivyo, Serikali ilifanya jitihada kubwa ya kuanzisha vyuo vya Ualimu ili kupeleka
walimu katika shule hizo.
2. Shule ya Msingi ya kwanza kujengwa na Serikali hapa Dodoma ilikuwa ni Uhuru
Shule ya Msingi – 1961.
43
Shule ya Msingi Uhuru
44
Shule ya Msingi ya Uhuru kama inavyoonekana sasa
(iii) ELIMU YA MSINGI WAKATI WA UHURU - MIAKA YA 1971 - 1980:
Kupitia Sera ya Ujamaa na kujitegemea na hasa uanzishaji wa vijiji vya Ujamaa,
Serikali Mkoani Dodoma iliweza kuhamasisha wananchi katika shughuli za
maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule za msingi katika vijiji vyao. Hamasa ya
wananchi kuhamia vijijini, ilikwenda sambamba na ujenzi wa shule za msingi. Shule
nyingi zilizengwa kutekeleza azimio la msemo la Elimu kwa wote (UPE) la mwaka
1974
45
Jedwali Na. 13 idadi ya Shule za Msingi zilizokuwepo Miaka ya 1971 – 1980
WILAYA
IDADI YA SHULE
SHULE ZA
SERIKALI
SHULE ZISIZO ZA SERIKALI
Dodoma 53
Kondoa 70 1
Mpwapwa 48
Dodoma (V) 79
Jumla 150 1
Chanzo: Taarifa kutoka Wilaya husika
ELIMU YA MSINGI WAKATI WA UHURU – MIAKA YA 1981 – 1990
Jitihada za kuongeza shule za msingi ziliendelezwa, kwani Serikali iliweza kujenga
shule sambamba na mashirika ya dini.
Jedwali Na. 14 idadi ya Shule za Msingi zilizokuwepo Miaka ya 1981 – 1990
WILAYA
IDADI YA SHULE
SHULE ZA
SERIKALI
SHULE ZISIZO ZA SERIKALI
Dodoma 66 7
Kondoa 180 -
Mpwapwa 72
Dodoma (V) 83
Jumla 401 1
Chanzo: Taarifa kutoka Wilaya husika
(iv) ELIMU YA MSINGI WAKATI WA UHURU - MIAKA YA 1991 - 2011
Kuanzia mwaka 1991 – 2011, Mkoa wa Dodoma umeweza kuongeza kujenga shule
nyingi za msingi. Uwezo huu unatokana na mpango kamambe ulioanzishwa na
Serikali, Mpango wa MMEM. Kwa usimamizi mzuri wa mpango wa MMEM,
mashirika ya dini na Asasi Binafsi nayo hayakubaki nyuma katika kutoa changamoto
ya kujenga shule Jedwali lifuatalo linaonesha hali halisi ya idadi ya shule zilizopo
hadi sasa.
46
Jedwali Na. 15 idadi ya Shule za Msingi zilizopo Miaka ya 1991 – 2011
WILAYA
IDADI YA SHULE
SHULE ZA
SERIKALI
SHULE ZISIZO ZA SERIKALI
Dodoma 92 14
Kondoa 220 2
Mpwapwa 115 -
Chamwino 110 -
Bahi 70 -
Kongwa 105 -
Jumla 712 16
Chanzo: Taarifa kutoka Wilaya husika
NB: Wilaya ya Mpwapwa iligawanywa mwaka 1995 na kuunda Wilaya mbili za
Mpwapwa na Kongwa. Aidha Wilaya ya Dodoma Vijijini iligawanywa mwaka
2006 na kuunda Wilaya mbili mpya za Bahi na Chamwino
(v) ELIMU YA SHULE ZA SEKONDARI KABLA YA UHURU
Wahitimu waliomaliza Elimu ya Msingi kwa wakati huo zikiitwa Shule za Kati
(Middle schools) na kufaulu mitihani walichaguliwa kujiunga na masomo ya
Sekondari. Shule za Sekondari Mkoani Dodoma kabla ya Uhuru zilikuwa ni saba
(7) tu. Wahitimu waliomaliza Elimu ya msingi kwa wakati huo zikiitwa shule za
kata (Middle Schools) na kufaulu Mitihani walichaguliwa kujiunga na shule hizo
ambazo ni Bihawana, Msalato, Alliance (Mazengo) Mpwapwa Indian (Dodoma
Sekondari), Mvumi na Muslim (Jamhuri Sekondari).
Jedwali Na.16 -idadi ya Shule za Sekondari kabla ya Uhuru
WILAYA SHULE ZA
SERIKALI
SHULE ZISIZO ZA
SERIKALI
MAELEZO
DODOMA -
2
2
1
Mmiliki Kanisa Katoliki
Mmiliki Aglikana
Indian
Mpwapwa 1 - Mmiliki Serikali
Jumla O1 06
47
(vi) SHULE ZA SEKONDARI BAADA YA UHURU - 1961 - 2011
Shule zilizokuwepo kabla ya Uhuru ziliendelezwa katika kipindi hiki na
nyingine mpya kujengwa kufikia Kidato cha Nne na Sita badala ya kuishia
darasa la Kumi. Shule hizo ni: Bihawana, Alliance (Mazengo), Mpwapwa,
Msalato Girls, Kondoa Girls, Dodoma Central, Mvumi Girls, Muslim Schools
na Indian Schools. Zaidi ya hapo shule zilizokuwepo katika Madhehebu ya
Dini zilibadilishwa na kuwa shule za Serikali.
Shule za Sekondari zimeongezeka kutoka shule saba (7) zilizokuwepo kabla
na miaka ya mwanzo ya Uhuru na kufikia shule 204 zilizopo sasa, ambapo
shule za Serikali ni 180 na zisizo za Serikali ni 24 (Ishirini na mbili ) kama
inavyoonesha kwenye jedwali lifuatalo:
Jedwali Na. 17. - Shule za Sekondari baada ya Uhuru - 1961 – 2011
IDADI YA SHULE
WILAYA SHULE ZA
SERIKALI
SHULE ZISIZO ZA
SERIKALI
BAHI 20 -
CHAMWINO 24 2
DODOMA(M) 36 14
KONDOA 52 04
KONGWA 24 03
MPWAPWA 24 01
JUMLA 180 24
(vii) VYUO VYA UALIMU KABLA YA UHURU 1920 - 1960
Katika kipindi hiki (1920 – 1960), Mkoa wa Dodoma haukuwa na Chuo cha
Ualimu kilichotambuliwa rasmi isipokuwa palikuwepo na Chuo
kilichoanzishwa na Wamisionari wa Shirika la CMS huko Kongwa mnamo
mwaka 1930. Chuo hiki kilianzishwa kwa ajili ya kutoa mafunzo ya uchungaji
(pasta) kwa dini ya Ukristo madhehebu ya Anglikana, lakini baadaye wakaona
vema kutoa mafunzo ya Ualimu ikiwa ni kwa ajili ya kupata walimu wa shule
zao ambazo zilikuwa zimeanzishwa katika mwaka 1926. Chuo kiki kwa sasa
bado kipo na kinaendelea kutoa mafunzo ya Uchungaji.
48
(viii) VYUO VYA UALIMU BAADA YA UHURU - MIAKA YA 1961 - 1990:
Kadri ya mahitaji ya ki-elimu yalivyokua kutokana na ongezeko la Shule za
Msingi katika kipindi cha wakati wa Uhuru na miaka kumi baadaye (1961 –
1970), Serikali ilijenga Chuo cha Ualimu huko Mpwapwa na kuanza kutoa
mafunzo ya Cheti cha Ualimu Daraja C na Daraja A mnamo mwaka 1964. Hiki ni
Chuo cha kwanza kujengwa katika Mkoa wa Dodoma, na hadi leo Chuo hiki
kinatoa/kinaendesha mafunzo ya Ualimu kwa ngazi ya Cheti cha Daraja la IIIA na
Stashahada.
Mwaka 1975 kilianzishwa chuo cha Ualimu Bustani. Hapo awali majengo ya
Chuo hicho yalitumika kama shule ya wasichana iliyojulikana kama St. Mary’s
Middle School na ilikuwa ikimilikiwa na Madhehebu ya dini ya Kristo (Roman
Catholic Vyuo vingine ambavyo vimejengwa katika Mkoa wa Dodoma ni vile
ambavyo sio vya Serikali. Vyoo hivi ni kama inavyooneshwa katika Jedwali
lifuatalo:
Jedwali Na.18 - Vyuo vya Ualimu miaka ya 1991 - 2011
WILAYA CHUO
MWAKA WA
KUANZA MMILIKI
Dodoma (M) Salesian Seminari T.T.C. 1991 Kanisa Katoliki
Dar-ul-Muslimeen T.T.C. 1998 Shia Ithnashari
Capital T.T.C. 2007 Binafsi
Mtumba T.T.C. 2009 Anglican
Kondoa Bustani T.T.C. 1975 Serikali
Kongwa Nkurumah T.T.C. -
Mkoka
2007 Binafsi
(x) SHULE/VITUO VYA WALEMAVU KABLA YA UHURU:
Kulikuwepo na shule 1 tu ya watoto (walemavu) wasioona katika Mkoa huu wa
Dodoma ambayo ni Shule ya Watoto Wasioona katika Kituo cha Buigiri
kilichomilikiwa na Anglican. Kituo kingine kimoja katika Wilaya ya Kondoa cha
kutunza watoto yatima. Kituo hiki kinamilikiwa na Dhehebu la Kikatoliki.
49
(xi) SHULE/VITUO VYA WALEMAVU BAADA YA UHURU:
Pamoja na vituo viwili vilivyokuwepo wakati wa Uhuru, baada ya Uhuru vituo
vimeongezeka kufikia vituo vitano kama jedwali linavyoonesha hapa chini:
Jedwali Na. 19 - Shule/Vituo vya Walemavu baada ya Uhuru:
WILAYA KITUO
MWAKA WA
KUANZA MMILIKI MAELEZO
Dodoma (M) Kijiji cha Matumaini Kisasa 1995
Kanisa Katoliki
Watoto
waathirika
Kituo cha Cheshire Home
Miyuji
1987 Kanisa Katoliki Watoto
walemavu
Kongwa Watoto walemavu wa viungo
Mlali
1985 Kanisa Katoliki
Chamwino Buigiri wasioona 1954 Anglican Msingi
Kondoa Kituo cha watoto yatima 1937 Kanisa Katoliki
Bahi Kigwe Viziwi 1991 H/Wilaya Msingi
(xii) ELIMU YA WATU WAZIMA KABLA YA UHURU:
Elimu ya Watu Wazima katika kipindi cha kabla ya kupata Uhuru, ilifanywa kuwa ni
sehemu ya maisha ya kila siku ya mwanadamu. Aidha, Elimu ya Watu Wazima
iliwawezesha wazee wetu kupambana na mazingira na hivyo iliwalazimu kujifunza
kila mara mbinu bora zaidi katika nyanja za kilimo, utunzaji wa familia na ufundi
mbalimbali ili kuendeleza na kukuza uchumi. Pamoja na kuanzisha mfumo wa Elimu
ya Msingi kwa kuanzisha shule za vijijini (Bush Schools) ambazo zilijengwa vijijini,
Wajerumani waliweza kutoa elimu kwa watu wazima (chini ya miti) ili waweze kuwa
Makatekista na Wainjilisti (walimu wa dini).
Waziri wa Makoloni ya Uingereza alianzisha mpango wa uchumi na maendeleo wa
miaka 10 (1946 - 1956) ambao moja ya utekelezaji wake ni kuanzisha kisomo na
Elimu ya Watu Wazima, Elimu ya Ufundi, Afya, Kilimo na mafunzo kazini.
Utekelezaji huo ulifanywa katika Wilaya/maeneo kadhaa nchini. Katika Mkoa wa
Dodoma, Wilaya ya Mpwapwa na Kondoa zilihusishwa. Mambo yafuatayo
yaliainishwa katika utekelezaji wa mpango huo.
(a) Kutoa Elimu kwa watu wazima kwa ajili ya askari 68,000 wa Kiafrika waliokuwa
wanarudi nchini baada ya vita ya pili ya Dunia.
50
(b) Kuongeza mbinu ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.
(c) Kufanya majaribio ya kisomo ili kutekeleza maagizo mbalimbali yatolewayo na
Serikali.
Chama cha TANU kilipoundwa Julai 7, 1954 kilitamka umuhimu wa Elimu ya
Watu Wazima katika Katiba yake sehemu ya 6 ya ahadi za mwana TANU
“Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia Elimu yangu kwa faida ya
wote” Ahadi hiyo iliweza kuwahamasisha watu wazima katika kampeni za kudai
Uhuru. Wakoloni wa Kiingereza waliweza kufanikiwa kuendeleza kisomo kwa
mbinu zao ambazo zilikuwa ni:-
♦ Kutumia gari la Sinema
♦ Kutumia mabango
♦ Kutoa/kugawa vifaa vya kujifunzia kama vile madaftari na kalamu
♦ Walimu waliokuwa wanafundisha watu wazima walilipwa posho.
(xiii) ELIMU YA WATU WAZIMA BAADA YA UHURU 1961 - 1970
Ni dhahiri na muhimu kutambua kuwa Elimu ya Watu Wazima kupitia Siasa
iliyoendeshwa na TANU chini ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere ilichangia kwa kiasi kikubwa juhudi za kufanikisha kuleta
Uhuru wa Tanganyuika. Dhana hiyo yatokana na ukweli kwamba, Baba wa Taifa
hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitambua kuwa, bila kuwaelimisha
watu wazima, huenda Uhuru usingepatikana katika njia hiyo, vinginevyo
wananchi wangelazimika kumwaga damu ili kujikomboa.
Katika kipindi cha 1961 - 1966, Elimu ya Watu Wazima ilikuwa inatekelezwa bila
sera au mwongozo maalumu, na ndiyo maana baadhi ya Mikoa ukiwemo Mkoa wa
Dodoma, mpango haukutekelezwa sana. Kadhalika, kipindi cha 1967 – 1969,
kinakumbukwa sana katika historia ya nchi yetu ikiwa ni pamoja na kuanzishwa
kwa Azimio la Arusha (5 Feb. 1967), kuanzishwa kwa Mpango wa Pili wa
Maendeleo wa miaka mitano na kufanyika kwa sensa ya watu wote nchini Oktoba,
1967. Ni katika kipindi hiki (1967) cha sensa ya watu wote, Takwimu za kubaini
idadi ya watu wanaojua na wasiojua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu katika Mkoa
wa Dodoma zilianza kuonekana/kujulikana. Mwaka 1969 Oktoba, Serikali
ilipitisha uamuzi wa kuanzishwa kisomo cha Watu Wazima, uamuzi uliotangazwa
51
na Mwalimu J. K. Nyerere katika mkesha wa mwaka mpya na kuufanya mwaka
1970 kuwa ni mwaka wa Kisomo cha Watu Wazima.
Lengo la mwaka wa kisomo cha Watu Wazima lilikuwa ni:-
(i) Kubadilisha maisha ya watu ili waweze kuishi maisha ya kisasa.
(ii) Kuwafanya watu wajifunze namna nzuri ya kuendesha maisha yao.
(iii) Kumfanya kila mmoja kuielewa Sera ya Taifa ya Ujamaa na Kujitegemea.
(xiv) ELIMU YA WATU WAZIMA MIAKA YA 1971 - 1990
Katika kipindi cha kuanzia mwaka 1971 - 1980, Elimu ya Watu Wazima iliweza
kudhihiri pande mbalimbali za nchi ukiwemo Mkoa wetu wa Dodoma. Ni katika
kipindi hiki, upimaji wa wanakisomo ulifanyika mara tatu ukiwa ni mwaka 1975
na 1977. Aidha, mwaka 1978 kulifanyika Sensa nchini, sensa iliyoonesha idadi ya
watu wazima wanaojua na wasiojua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu.
Ukilinganisha takwimu za mwaka 1967 (wakati wa sensa ya kwanza baada ya
Uhuru) na takwimu za sensa ya mwaka 1978 utabaini mambo mawili, mosi, ni
ongezeko la watu kutoka 709,380 hadi 971,921 na kuongezeka kwa idadi ya Watu
Wazima wanaojua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kutoka 307,228 hadi 339,582.
Idadi ya watu wanaojua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu ilikuwa ikiongezeka
mwaka hadi mwaka.
Program za KKK zilianzishwa ili kuhakikisha wanakisomo waliofuta ujinga
hawaludi ujinga. Vile vile mwaka 1980 lilianzishwa gazeti la Elimu ya Watu
Wazima lililojulikana kama Elimu Yetu kwa ajili ya Kanda ya Kati. Gazeti hili
lilisaidia sana kuwaelimisha wananchi wa Mkoa wa Dodoma.
Uteuzi wa Waratibu wa Elimu ngazi ya Tarafa mwaka 1973 (isipokuwa ngazi hii
ya uongozi ilidumu hadi Juni, 1984). Aidha, uteuzi wa waratibu wa Elimu wa
Kata ulifanyika mwaka 1975. Kutamuliwakwa viongozi hawa kulirahisisha
ufuatiliaji wa EWW kuanzishwa kwa program ya mtaala mpya ambao ulilenga
kuwapatia wanakisomo maarifaa katika fani ya kilimo na ufugaji, Sayasikimu na
Afya na masono ya ufundi.
52
(xv) ELIMU YA WATU WAZIMA MIAKA YA 1991 - 2011:
Kutokana na mabadiliko ya nyakati, Sayansi na Teknolojia Serikali imekuwa
ikibuni mipango mbalimbali kwaajili ya kuimarisha EWW. Serikali imeweza pia
kuzishirikisha asasi zisizo za Serikali katika uendeshaji wa Elimu ya Watu
Wazima.
Kwa kipindi hiki Serikali imeanzisha program za MUKEJA na MEMKWA.
Program hizi zimesaidia sana kuimarisha Eili ya Watu Wazima katika Mkoa wa
Dodoma. Programu ya MUKEJA imewasaidia wananchi kuapta elimu wakati huo
huo wakiendelea na shughuli zao za uzalishaji mali.
Program ya MEMKWA ambayo ilianzishwa mwaka 2002 imesaidia sana
kuwapatia watoto wenye umri wa miaka kati ya 11 – 18 ambao walikuwa
wamekosa elimu ya msingi. Wengi wao wameweza pia kuendelea na elimu ya
Sekondari.
CHANGAMOTO:
(i) Mwezi Julai, 1993, Gazeti la Kanda ya Kati Dodoma - Elimu Yetu” lilitoa
nakala ya mwisho kwani kuanzia hapo, Gazeti hilo halijachapishwa tena.
(ii) Kukosekana kwa takwimu sahihi zihusuzo Elimu ya Watu Wazima kwa
sababu ya kutokufanyika kwa sensa ya watu wote nchini kwa wakati
unaotakiwa.
(iii) Mahudhurio hafifu ya wanakisomo darasani na Kuongezeka kwa idadi ya
watu (uhamiaji) kunasababisha ongezeko la watu wasiojua kusoma, kuandika
na kuhesabu.
(iv) Mdondoko wa wanafunzi (Drop Out) katika madarasa ya shule za Msingi
kunakosababishwa na sababu mbalimbali kwa mfano kukabiliwa na
majukumu ya kulea familia na Utoro wa rejareja na wa kudumu.
(v) Ukosefu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia na Ukosefu wa fedha za
kuendeshea shughuli za Elimu ya Watu Wazima.
53
HITIMISHO
Katika vipindi vitatu vilivyoanishwa katika taarifa hii ni bayana kuwa kulikuwa na
maendeleo katika sekta ya Elimu kabla, wakati na baada ya Uhuru. Hata hivyo
Serikali kuu na ile ya Mkoa wa Dodoma imejitahidi katika kuzipatia ufumbuzi
changamoto zilizo bainishwa katika taarifa hii,ikiwa ni sambamba na upanuzi wa
vyuo vya Elimu ya juu ili kupata wataalamu wa fani mbalimbali wengi zaidi.
3.2.4. SEKTA YA MAJI
1.0. HALI YA HUDUMA ZA MAJI KABLA YA UHURU MWAKA 1961
Kabla ya kupata uhuru, mwaka 1961, Mkoa wa Dodoma ulikuwa na Wilaya
tatu (3) ambazo ni Mpwapwa, Kondoa na Dodoma. Wakati ule hali ya hewa
katika Mkoa huu ilikuwa tofauti na ilivyo sasa. Mvua zilikuwa zikinyesha za
kutosha na ziliruhusu watu kupata huduma ya maji kutoka katika vyanzo vya
asili kama visima vya kienyeji ambavyo vilikuwa vifupi na havikuhitaji kazi
kubwa ya kuchimbwa, visima vifupi ambavyo vilichimbwa kwa kutumia zana
duni zilizokuwepo kwa wakati ule hadi kufikia urefu wa mita 6 au 7 (futi 20),
malambo yaliyotumika kwa ajili ya mifugo na wanadamu pia, Chemchem
pamoja na visima virefu vichache vilivyotoa maji katika maeneo kama ya
Mpwapwa na Kondoa walipokuwa wafugaji wengi na hapa Dodoma Mjini.
Kisima kirefu cha kwanza katika Mkoa wa Dodoma kilichimbwa Mjini
Dodoma mwaka 1910.
Baadhi ya vyanzo vichache vya maji vilivyokuwepo wakati ule ni kama
ifutavyo:
Jedwali Na. 20 Hali ya Huduma za Maji kabla ya Uhuru mwaka 1961
Na Wilaya VYANZO MBALIMBALI
Visima
virefu
Mabwawa/
Malambo
Chemchem Visima
vifupi
1 Dodoma 19 5 11 -
2 Mpwapwa 6 - 41 2
3 Kondoa 13 - 21 -
JUMLA 38 5 73 2
54
1.0. HALI YA HUDUMA YA MAJI ILIVYOKUWA MIAKA KUMI (10)
BAADA YA UHURU
Miaka kumi iliyofuata baada ya Uhuru Mkoa wa Dodoma Kiutawala bado
ulikuwa unaundwa na Wilaya tatu kama zilivyotajwa hapo juu. Huduma ya
Maji katika kila Wilaya iliendelea kuboreka zaidi. Takwimu za visima virefu
zilizopo zinaonesha kuwa kati ya miaka ya 1961 na 1971 idadi ya visima
vilivyokuwa vimejengwa ilikuwa ni 59 kwa mchanganuo ufuatao:
Jedwali Na. 21 Idadi ya Visima Vilivyojenga baada ya Uhuru mwaka 1961 - 1971
Na Wilaya Idadi ya Visima
1 Dodoma 30
2 Kondoa 22
3 Mpwapwa 7
JUMLA 59
Bahati mbaya sababu ya kuchimbwa visima vichache katika Wilaya ya
Mpwapwa ikilinganishwa na Wilaya zingine, haikuelezwa.
2.0. HUDUMA YA MAJI KATI YA MIAKA YA 1972 HADI 1991
Miaka ishirini iliyofuata kulitokea mabadiliko katika mfumo wa Kiutawala wa
Mkoa wa Dodoma ambapo Wilaya ya Dodoma iligawanywa na kuwa Wilaya
mbili za Dodoma Mjini na Dodoma Vijijini. Pamoja na mgawanyiko huo wa
Wilaya baadhi ya Vijiji vilivyokuwa katika Wilaya ya Dodoma viliingizwa
katika Wilaya Dodoma Mjini. Hii ilileta changamoto katika utoaji wa huduma
za maji kwa kuwa eneo moja la Wilaya lilikuwa likihudumiwa kama Mji halisi
(yaani idara ya Maji Mjini) wakati eneo lingine huduma zake ziliendeshwa
chini ya mfumo wa Maji Vijijini.
Katika kipindi hicho ndipo ilipotungwa Sera ya Maji ya mwaka 1971 ambayo
ililenga kuwapatia wananchi wote maji bila malipo katika umbali usiozidi mita
400 kutoka kwenye makazi yao.
Inakadiriwa kuwa takribani visima virefu 100 vilichimbwa katika Mkoa wa
Dodoma kwa mchanganuo ufuatao Kiwilaya.
55
Jedwali Na. 22 Idadi ya Visima Vilivyojenga Miaka ya 1972 - 1991
Na Wilaya Idadi ya Visima
1 Dodoma Vijijini 40
2 Kondoa 32
3 Mpwapwa 9
4 Dodoma Mjini 21
JUMLA 102
Shughuli za usimamizi wa kazi zote za maendeleo katika Mkoa zilikuwa
zikifanyika kupitia Ofisi ya Mhandisi wa Maji wa Mkoa. Kazi za Ofisi hii
zilijumuisha kubuni miradi ya maji, kuisanifu, kuijenga, kuiendesha pamoja na
kuifanyia matengenezo.
3.0. HUDUMA YA MAJI KATI YA MWAKA 1991 NA 2008
Mabadiliko ya Kiutawala yaliendelea kutokea ambapo mwaka 1995 Wilaya ya
Mpwapwa iligawanywa na kupatikana Wilaya mbili za Kongwa na Mpwapwa
na mwaka 2005 Wilaya ya Dodoma Vijijini nayo iligawanywa nakupatikana
Wilaya mbili za Bahi na Chamwino. Kugawanyika kwa Wilaya hizi
kuliongeza majukumu na kuboresha utekelezaji katika Sekta ya Maji kwa vile
kila Wilaya ilikuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa inasogeza huduma ya
maji kwa wananchi wake kwa ubora zaidi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Hii ilitokana na ile dhana kwamba usimamizi wakati huo ulikuwa karibu na
wananchi
Kipindi hiki kiliambatana na kutungwa kwa Sera mpya ya Maji ya mwaka
2002 ambayo ndani yake hata majukumu ya Serikali nayo yalibadilika.
Serikali iliamua kuacha utaratibu wake wa kutoa maji bure kwa wananchi na
hivyo kuwataka wawe wanachangia kiasi fulani cha fedha katika miradi yote
itakayotekelezwa katika Vijiji. Utaratibu huu ulianzishwa baada ya kuona
kwamba uwezo wa Serikali kugharamia shughuli zote za kijamii peke yake
ulikuwa unapungua lakini pia ilionekana kwamba kwa kuchangia katika ujenzi
wa miradi ya maji wananchi walikuwa wanaithamini na kuiona ni mali yao
kuliko wakati ule ilipokuwa inagharamiwa kwa asilimia 100 na Serikali.
56
Hata vile vile wananchi walitakiwa kuanza utaratibu wakulipia maji kote
Mijini na Vijiji. Pia katika kipindi hiki tulishuhudia uanzishwaji wa
utekelezaji wa Programu mbili kubwa za maji zilizokuwa zikifadhiliwa na
Benki ya Dunia. Kwanza kabisa kulianzishwa utekelezaji wa program ya Maji
Vijijini na Usafi wa Mazingira (RWSSP). Chini ya Program hii Wilaya 32
nchini zilichaguliwa na kutakiwa kuteua Vijiji kumi kila Wilaya ambavyo
vingelihusika katika mradi huu. Bahati nzuri Wilaya za Kondoa, Mpwapwa na
Kongwa za Mkoa wa Dodoma zilichaguliwa. Baadaye kila Wilaya, nchini
iliingizwa katika utekelezaji wa Programu kwa utaratibu ule ule wa kuteua
Vijiji kumi katika kila awamu ya utekelezaji.
Mwaka 2008/2009 ilianzishwa Program ya Maendeleo ya Sekta ya Maji.
Program hii iliongeza maeneo ya utekelezaji kwa kuwa sasa siyo tu Vijiji
vilipewa fedha za utekelezaji wa miradi bali hata Ofisi za Mabonde ya Maji
pamoja Mamlaka za Majisafi na Majitaka za Miji nazo zilipata.
Jedwali Na. 23 Mchanganuo wa visima virefu vilivyochimbwa kati ya miaka ya
1991 na 2008 Kiwilaya.
Na Wilaya Idadi ya Visima
1 Bahi 19
2 Chamwino 21
3 Kondoa 19
4 Mpwapwa 4
5 Dodoma Mjini 3
6 Kongwa -
JUMLA 66
4.0. HALI YA HUDUMA YA MAJI ILIVYO SASA HIVI
Usambaji wa huduma ya maji katika Mkoa wa Dodoma unaathiriwa na uhaba
wa mvua zinazonyesha mwaka hadi mwaka. Kutokana na hali hii ya ukame
visima vifupi vingi vinazidi kukauka na visima vya asili huko Vijijini
ambavyo vimekuwa tegemeo la wananchi wengi wa huko tokea zamani navyo
vimekauka. Mbaya zaidi hata visima virefu ambavyo vilichimbwa kwa
gharama kubwa navyo vimeathiriwa na uhaba wa mvua na hivyo
kupungukiwa na uwezo wake wa kutoa maji kwa kiasi kikubwa mpaka
vingine navyo kukauka kabisa.
57
Kiwango cha usambazaji wa huduma ya maji kwa sasa ni asilimia 50.9 wakati
kiwango cha huduma hiyo mijini ni asilimia 79.8 na Vijijini ni asilimia 44.1.
Jedwali lifuatalo hapa chini linaonesha idadi ya vyanzo mbalimbali vya maji
tulivyonavyo hapa Mkoani, na idadi ya watu wanaopatahudumayamajisafi na
salama katika kila Wilaya.
58
5.0. CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SEKTA YA MAJI MKOANI
• Bado tunayo idadi kubwa ya wananchi ambao hawajafikiwa na huduma hii
ya maji safi na salama (Asilimia 49.9)
• Uhaba wa mvua zinazoonyesha mwaka hadi mwaka unasababisha hata
vyanzo kidogo vilivyopo kupungukiwa na uwezo wa kutoa maji ya
kukidhi mahitaji
• Gharama za uendeshaji wa miradi ya maji zinaendelea kuwa kubwa
kutokana na gharama za umeme, mafuta ya diesel pamoja na vipuri
kupanda kila mara.
• Hali ya ukame katika Mkoa inatusababishia kutokuwa na njia nyingine
mbadala ya kuwapatia wananchi wetu maji isipokuwa visima virefu pekee
ambavyo ni aghali kuchimba
• Baadhi ya visima virefu vinavyochimbw,a tena kwa gharama kubwa,
vinakuwa na maji ya chumvi yasiyofaa kwa matumizi ya binadamu.
6.0. MATARAJIO YA BAABAYE
Ukame wa muda mrefu pamoja na uhaba wa vyanzo vya maji ni mambo
ambayo kama binadamu hatuna uwezo nayo.
Hata hivyo teknolojia ya uvunaji wa maji ya mvua inaweza kuleta nafuu hasa
vijijini endapo wananchi watahamasishwa na kuikubali. Hii ni teknolojia
ambayo ni rahisi kwa gharama na kwa utekelezaji wake lakini tatizo kubwa
lililopo hasa katika Mkoa huu ni wananchi wengi huko Vijijini kutokuwa na
nyumba za bati ambazo ndizo zinazotumika kuvuna maji yenye kiwango cha
usafi na kilicho bora katika ngazi ya kaya.
Uvunaji wa maji ya mvua unaweza kufanyika kwa kujenga mabwawa na
malambo kwenye ngazi za Vijiji lakini tatizo kubwa hapa ni kwamba maji
kutoka katika vyanzo vya aina hii yanahitaji kuchemshwa au kutumia dawa za
kutibia maji, mambo ambayo wananchi wengi huko Vijijini hawapendi
kufanya na vhivyo maji hayo yanaweza kuwaletea athari za kiafya.
59
3.2.5. MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAJITAKA MJINI DODOMA
Kabla ya miaka ya 1950 huduma za majisafi katika Mji wa Dodoma zilikuwa
zikitolewa na kutegemea chanzo cha Maji cha bwawa la Mkalama ambapo idadi ya
watu ilikuwa ndogo. Baada ya idadi ya watu kuanza kuongezeka, chanzo kingine cha
Maji katika bonde la Makutupora kilianzishwa na ndicho chanzo ambacho kinatumika
hadi hivi sasa kikiwa kina uwezo wa kuzalisha maji kiasi cha meta za ujazo 70,000
kwa siku (SEURACE/NETWAS, 2003).
Kabla ya mawaka 2002, hali ya maji Mjini Dodoma ilikuwa siyo ya kuridhisha
kutokana na kuwepo kwa migao mikali ya huduma ya maji. Migao hiyo ilisababisha
baadhi ya maeneo kupata maji mara moja kila baada ya wiki mbili tena kwa muda
mfupi sana na mengine kutopata kabisa hali iliyotishia ustawi wa maji kutokana na
wawekezaji wengi kutotaka kuwekeza Dodoma.
Hali hii ilichangiwa kwa kiasi kikubwa na kuwepo kwa eneo la kilimo cha
Umwagiliaji maji kati ya Mzakwe na Msalato lililojulikana kama ukanda wa kijani
(Green Belt). Katika eneo hili, asilimia 80 ya maji yaliyokuwa yakizalishwa yakiishia
katika matumizi ya kilimo cha Zabibu, bustani za mbogamboga na migomba.
Kutokana na mfumo wa kulipia kiwango sawa (Flat rate) uliokuwepo hapo zamani,
matumizi ya maji kwa umwagiliaji katika eneo hili yalikuwa mabaya na yasiyolipika.
Aidha kabla ya mwaka 1998, huduma ya Majisafi ilikuwa ikitolewa na Idara ya Maji
iliyokuwa chini ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Maendeleo wa Mkoa (RDD) ambapo
gharama zote za uendeshaji, matengenezo na uwekezaji ziligharamikiwa na Serikali
Kuu na huduma ya maji ilikuwa ikitolewa bila kuwa na msisitizo wa kuliipia kutoka
kwa wanufaikaji.
60
KUANZISHWA KWA MAMLAKA YA MAJISAFI NA MAJITAKA MJINI
DODOMA - DUWASA:
Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka Mjini Dodoma (DUWASA) ilianzishwa Julai
1998 kwa mujibu wa kifungu 3(i) cha sheria Na. 8 ya mwaka 1997 kama
ilivyofanyiwa marekebisho na sheria Na. 12 ya mwaka 2009 ya usambazaji majisafi
na uondoshaji majitaka kwa wakazi wa Mji wa Dodoma.
Mara baada ya DUWASA kuanzishwa, na kwa msaada wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
naz Makuu wa wilaya, ilianza mkakati wa kuzuia matumizi ya majisafi kwa kilimo.
Aidha ilianza mpango wa kufunga mita za maji kwa watumiaji wote wa maji ili mteja
alipie kulingana nas matumizi yake badala ya mfumo wa “flat rate”.
Ufungaji mita kwa wateja wote ulikamilika mwaka 2003. Kwa hatua hizo kulisaidia
kuboresha huduma ya maji kwa wakazi wa Mjini Dodoma ambapo migao ya maji
ilikoma na maeneo yote yaliyokuwa hayapati maji yalianza kupata maji ya uhakika
mda wote.
Hali halisi ya Huduma ya Maji Mjini Dodoma:
Kwa mujibu wa utafiti na stadi za karibuni juu ya mahitaji ya maji kwa wakazi wa
Mji wa Dodoma uliofanywa na Mhandisi Mshauri SEURECA/NETWAS mwaka
2002/2003 na kufanyiwa mapitio na Mhandisi Mshauri COWI CONSULT mwaka
2009, mahitaji ya Maji Mjini Dodoma kwa sasa ni wastani wa meta za ujazo 54,000
kwa siku. Kiasi hiki kinajumuisha mahitaji ya chuo Kikuu cha Dodoma mahitaji ya
Chuo Kikuu cha Dodoma ambapo kitakapo kamilika kitakuwa na Jumla ya watu
wapatao 100,000 ambao watahitaji maji kiasi cha meta za ujazo zisizopungua 10,000
kwa siku.
Chanzo pekee cha uzalishaji maji kwa matumizi ya wakazi wa Mji wa Dodoma ni
visima virefu vilivyochimbwa katika bonde la Makutupora. Kuna jumla ya visima vya
uzalishaji maji 22 na vitano (5) vya kuchunguza mwenendo wa maji ardhini
(Observation Boreholes). Uwezo wa visima vilivyopo kwa sasa ni kuzalisha meta za
ujazo zipatazo 45,000 M3 kwa siku. Hata hivyo kutokana na kuchakaa kwa pampu
kumi na moja (11) za baadhi ya visima na uwezo mdogo wa bomba kubwa la
kusafirishia maji, kiasi cha maji kinachozalishwa kwa sasa ni wastani wa meta za
ujazo zipatazo 30,000 tu kwa siku.
61
3.2.6 SEKTA YA KILIMO
Idara ya Kilimo kuanzia miaka ya 1961 imekuwa ikijihusisha katika kutoa elimu kwa
wakulima kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa mazao mashambani yakiwemo ya
chakula na biashara pamoja na mazao ya mifugo.
Kumekuwa na sera mbalimbali zinazosimamia Idara hii zikiwemo Sera ya Kilimo,
Sera ya Mifugo, Sera ya Umwagiliaji na Sera ya Ushirika pamoja na, Sheria ya
Ushirika ya 2002 na Kanuni zake za 2003.
Kati ya miaka ya 1961-1972 shughuli za Kilimo zilikuwa chini ya Serikali kuu, na
watumishi wake waliwajibika kwa Katibu Mkuu wa Wizara.Mwaka 1972 (Madaraka
Mikoani). Idara ya Kilimo iliongezewa utendaji, ambako idara ya Mifugo na idara ya
Ushirika zilijitegemea.
Majukumu na Malengo ya Idara ya Kilimo
• Kusogeza huduma za ughani karibu na wakulima ili kuharakisha
maendeleo ya uchumi hasa katika sekta ya kilimo.
• Kuwafikishia wakulima vijijini maarifa na kanuni za Kilimo Bora cha
mazao wayalimayo na elimu juu ya hifadhi ya udongo
• Kubuni mpango kabambe wa kueneza matumizi ya plau za kuvutwa na
maksai katika Wilaya
SERA NA SHERIA ZILIZOKUWEPO TANGU 1961 HADI SASA
Sera ya Taifa ya Kilimo ya mwaka 1983 ambayo madhumuni yake yalikuwa ni
Kuendeleza jamii ya wakulima wenye usawa kwa misingi ya siasa ya Ujamaa na
Kujitegema, kuweza kujitosheleza kwa chakula Kitaifa na kuongeza kiwango cha
chakula bora kwa watu wote, kuzalisha zaidi ili kusaidia kuinua hali ya maisha ya
watanzania wote, kulipatia taifa fedha za kigeni na kukidhi mahitaji ya Kilimo,na
kukuza sekta ya Kilimo yenye uwiano kwa kutumia mbinu za kisayansi za Kilimo na
teknologia inayofaa kwa mazao mbalimbali.
62
SHERIA
• Sheria ya kuhifadhi ardhi na mazingira za mwaka 1999
• Sheria kudhibiti visumbufu vya mimea
MISUKUMO YA KILIMO ILIYOTOKEA KITAIFA
Serikali iliunda azma ya Kufa na Kupona mwaka 1972 ambayo iliwataka wananchi/
wakulima wafanye kazi kwa bidii ili kuongeza uzalishaji katika Kilimo na Mifugo.
Mwaka 1972 Serikali ilitangaza mwongozo wa kuhimiza Kilimo ulioitwa Siasa ni
Kilimo huko Iringa ambao madhumuni yake yalikuwa ni kuongeza uzalishaji wa
mazao kwa eneo kwa kutumia mbinu za Kilimo za kisasa. Mwaka 2009 azma ya
Kilimo kwanza ilitangazwa na Serikali. Madhumuni ni kukifanya Kilimo na Mifugo
kuwa cha biashara zaidi. Pia uzalishaji wa mazao ya Kilimo na Mifugo uwe na tija.
Nguzo 10 za Kilimo kwanza ni kama ifuatavyo:
Utashi wa kisiasa kutoa msukumo wa mapinduzi ya Kilimo Kugharamia mapinduzi
ya Kilimo na Uboreshaji wa mfumo wa utawala wa Kilimo
• Mabadiliko ya mfumo mkakati katika Kilimo
• Upatikanaji wa Ardhi kwa ajili ya Kilimo
• Vivutio vya kuchochea uwekezaji katika Kilimo
• Uendelezaji wa viwanda katika kuleta mapinduzi ya Kilimo
• Sayansi, Technolojia na raslimali watu katika kuwezesha mapinduzi
ya Kilimo
• Uendelezaji wa miundo mbinu ili kuwezesha mapinduzi ya Kilimo
Uhamasishaji na ushirikishwaji wa Tanzania kuunga mkono na kutekeleza KILIMO
KWANZA.
MALENGO
Malengo ya Kilimo yameendelea kubadilika kwa kadri sera zilivyobadlika. Hata
hivyo lengo kuu bado ni kuongeza uzalishaji wa mazao ya Kilimo na kuongeza kipato
cha mkulima ili hatimaye kupunguza umaskini
63
UZALISHAJI WA MAZAO YA CHAKULA NA BIASHARA
Mara baada ya Uhuru, uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara ulikuwa duni
kutokana na msukumo mdogo katika Kilimo pamoja na matumizi ya zana duni
(Jembe la mkono) Mkoa wa Dodoma una eneo la ardhi lenye ukubwa wa hekta
12,262,789 linalofaa kwa Kilimo, hekta 25,683 zinafaa kwa Kilimo cha umwagiliaji.
Eneo hili ni moja ya fursa za uwekezaji katika uzalishaji wa mazo ya chakula na
biashara. Uzalishaji wa mazao ya chakula katika maeneo mbalimbali ya Wilaya
ulikuwa ukibadilika badilika kufuatana na misimu. Msimu wa mwaka 2002/03
uzalishaji wa mazao ya chakula ulikuwa tani 216,705 ,msimu wa 2003/04 tani
245,714 ya mazao ya chakula zilivunwa na upungufu wa chakula ulionekana
kutokana na ukame uliojitokeza msimu huo.
Msimu wa 2006/07 mavuno yalikuwa tani 352,366 hivyo ilionekana kuna chakula cha
kutosha japo kulikuwa na uvamizi wadudu waitwao makombelele (green stink burg).
Msimu 2007/08 mvua zilinyesha vizuri baadhi ya maeneo kama vile ukanda wa kati
na nyanda za juu, pia maeneo ya ukanda wa Bonde la Ufa kulikuwa na ukame.
Mabadiliko ya mavuno ya mazao ya chakula na biashara yaliendelea kubadilika
kulingana na mabdiliko ya hali ya hewa. Msimu 2008/09 tani 233,107 za mazao ya
chakula zilivunwa za chakula. Msimu 2010/11 tani 434,481 za chakula zilivunwa.
Hata hivyo uhamasishaji wa matumizi ya zana za kisasa na matumizi ya mbegu bora
na mazao yanayostahili kutokana na hali ya hewa ya Mkoa wa Dodoma ndiyo
kichocheo kikubwa katika ongezeko la uzalishaji kwa heka. Usimamizi imara katika
kanda za kilimo katika ngazi zote.
ZABIBU KUWA ZAO KUU LA UCHUMI DODOMA
Mnamo mwaka 1965 Mwalimu J.K.Nyerere alipotembelea Kijiji cha Nkulabi
alisimama na kutangaza kuwa zabibu zitakuwa ndio zao kuu la biashara na uchumi
kwa Dododma. Hili ni tukio kubwa lililoendeleza Kilimo cha zabibu na kiwanda
kikajengwa na Wamisionari kikaendeshwa na Waingereza kabla ya kukabidhiwa kwa
National Milling Cooperation ambako kilikufa kutokana na uongozi mbovu.
Uzalishaji wa zao la Zabibu kwa sasa umeendelea na kuwa wa kisasa zaidi katika
baadhi ya wilaya (Wilaya ya Chamwino).Shamba kubwa lenye zaidi ya ekari 1000
64
limeanzishwa eneo la Chinangali na kufikia Julai 2010 ekari 300 zilisha pandwa
nakutarajia mavuno ya kwanza mwezi wa nane 2011. Pia kumekua na mwamko
mkubwa wa wakazi wa Dodoma katika uendelezaji wa zao hili hivyo baadhi ya
maeneo ya Wilaya za Chamwino, Bahi na Dodoma mjini zinaendelezwa kwa
kutengenezwa skimu za umwagiliaji kwa ajili ya zao hilo.
Jedwali Na.25 -Ongezeko la uzalishaji (tija) wa Mazao ya Kilimo kwa Hekta 1970 - 2011
MWAKA MAZAO/TANI
MTAMA UWELE MUHOGO MAHINDI KARANGA ALIZETI UFUTA ZABIBU
1970-1995 1.0/ha 0.1/ha 0.4/ha 0.4/ha 0.4/ha 0.2/ha 0.2/ha 1.0/ha
1996-2005 1.0/ha 1.0/ha 4.0/ha 1.5/ha 0.5/ha 0.5/ha 0.7/ha 3.6/ha
2006-2011 1.5/ha 1.2/ha 5.0/ha 2.0/ha 1.5/ha 1.2/ha 0.9/ha 7.5/ha
MAFANIKIO YALIYOPATIKANA MPAKA MWAKA 2011
(i) UMWAGILIAJI
Kilimo cha umwagiliaji kilianzishwa na Wakoloni kati ya miaka ya 1930 na 1940.
Skimu za umwagiliaji kabla ya uhuru zilikuwepo 21. Skimu hizo zilikuwa ni za
kienyeji kwani ujenzi wake ulitumia vifaa rahisi na vilivyopatikana katika maeneo
yao kama vile magogo, nyasi na udongo kwa ajili ya kutengeneza mabanio na
vigawa maji. Miundombinu hiyo ilikuwa dhaifu na haikukidhi mahitaji ya
uzalishaji.
Baada ya Uhuru kilimo cha umwagiliaji kilitiliwa mkazo na miradi ya umwagiliaji
(skimu ilianzishwa ili kuongeza uzalishaji wa mazao na kupunguza utegemezi wa
mvua za msimu ambazo hazina uhakika na mtawanyiko mbaya wa mvua
unaobadilikabadilika kila mwaka).
Hadi sasa Juni 2011 kuna Skimu za umwagiliaji 43 ambazo zinatumika ndani ya
Mkoa. Skimu hizi zimejengwa kwa kutumia mbinu na njia za kisasa za kudumu
ili kufanya skimu iwe endelevu na kuwa na tija katika ngazi ya kaya hadi Taifa.
Mazao yanayolimwa katika skimu hizo ni: Mahindi, Mpunga, Maharage,
Vitunguu, Nyanya Mbogamboga na Zabibu.
65
Kutokana na miundombinu ya kudumu imefanya uzalishaji wa mazao kuongezeka
kutoka Tani 0.8 kwa hekta hadi Tani 2.5/ha za Mahindi na Mpunga tani 1/ha hadi
tani 3/ha Juni 2011.
(ii) MATUMIZI YA ZANA ZA KILIMO
Kilimo cha jembe la mkono kimeonekana hakina tija hivyo jembe la kukokotwa
na ng’ombe limeonekana kuwa na msisitizo mkubwa sana ili kuleta tija kwenye
kilimo. Baada ya Uhuru vituo vya kufundishia wanyamakazi vimeongezeka.
Matumizi ya majembe ya kukokotwa na wanyama kazi kabla ya Uhuru
hayakuwepo, baada ya Uhuru kuna ongezeko la majembe ya kukokotwa na
wanyama kazi. Wakulima wa Dodoma wamekuwa na mwamko mkubwa katika
matumizi ya zana za kisasa hivyo kumekuwa na ongezeko kubwa la matumizi ya
trekta ndogo (powertiller) na trekta makubwa ambayo hadi sasa kwa idadi
matrekta madogo ni 65 na matrekta makubwa ni 881.
(iii) HIFADHI YA CHAKULA
Kabla ya Uhuru chakula kilikuwa kinahifadhiwa kwenye vilindo.Baada ya Uhuru
kulikuwa na msisitizo wa kujenga maghala makubwa kwa ajili ya kuhifadhia
mazao ya wakulima. Maghala hayo yalijengwa na mradi wa mahindi IDA
(International Development Association), watu binafsi na serikali chini ya
Mpango wa Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (DADPs).
(iv) MASOKO YA MAZAO
Kabla ya Uhuru hapakuwepo na masoko ya mazao. Baada ya uhuru masoko
makubwa na yakisasa yalijengwa katika baadhi ya Wilaya likiwemo soko la
kimataifa la mahindi la Kibaigwa.
66
3.2.7. SEKTA YA MIFUGO
Mifugo ni chanzo cha ajira, chakula, kipato, nguvu kazi, mbolea, fahari, zawadi na
hata kwa ajili ya kufanyia malipo ya aina mbali mbali. Kwa kifupi, ufugaji ni sehemu
muhimu sana ya mfumo wa maisha ya wakazi walio wengi katika Mkoa huu.
Inakadiriwa kuwa idadi ya Kaya kati ya 150,000 hadi 200,000 sawa na 30% hadi 40%
ya kaya zote takriban 500,000 zilizopo hapa mkoani, wanajishughulisha na Ufugaji.
Mifumo ya Ufugaji Mkoani
Ufugaji Mkoani Dodoma unafanyika kwa mifumo ya aina nne;
(i) Ufugaji huria (extensive) – huu ndiyo mfumo mkuu ambapo mifugo
huchungwa katika maeneo yaliyotengwa kwa shughuli hizo ndani ya
kijiji.
(ii) Ufugaji huria na ndani (semi-intensive) – Mfumo huu unatumiwa na
wafugaji ‘wakisasa’ huko katika Ranchi ya Kongwa na Juva Holdings
Ltd naye wa Wilayani Kongwa.
(iii) Ufugaji wa ndani (zero grazing) – Unatumika zaidi kwa ng’ombe na
mbuzi wa maziwa
(iv) Unenepeshaji (Feedlotting ) – Mfumo huu uko Kongwa Ranch na
Juva Holdings Ltd
Aina na Idadi ya Mifugo
Mkoa una hazina kubwa ya mifugo ya aina mbalimbali. Sensa kamili ya mifugo
ilifanyika kwa mara ya mwisho mwaka 1984. Baada ya hapo, zimekuwa zikifanyika
sensa za sampuli tu na matokeo ya sensa hizo za sampuli yamekuwa ya utata na yenye
kuzua maswali mengi kutokana na kutofautiana na ufahamu wa wakazi wa mkoa.
Pamoja na hayo, makadirio ya idadi ya mifugo mkoani Dodoma katika mwaka huu wa
2009 ni yanaoneshwa katika Jedwali namba 2.1.
Wastani wa mm 400 hadi mm 600 za mvua kwa mwaka na kiangazi kirefu kinachozuia
uzalianaji wa haraka wa kupe waenezao magonjwa na kutokuwepo kwa ndorobo katika
maeneo mengi Mkoani ni miongoni mwa sababu zinazochangia ustawi mzuri wa
mifugo katika Mkoa
67
Jedwali Na 26 Aina na Idadi ya Mifugo Kiwilaya 2010
AINA YA
MIFUGO
IDADI YA MIFUGO KIWILAYA
BAHI CHAMWINO DODOMA KONDOA KONGWA MPWAPWA JUMLA
Ng’ombe wa Asili 189,925 185,659 105,340 418,480 98,006 167,976 1,165,386
Ng’ombe
walioboreshwa
83 1,971 3,660 394 8,978 1,240 16,326
Mbuzi wa Asili 39,530 45,865 65,878 276,853 69,894 135,495 633,515
Mbuzi wa maziwa 106 53 746 850 487 584 2,880
Kondoo 7,604 9,904 29,694 130,000 32,592 51,691 261,485
Nguruwe 808 4,423 3,826 2,420 32,768 12,825 52,647
Kuku wa Asili 314,788 236,047 104,323 525,000 373,180 164,600 1,717,938
Kuku wa Mayai 246 2,763 11,092 1,200 3,697 2,345 21,343
Kuku wa nyama 210 0 5,700 0 0 0 5910
Bata 440 1,350 2,519 433 5,627 1,117 11,486
Sungura 231 177 914 81,000 238 0 81,646
Simbilisi (Guinea
pig)
0 0 0 0 102 0 102
Mbwa 2,839 3,820 3,450 4,000 1,073 9,064 24,246
Punda 1,816 39,000 1,760 19,400 2,656 3,262 67,894
Farasi 0 0 0 0 6 0 6
Paka 1,781 493 1,120 2,000 237 793 6,424
Njiwa 189 0 0 512 487 2,100 3,288
Kanga 984 4,580 0 680 875 2,160 9,279
CHANZO: Afisa Mifugo wa Mkoa; Septemba 2009
68
Mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 50:
Katika kuadhimisha sherehe hizi za miaka ya 50 mambo mengi yamefanyika katika Sekta
ya Mifugo Mkoani Dodoma. Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya mambo yaliyofanyika.
(i) Ongezeko la Mifugo (ng`ombe, mbuzi, Kondoo, kuku na kuku).
(ii) Ogezeko la huduma za ugani.
(iii) Ongezeko la vyanzo vya maji ya kunywa kwa mifugo na ongezeko la
malisho.
(iv) Uboresha wa Mifugo ili kuongeza uzalishaji (A.I na kwa kutumia madume
na majogoo ya kisasa).
(v) Ongezeko la uthibiti wa magonjwa mbalimbali (Kinga na Tiba)
(vi) Ongezeko la upatikanaji wa masoko ya mifugo
(vii) Uanzishwa wa viwanda vidogo na uwekazaji vya usindikaji.
1.0. SHUGHULI ZILIZOFANYIKA TANGU UHURU
Kabla ya Uhuru Makao Makuu ya Idara ya Huduma za Mifugo yalikuwa
Mpwapwa katika kipindi cha kati ya mwaka 1920 hadi 1961 chini ya Utawala wa
Waingereza. Watawala wa Kiingereza walivutiwa na eneo hili kutokana na juhudi
za utawala wa kijerumani kujenga Josho la kwanza la Mifugo katika Ukanda wa
Afrika Mashariki mwaka 1905.
Baada ya Uhuru mikakati mbalimbali ilianza kufanyika ili kinua sekta ya Mifugo
katika mkoa wa Dodoma. Mikakati hii iliwekwa kupitia sera na sheria mbalmbali
za mifugo. Katika uzalishaji wa mifugo na mazao kumekuwa na changamoto
nyingi ambazo zimejitokeza kama upungufu wa malisho, magonjwa ya mlipuko.
Hivyo kupelekea katika kushuka uzalishaji na ubora wa mazao ya mifugo. Soko
lisilokuwa la uhakika la mazao ya mifugo limesabababisha kipato cha mfugaji
kushuka.
Baada ya uhuru kumekuwa na mabadiliko ya uzalishaji kutokana na Serikali
kuwa na mikakati ya kuthibiti milipuko ya magonjwa kwa kutoa chanjo bure au
kwa gharama nafuu. Aidha serikali imekuwa na mikakati ya kuwapatia soko la
69
uhakika (minada) kwa ajili mifugo yao. Aidha uzalishaji wa mazao ya mifugo
hususani kama maziwa, nyama na ngozi umeendelea kuongezeka na kuwapatia
kipato wafugaji. Hali hii imesaidia katika kupunguza umasikini miongoni mwa
wafugaji.
2.0. MIUNDO MBINU MBALIMBALI ILIYOJENGWA BAADA YA UHURU.
Kabla ya uhuru kulikuwa na majosho manne (4) tu, ambapo lilijengwa josho moja
moja kila Wilaya kwa ajili ya kuogeshea mifugo (ng’ombe, mbuzi na kondoo) ili
kuzuia magonjwa yaenezwayo na kupe. Josho la Kikombo Mpwapwa ni la
kwanza Afrika Mashariki na Kati. Baada ya uhuru majosho yaliendelea kujengwa
ambapo mpaka sasa kuna jumla ya majosho 110.
1.1. MALAMBO
Kabla ya Uhuru kulikuwa hakuna lambo hata moja baada ya Uhuru
Malambo yalijengwa ambapo hadi sasa kuna malambo 49.
1.2. KITUO CHA UCHUNGUZI MAGONJWA YA MIFUGO
Kabla ya uhuru kulikuwa na kituo kimoja cha uchunguzi magonjwa ya
mifugo. Sasa kituo hicho kimepanuliwa na kuwa cha kisasa zaidi na
kuwa na uwezo kutoa uchunguzi wa magonjwa ya mifugo katika kanda
ya kati DODOMA na SINGIDA.
1.3. VITUO VYA TIBA YA MIFUGO (VET CENTERS)
Kabla ya uhuru vituo vya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo vijijini
vilikuwa havipo, lakini baada ya uhuru vituo 12
1.4. MACHINJIO
Kabla ya uhuru hapa Mkoani palikuwa hakuna machinjio sehemu chini ya
mti ilichaguliwa na kuwa ndipo mahali mnyama anachinjwa, kwa sasa
kuna machinjio 6 kila Wilaya kuna machinjio moja.
70
1.5. MABANIO
Kabla ya uhuru kulikuwa na mabanio manne (4) kulikuwa na banio moja
kila Wilaya wakati huo wilaya zilikuwa nne tu, baada ya uhuru mabanio
yaliendelea kutengenezwa hadi kufikia jumla ya mabanio 20.
1.6. MINADA
Kabla ya Uhuru kulikuwa na minada mikubwa 8 ambapo shughuli za
kununua na kuuza mifugo ilikuwa inafanyika, kwa sasa kuna jumla ya
minada 30.
1.7. MABANDA YA NGOZI
Kabla ya uhuru kulikuwa na jumla ya mabanda 6 ya ngozi, baada ya
Uhuru mabanda ishirini na manne (24) yamejengwa.
1.8. NYUMBA ZA WATUMISHI
Kabla ya Uhuru kulikuwa hakuna nyumba za watumishi na baada ya
Uhuru jumla nyumba 20 za watumishi zilijengwa:
1.9. IDADI YA WATUMISHI
Kabla ya Uhuru kulikuwa na watumishi 30 wa mifugo, na baada ya
Uhuru, idadi ya watumushi imeongezeka hadi kufikia 300.
1.10. VITENDEA KAZI
Kabla ya Uhuru idara ya mifugo ilikuwa haina Pikipiki wa Gari, kwa sasa
Idara ina Pikipiki 104 na magari 7 ya Mifugo
2.0. KITUO CHA UTAFITI WA MIFUGO
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Mifugo (NLRI) Mpwapwa, imeundwa upya kufuatia
muundo mpya wa Serikali ya awamu ya nne iliyoundwa baada ya Uchaguzi Mkuu
uliofanyika mwezi Desemba 2005. Muundo huo mpya umepelekea kuundwa kwa
Wizara mpya ya Maendeleo ya Mifugo. Kwa sasa Taasisi hii inawajibika moja kwa
moja kwa Katibu Mkuu katika kufanya tafiti za uzalishaji wa mifugo ili kukidhi
matakwa ya nchi nzima, tofauti na mfumo wa zamani wa kufanya tafiti kikanda
(zones). Tunaishukuru Serikali kwa muundo huu ambao unategemewa kukidhi
matakwa ya Wadau wengi. Taasisi hii, kwa muda takriban karne nzima, imekuwa
71
ikitumika kama kitovu cha utafiti wa mifugo hapa Tanzania, ikiwa inabadilika
shughuli na majina mara kwa mara.
3.0. KITUO CHA UTAFITI WA MAGONJWA YA MIFUGO-VIC
Kituo hiki ni Maabara ya Uchunguzi wa Maradhi ya Mifugo katika Kanda ya Kati
inayojumuisha Mikoa ya Dodoma na Singida baada ya Morogoro kuingizwa
Kanda ya Mashariki kuanzia 1998. Kipo Km 2 kutoka Mpwapwa mjini katika
eneo la Kikombo ambako pia kuna Kituo cha Taifa cha Utafiti wa Mifugo NLRI
na Chuo cha Mafunzo ya Wataalam wa Tiba na Uzalishaji wa Mifugo ‘LITI’.
Kihistoria Kituo hiki kilianzishwa mwaka 1959 wakati wa Wakoloni kikihudumia
Mikoa mitatu (3) ya Morogoro, Dodoma na Singida Serikali ya wakati ule
ilipoanzisha Maabara za Utambuzi na Uchunguzi wa Magonjwa katika Kanda
mbalimbali za nchi. Kituo cha Mpwapwa ni kimoja kati na Vituo saba vya namna
hii vilivyoko nchini. Vingine vipo Arusha, Iringa, Mtwara, Mwanza, Tabora na
Temeke. Kituo hiki cha Kanda ya kati kinahudumia takribani Ng’ombe
3,198,000, Mbuzi 994,000, Kondoo 446,800, Kuku 2,329,700, Nguruwe 22,500,
Punda 97,200, Mbwa 26,860 na Paka 10,160.
72
3.2.8. SEKTA YA USHIRIKA 1961 HADI 2011
UTANGULIZI
Katika kipindi mara baada ya uhuru mwaka 1961, vyama vya ushirika
vilichukuliwa kama njia dhahiri na pekee ya kumuendeleza mkulima mdogo na
kumlinda dhidi ya unyonyaji wa wachuuzi. Kwa mantiki hiyo serikali ilitoa
msukumo mkubwa wa kuanzisha vyama vikuu katika mikoa ambako haja ya
kuwa na ushirika ilikuwa haijatokea miongoni mwa wananchi wenyewe.
Katika mkoa wa Dodoma Ushirika ulianza kwenye miaka ya 1960/61 sambamba
na vuguvugu la kupatikana kwa uhuru mwaka 1961. Vyama vya ushirika mkoa
wa Dodoma, kama ilivyokuwa kwa mikoa mingine nchini vilianzishwa kwa
madhumuni ya kununua na kuuza mazao ya wakulima kupambana na
wafanyabiashara binafsi waliojulikana kama “middlemen” ambao waliwapunja
bei wakulima.
Kwa kuanzia vyama vya msingi vya kila wilaya katika ya wilaya tatu za wakati
huo yaani Dodoma, Kondoa na Mpwapwa vilijiunga na kujiundia vyama vikuu
vyao, ambavyo vilikuwa ni Wella Cooperative Union kwa Dodoma, Kondoa
Cooperative Union na Mpwapwa Cooperative Union. Vyama vikuu hivi baadaye
vililazimika kuvunjika na vyama vyake vya msingi kujiunga pamoja kuunda
chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa yaani Central Region Cooperative Union –
CRCU Ltd. (Yalikuwa ni maelekezo ya serikali kuunda vyama vikuu vya mikoa).
Mwezi Mei 1976 Vyama Vikuu na vyama vyake vya msingi vya ununuzi wa
mazao vilivunjwa nchini kote ikiwa ni pamoja na Central Region Cooperative
Union Ltd. (CRCU Ltd) ambayo shughuli zake zilichukuliwa na NMC na
GAPEX kwa ajili ya ununuzi wa mazao, RTC kwa shughuli za ugawaji na
KAUDO kwa shughuli za usafirishaji na uchukuzi.
Vyama vya ushirika vilirejeshwa tena mwaka 1983/84 ambapo mkoani Dodoma
ikaundwa Central Region Cooperative union (1984) Ltd kutokana na vyama vya
Ushirika vya Msingi vilivyoanzishwa wakati huo. Madhumuni ya kuanzishwa
CRCU (1984) Ltd yalikuwa yale yale ya ununuzi wa mazao ya wakulima. Vyama
73
vya ushirika vya wakati huo vilianzishwa kwa mtaji wa mikopo mikubwa kutoka
mabenki na vilishindwa kulipa mikopo hiyo hatimaye kulazimika kufilisiwa na
hivyo kukosekana kwa shughuli za ununuzi wa mazao mkoani.
UANZISHAJI WA VYAMA VYA USHIRIKA VYA AINA MBALI MBALI
BAADA YA MWAKA 1961
Kwenye mwaka 1962 na kuendelea, katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru, vyama
vya Ushirika vya aina mbali mbali vilianzishwa. Hadi kufikia tarehe 31 Machi
2011 kulikuwa na vyama vya ushirika vya msingi 212 kwa mchanganuo ufuatao:-
1. Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) -174
2. Ushirika wa Kilimo na Masoko (AMCOS) -15
3. Ushirika wa umwagiliaji -3
4. Ushirika wa wafugaji -1
5. Ushirika wa nyumba -1
6. Ushirika wa Huduma -1
7. Aina nyingine -17
Aidha kuna chama kimoja cha Ubia
Hadi kufikia tarehe 31 Machi 2011 SACCOS zilikuwa na wanachama 65,362 kati
ya hao wanaume wakiwa 20,300, wanawake 43,733 na vikundi 1,319; hisa zenye
thamani ya Shs. 2,151,915,207/-, akiba za Shs. 5,158,123,518 na amana za Shs.
854,073,173/-.Zilikuwa zimetoa mikopo ya Shs. 32,753,484,456/- na marejesho
yalikuwa Shs.21,997,000,846/-.
Vyama vingine mbali na SACCOS vilikuwa na wanachama 3,494 kati ya hao
1,934 wakiwa wanaume, wanawake 1,534 na vikundi 26.Vyama hivi vilikuwa na
hisa zenye thamani ya Shs. 65,292,000/-.
MATATIZO YALIYOUKUMBA USHIRIKA
Ushirika umekumbwa na matatizo makubwa katika kipindi cha miaka 50 iliyopita
Matatizo hayo ambayo kwa kiasi fulani yamechangia kuzorota kwa ushirika mkoa
wa Dodoma ni pamoja na yafuatayo:-
• Vyama kutokuwa na mitaji ya kutosha
74
• Elimu duni ya ushirika kwa Viongozi, Watendaji na Wanachama
• Ukosefu wa Watendaji wanaofaa kwenye vyama
• Uongozi mbovu, ubadhirifu na wizi katika ushirika
• Vyama kushindwa kulipa madeni
• Wanachama kutokuona kuwa vyama hivyo ni vyao na kuwaachia
watendaji kuviteka nyara.
Kamati ya maalum ya Rais ya kumshauri kuhusu kufufua, kuimarisha na
kuendeleza ushirika ya mwaka 2000 pamoja na kuainisha mambo ambayo
yalikuwa ni kikwazo katika kufikia malengo ya ushirika, ilitoa mapendekezo ya
utatuzi. Moja ya matokeo makuu ya jitihada hizo ni kuandikwa kwa Sera ya
Maendeleo ya Ushirika ya mwaka 2002 na kutayarishwa na kupitishwa kwa
Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 20 ya mwaka 2003.
SERA YA MAENDELEO YA USHIRIKA YA MWAKA 2002
Sera ya Maendeleo ya Ushirika ya mwaka 2002 imeandaliwa kwa kuzingatia
umuhimu wa kuwepo kwa mazingira mwafaka kwa vyama vya ushirika kufanya
shughuli zake kwa ufanisi zaidi na kumudu ushindani katika mfumo mpya wa
soko huru na utandawazi. Sera inazingatia ujenzi wa ushirika shirikishi, endelevu
na wenye nguvu za kiuchumi.Maeneo yafuatayo yametiliwa mkazo:-
• Ujasirishaji wa wanachama (member empowerment)
• Ustawi wa vyama vya ushirika vyenye uhai wa kiuchumi na endelevu
vinavyodhibitiwa na kumilikiwa na wanachama wenyewe
• Kuimarisha vyama vya msingi viweze kufanya shughuli zake kibiashara na
kuhimili ushindani na kuwanufaisha wanachama
• Kuwepo kwa uongozi wenye ujuzi na uwezo wa kuendesha vyama vya
ushirika kibiashara na kuwajibika kwa wanachama
• Viongozi kuajiri watendaji wenye vipaji vya ujasiriamali na uwezo wa
kutafsiri dira na mipango ya maendeleo ya chama.
• Kuhamasisha uanzishwaji na uimarishaji wa vyama vya akiba na mikopo na
uundwaji wa vyombo vya fedha vya wanachama wenyewe ili kuimarisha
upatikanaji wa mitaji.
75
• Kutambuana kuunga mkono jitihada za vikundi vidogo vidogo vya uzalishaji
mali na biashara
• Kuhimiza wanawake na vijana pamoja na makundi mengine maalumu
kujiunga nakuchukua nafasi za uongozi na ajira.
• Kuhimiza utoaji wa elimu ya ushirika, mafunzo na huduma za utafiti
zinazolenga uwezeshaji wananchama
• Kuhimiza uazishwaji wa vyama vya ushirika katika sekta zote za kiuchumi na
kijamii.
SHERIA YA VYAMA VYA USHIRIKA NA.20 YA 2003
Sheria hii ilitungwa baada ya kufanya mapitio makubwa katika Sheria ya Vyama
vya Ushirika Na. 15 ya mwaka 1991 na kwa ajili ya kutekeleza Sera ya
Maendeleo ya Ushirika. Maeneo muhimu yaliyoangaliwa kwa nafasi ya juu katika
mabadiliko ya sheria ni:-
• Kuimarisha nguvu za kiuchumi (economic viability) za vyama vya
ushirika pamoja na kuondoa hali ya vyama kuwa tegemezi wa kudumu
kwa Serikali.
• Mfumo wa vyama vya ushirika nchini.Sheria inawapa wanachama uwezo
na mwongozo wa kuweka mfumo unaokidhi mahitaji yao.
• Uchaguzi na maadili ya viongozi. Sheria inaweka utaratibu wa uchaguzi
wa viongozi na ajira kwa watendaji unaozingatia maadili ya uongozi
(Code of Conduct)na utendaji makini katika vyama.
• Vipindi vya uongozi vimerekebishwa ili kuondoa tabia ya baadhi yao
kuwa madarakani kwa muda mrefu. Kila baada ya miaka mitatu theluthi
moja inalazimika kujiuzulu na hawagombei tena mpaka baada ya miaka
mitatu.
Kufuatilia kesi za ushirika, Sheria sasa imeweka kipengele kinachowapa
Maafisa maalum (Special Prosecutors) kusimamia kesi za vyama vya
Ushirika.
76
3.2.9. SEKTA YA UJENZI NA MAWASILIANO:
1.0. HUDUMA ZA BARABARA:
Pamoja na kuwepo barabara zilizokuwa zikitumiwa na Waarabu wakati
wa biashara ya Utumwa na Wakoloni kwa kupita kwa miguu, mtandao wa
Barabara zilizokuwa zikitambuliwa kwa wakati huo ulikuwa ni mdogo
sana. Baada ya Uhuru mwaka 1961 mtandao wa Barabara umekuwa
ukiongezeka kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya barabara ambazo
hazikuwa rasmi na pia kuanzishwa kwa barabara nyingine ambazo
hazikuwepo kabisa.
Baada ya Uhuru mgawanyo wa Barabara nchini koteulikuwa kama
ifuatavyo:
(i) Barabara kitaifa
(ii) Barabara za Mkoa
(iii) Barabara za Wilaya
(iv) Barabara za Vijijini na Mitaa
Menejimenti ya barabara hizi ilihusika. Mamlaka chini ya Mhandisi
Mkuu, barabara kuu na barabara za mkoa. Mtandoa wote wa barabara
ndani yaMkoa ulikuwa na kiasi cha Km. 20 tu za lami kati ya km. 2,280 za
mtandao wote ambao ulikuwa wa tabaka la udongo.
Aidha katika kipindi hiki sheria ya barabara iliyokuwa ikitumika ni ile ya
“The Hglway Ordinance, (AP. 1967) iliyotungwa mwaka 1932 ambayo
imekuwa ikifanyiwa marekebisho. Sheria mpya yas barabara namba 13 ya
mwaka 2007 ndio inayotumika sasa, ambayo imegawanya barabara katika
makundi yafuatayo:
(i) Barabara chini ya Wakala wa barabara ambazo zinahusika
barabara kuu na barabara za Mkoa
(ii) Barabara chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa zinahusisha
barabara za Wilaya, barabara za Vijijini na barabara za Mjini na
barabara za jumuia.
77
Hali ya barabara katika kipindi hiki haikuwa nzuri kwa vile nyingi zilikuwa za
udongo ambazo hazikuweza kupitika nyakati zote za mwaka.
Mkoa wa Dodoma sasa una mtandao wa barabara wenye jumla ya urefu wa
kilometa 5,965.95 ambao umegawanyika katika madaraja mbalimbali kama
inavyooneshwa katika majedwali yafuatayo:
Jedwali Na. 27 (a) Mtandao wa Barabara chini ya Wakala wa Barabara Mkoa 2011
Mamlaka Urefu
(Km)
Urefu wa kila daraja (Km) Aina ya tabaka (km)
Barabara za
Mkoa (km)
Barabara
Kuu (km)
Barabara
zisizo za lami
Barabara
za lami
Wakala wa
Barabara
1,656.65 1,102.04 354.6 1,442.58 214.07
Jedwali Na. 27 (b) Mtandao wa Barabara chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa
2011
Mamlaka Urefu
(Km)
Urefu wa kila daraja (Km) Aina ya tabaka (km)
Barabara
za Wilaya
(km)
Barabara
za
Vijijini
(km)
Barabara
za Mjini
(km)
Barabara za
Changarawe
Barabara
za
Udongo
Barabara
za lami
Halmashauri
za Wilaya
na Manispaa
4,309.3
1,744.03 2,280.1 284.9 857 3,393.5 58.8
Mafanikio:
Kuanzishwa kwas Bodi ya Mfuko wa Barabara
Mnamo mwaka 1998, Serikali ilianzisha Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund Board)
ambayo ilianza kazi rasmi mwaka 2000 kwa lengo la kuboresha miundombinu hii
muhimu ya Barabara kwa fedha za ndani ya nchi kutokana na kodi itokanayo na bidhaa
ya mafuta. Tangu kuanzishwa kwa mfuko huu, Barabara Kuu, barabara za Mikoa, Wilaya
na Vijiji zimeweza kuboreshwa hadi kupandishwa madaraja na kuwezesha kiasi cha 55%
ya Mtandao wote was barabara ndani ya Mkuoa kuwa katika hali nzuri ya kuridhisha.
78
Changemoto:
• Serikali imekuwa ikitenga fedha kidogo kwa ajili ya matengenezo ya
barabara hivyo kufanya hali ya barabara kutokuwa katika viwango
vinavyotarajiwa na watumiaji.
• Uharibifu wa Mazingira unaotokana na Kilimo holela kwenye miinuko
pamoja na ufyekaji wa miti vimekuwa vikisababisha matengenezo ya
mara kwa mara katika barabara ikiwa ni pamoja na ongezeko la mahitaji
makubwa ya vivuko.
2.0. MAWASILIANO YA SIMU:
Mkoa wa Dodoma ulianza kuwa kitovu cha mawasiliano mwaka 1955 ambapo
kilijengwa kituo cha simu ya Upepo cha aina ya VHF kwenye mlima wa Viganga.
Hata hivyo kutokana na sababu zisizoeleweka, kituo hicho hakikutumiwa mpaka
mwanzoni mwa dahari za miaka 1960 ambayo ilikuwa ni miaka sita baada ya
kumalizika kujengwa kwake. Kituo hiki kilikuwa ndiyo chanzo cha mipango ya
simu za upepo na baadaye kilipevuka kwa kufuatana na maendeleo ya kisayansi.
Huduma za Simu baada ya Uhuru:
Baada ya nchi yetu kupata Uhuru, huduma za mawasiliano ya simu yalikuwa ya
Siwaya ambapo kulikuwa na waya zilizopita juu ya nguzo ambazo zilipita kando
ya barabara ili kusaidia matengenezo ya simu endapo waya zitakatika na
kusababisha kutokuwepo kwa mawasiliano ya simu. Huduma hii ilisaidia
kurahisisha mawasiliano katika maeneo muhimu ya kiutawala hususani ofisi za
Wakuu wa Mikoa na Wilaya.
Mnamo mwaka 1976, mtambo wa mawasiliano ya simu wenye laini 600
ulifunguliwa na aliyekuwa Makamu wa Rais Ndugu Aboud Jumbe. Mtambo huu
ulikuwa wa kupiga moja kwa moja (Automatic Cross – bar Telephone exchange
with STD Services). Kuziduliwa kwa mtambo huu kulirahisisha zaidi
mawasiliano ya simu ndani na nje ya nchi. Hadi leo kituo hiki kimekuwa ndiyo
kitovu cha mawasiliano kwa Afrika na Ulaya.
79
Teknolojia hii iliendelea kutumika hadi mwaka 1998 ambapo Teknolojia ya simu
za mikononi ilianza kutumika. Tangu wakati huo makampuni kadhaa ya simu
yamefunga mitambo yao Mkoani Dodoma. Makampuni hayo ni TTCL, TIGO
(zamani Mobitel), VODACOM, CELTEL (sasa Airtel) pamoja na ZANTEL.
3.0. HUDUMA ZA USAFIRI WA ANGA:
Kabla ya Uhuru:
Huduma za Usafiri wa anga katika Mkoa wa Dodoma zilianza mwaka 1928 baada
ya kukamilika kwa ujenzi wa uwanja wa Dodoma. Ndege ya mwanzo ilitua
Dodoma mnamo mwaka 1928 ikiendeleshwa na Luteni Bentley ikiwa njiani toka
Nairobi kwenda Johannesburg.
Mnamo mwaka 1932Sshirika la Ndege la Impreial Airways lilianzisha safari za
ndege za kwenda Cape Town kupitia Dodoma. Kuanzia hapo usafiri wa anga
ukawa ni sehemu ya maisha ya wakazi wa Dodoma.
Baada ya Uhuru:
Katika kipindi cha miaka hamsini ya Uhuru wa nchi yetu Uwanja wa Ndege
uliopo eneo la Area “C” umepanuliwa na kufikia hekta 98 pamoja na kuwekewa
lami. Aina ya ndege zinazotua katika uwanja huu ni Fokler 50, 28 na Cessna.
Pamoja na kuwa na uwanaja huu wa ndege Serikali ina mpango wa kujenga
uwanja mkubwa wa Kimataifa katika eneo la Kitelela nje kidogo ya Mji wa
Dodoma. Uwanaja huu utakapokamilika utakuwa na ukubwa wa mita za mraba
4,515,342 (p km x 4.5 km). Uwanja huu utawapatia ajira watu zaidi ya mia moja
kutoka ndani na nje ya nchi na uwezo wa kupokea idadi kubwa ya ndege kwa
wakati mmoja
• Ndege Tano aina ya Boeing 737 – 800
• Ndege Tatu aina ya Airbus – A. 380
• Ndege Tatu aina ya Boeing 737 – 800 pamoja na Airbus A.380
• Ndege mbili aina ya Airbus A.380 pamoja na Boeing 737 – 800.
80
4.0. KAMPUNI YA RELI TANZANIA:
Reli ya kati “Centrl line” kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma ilianza kujengwa
na Wajerumani mwaka 1906, ilipofika katikati ya mwaka 1910 Reli ilikuwa tayari
imefika Mkoani Dodoma. Kituo cha Dodoma kilifunguliwa kwa usafiri mnamo
tarehe 01 Novemba 1910. Ujenzi wa Reli hii ulifikia mwisho wake katika Mji wa
Kigoma mwaka 1914.
Baada ya Vita Kuu ya kwanza ya Dunia iliyoanza mwaka 1914 hadi 1918
Wajerumani walishindwa na Waingereza katika vita hiyo na hivyo Tanganyika
kutawaliwana Waingereza. Waingereza waliendeleza ujenzi wa Reli na mnamo
mwaka 1928 Reli ilifika Mwanza kutoka Tabora.
Katika Mkoa wa Dodoma kulijengwa Reli kutoka Msagali hadi Kongwa mwaka
1947 na baada ya miaka miwili yaani 1949 Reli hiyo ilifika Hogoro (kongwa).
Dhumuni la ujenzi wa Reli hii ni kuwa eneo hili la Kongwa lilikuwa mashuhuri
kwa uzalishaji wa Karanga. Hata hivyo Reli hii iling’olewa baadaye kutokana na
kushindwa kwa uzalishaji wa Karanga.
Madhumuni ya Wakoloni kujenga Reli:
Lengo kuu la Wajerumani kujenga Reli ya Kati lilikuwa kusafirisha mazao ya
biashara kama Katani, Kahawa, Pamba, Karanga na Ngano, kutoka maeneo
yauzalishaji kwenda kwenye masoko ndani na nje ya nchi ili kukidhi mahitaji
yaliyotokana na mapinduzi ya viwanda (Industrial Revolution) huko Ulaya.
Sambamba na hilo walianzisha pia usafirishaji wa Abiria.
Katika Mkoa wa Dodoma, Reli hii imepita katika Wilaya nne za Mpwapwa,
Chamwino, Dodoma Mjini na Bahi, ambapo kuna jumla ya vituo 10. Vituo hivi ni
Msagali, Gulwe na Godegode (Mpwapwa), Igandu (Chamwino) Kikombo,
Ihumwa, Dodoma na Zuzu (Dodoma Mjini) na Kigwe na Bahi (Bahi).
81
Mafanikio Sekta ya Reli:
(i) Mtandao was Reli umesaidia wakulima kupata Mbolea na Pembejeo
kutoka viwandani kwa matumizi ya kilimo
(ii) Treni ina uwezo wa kubeba mizigo mikubwa na mingi kwa wakati mmoja
na kwa gharama nafuu. Hali hii inawawezesha wafanya biashara kuuza
bidhaa zao kwa bei nafuu.
(iii) Reli ya Tanzania imechangia kuongeza Ajira kwa kuajiri wafanyakazi
Mijini na Vijijini. Kwenye Magenge na Stesheni zake. Hali kadhalika
imetoa fursa kwa jamii inayoishi karibu na maeneo hayo kufanya biashara
ya kuuza vyakula na bidhaa mbalimbali.
(iv) Ajira za wafanyakazi wa Shirika la Reli zimechangia kukuza mahitaji ya
Mifuko ya Jamii ambayo nayo hutumia sehemu ya pesa zinazokusanywa
kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo.
(v) Shirika la Reli limechangia kuongeza pato la Taifa.
Changamoto zilizopo:
(a) Uhaba wa fedha za uendeshaji na uwekezaji kumeasababisha uchakavu
mkubwa wa miundombinu, mabehewa, injini pamoja na vitendea kazi
vingine.
(b) Kupungua kwa vitendea kazi kama vile injini na mabehewa ya abiria na
mizigo kutokana na kuchakaa na hivyo kushindwa kukidhi mahitaji ya
usafirishaji wa mizingo na abiria kwa ufanisi.
(c) Ushindani mkali uliopo kati ya Reli na Barabara ukichangiwa na kuzorota
kwa huduma za Reli, imepelekea wateja wengi kuhamia kwenye usafiri wa
barabara. Mizigo inayosafirishwa kwa njia ya Barabara inafika mapema
kuliko inayosafirisha kwa treni. Hii ni kwa sababu ya ujenzi wa barabara nzuri
kwenda Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Tabora na hata Mikoa ya Mara na
kagera.
(d) Majanga makubwa kama vile mafuriko yamekuwa tishio kubwa kwa upande
wa Reli kama yale ya mwaka 1968, 1998 na 2010 ambapo Shirika la Reli
lilisitisha huduma zote za usafirishaj abiria namizigo kuanzia Dar es Salaam.
82
(e) Uhujumu wa njia za mawasiliano zilizojengwa kwa waya wa shaba na hata
zile za mkonga wa waya za “fibre optic cable” zilizochimbiwa kwenye mtaro
kandokando ya tuta la reli. Na hivyo kukosekana kwa mawasiliano kati ya
Stesheni na Stesheni.
3.2.10. SEKTA YA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAZI
UTANGULIZI
Sekta ya Ardhi ni mojawapo ya sekta muhimu hasa ikizingatiwa kwamba
shughuli zote za kiuchumi na kijamii zinafanyika kwenye ardhi. Katika
kuhamasisha Wananchi kutumia ardhi yao kikamilifu, juhudi za kupima mipaka
ya vijiji, kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi vijijijni, pamoja na kupima
viwanja mijini, zinaendelea vizuri. Aidha elimu kwa Wananchi kuhusu sheria na
miliki za ardhi, kwa lengo la kutumia hati miliki kupata mikopo na kujikwamua
kiuchumi, zinaendelea kutolewa.
Ardhi ya uwekezaji:
Pamoja na wananchi wengi kuhamasika na kupata miliki za mashamba yao, Mkoa
una maeneo yenye jumla ya hekta 137,714 kwa ajili ya wawekezaji. Kati ya hizo,
hekta 114,100 zinafaa kwa ufugaji(Ranch),hekta 4,950 kwa kilimo cha zabibu,
hekta 9,700 kwa hifadhi ya misitu na ufugaji nyuki, na zilizobaki ni kwa mazao
mengine. Aidha Mkoa una jumla ya hekta 32,715 ambazo zinafaa kwa kilimo
cha umwagiliaji.
Mbali na vijijini, katika Manispaa ya Dodoma, kuna viwanja vyenye jumla ya
ukubwa wa hekta 266 ambavyo ni kwa uwekezaji kwa matumizi mbali mbali
kama ujenzi wa viwanda, hoteli za kitalii, shule, nk.
Utatuzi migogoro:
Utatuzi migogoro hufanyika kadri inavyojitokeza kwa Viongozi wa Wilaya na
wataalam wa pande husika, kushirikisha wananchi husika. Migogoro mingi
iliyoainishwa na kamati za kushughulikia migogoro ya ardhi katika Wilaya tayari
83
imetatuliwa. Iliyobaki mingi ni ile ambayo kesi zake ziko mahakamani. Kwa
ujumla, sasa malalamiko yanayotokana na migogoro ya ardhi, yamepungua kwa
kiasi kikubwa.
Hata hivyo, suluhisho la kudumu, ni kwa kila kijiji kuwa na mpango wa matumizi
bora ya kijiji chake, na, kila eneo lililopangwa kumilikishwa kwa mwenyewe.
Ndipo kila mmiliki atalinda mipaka ya adhi yake kwa mujibu wa sheria, na
kuitumia hati miliki kupata mikopo.Kwa kuhamasisha na kuwashirikisha
Wanavijiji, tumeanza kazi ya upangaji wa matumizi bora ya ardhi katika vijiji.
Uboreshaji wa Makazi:
Kutokana na uduni wa Makazi katika Mkoa wetu, mwaka 1998, Serikali ya Mkoa
ilianzisha progamu ya uhamasishaji wa ujenzi wa nyumba bora. Wakati programu
hiyo inaanzishwa, kulikuwa na wastani wa nyumba bora wa asilimia
25(25%).Programu hiyo ilishirikisha Taasisi za ki- Serikali na zisizo za ki -
Serikali. Mikakati iliyotumika ni kuhamasisha na kushauri yafuatayo:-
• Wafugaji wakubwa kuuza baadhi ya mifugo yao ili kujijengea nyumba bora.
• Wakulima kutumia mauzo ya mazao yao kujijengea nyumba bora.
• Wananchi kujiunga katika vikundi vya ushirika wa kujengeana nyumba bora-
SACCOS.
• Waliopata miliki za kisheria (hati) za maeneo au mashamba yao, kutumia hati
zao kupata mikopo ili wajijengee nyumba bora.
• Mashirika na Taasisi mbali mbali kutoa mikopo kwa watu binafsi na vikundi
kwa ajili ya ujenzi wa nyumba bora.
Kutokana na programu hiyo, ubora wa Makazi katika Mkoa umeongezeka na
kufikia wastani wa asili mia 45(45%) hasa Wilaya ya Kondoa ambao
wamehamasika sana kujenga nyumba za matofali ya kuchoma na
bati.Uhamasishaji unaendelea kwa lengo la Mkoa kuondokana kabisa na
umasikini wa nyumba ifikapo 2025.
84
Kuanzishwa kwa Mkoa na Wilaya
Kama ilivyo ada kuanzishwa kwa Mkoa au Wilaya, Serikali inatoa tangazo rasmi
linaloelezwa mipaka ya Mamlaka hayo. Matangazo ya Serikali (General Notices
– GN) yaliyoanzishwa Mamlaka mbalimbali ni kama ifuatavyo:-
• GN No. 450 ya tarehe 27.9.1963 Kuanzishwa Mkoa wa Dodoma
• GN No. 21 ya tarehe 1.3.1996 Kuanzishwa Wilaya ya Kondoa
• GN No. 312 ya 17.10.1952 Kuanzishwa Wilaya ya Mpwapwa
• GN. No. 217 ya 22.9.1950 Kuanzishwa kwa Wilaya ya Dodoma
• GN No. 349 ya 8.11.1996 Kugawanywa Wilaya ya Mpwapwa kuwa Wilaya
mbili za Mpwapwa na Kongwa
• GN. No. 190 ya 31.8.2007 Kugawanywa Wilaya ya Dodoma Vijijini kuwa
Wilaya mbili za Bahi na Chamwino.
Hadi sasa Mkoa wa Dodoma una jumla ya Wilaya sita (6) nazo ni Bahi,
Chamwino, Kongwa, Kondoa, Mpwapwa na Dodoma Mjini ambayo
haikuandaliwa tangazo baada ya eneo lake lote kuingizwa kwenye Mamlaka ya
Ustawishaji Makao Makuu hapo mwaka 1973. Inategemewa kuwa Wilaya mpya
ya Chemba itaanzishwa baada ya kuigawanya Wilaya ya Kondoa.
Shughuli kuu za Sekta ya Ardhi
(i) Kutafsiri mipaka iliyotangazwa na matangazo ya Serikali.
(ii) Kusimamia upimaji wa Mipaka ya vijiji ndani ya Wilaya mbalimbali.
(iii) Kusimamia uendelezaji wa makazi katika Halmashauri mbalimbali kwa
kubuni michoro mbalimbali.
(iv) Kupima viwanja na mashamba kwa usimamizi wa kila Halmashauri ya
Wilaya na Manispaa Mkoa ukichukua nafasi ya ushauri, udhibiti na
ukaguzi wa kazi mbalimbali.
(v) Kusimamia upangaji wa matumizi Bora ya Ardhi za vijiji vilivyo ndani ya
Mkoa.
(vi) Kuhamasisha ujenzi wa makazi/nyumba bora kwa ajili ya afya za jamii.
(vii) Kusimamia na kudhibiti uharibifu wa mazingira.
85
Mafanikio
(a) Kumekuwa na ongezeko la idadi ya viwanja vilivyopimwa kuanzia miaka 20
kabla ya Uhuru na Miaka 50 baada ya Uhuru.
(b) Kumekuwa na maendeleo katika upangaji wa Matumizi Bora ya Ardhi katika
vijiji mbalimbali pamoja na maeneo ya uwekezaji.
(c) Uelewa wa wananchi juu ya sera na sheria za Ardhi na haki zao kikatiba
umeongezeka.
Changamoto
1. Kuelimisha Jamii juu ya umuhimu wa kumiliki ardhi/maeneo ya kisheria kwa
kutumia sera na Sheria za Ardhi kama zilivyoendelea kurekebishwa.
2. Kuzishauri Halmashauri za Wilaya na Manispaa kuongeza kasi ya upimaji wa
viwanja kwa ajili ya matumizi mbalimbali kwa kuwatumia wataalam
Serikalini na sekta binafsi.
3. Kuzishauri Halmashauri kununua vifaa vya kisasa ili kuongeza ufanisi na
hatimaye kumudu ongezeko la kazi na mahitaji ya teknolojia ya kisasa.
Hitimisho:
Jedwali lifuatalo linaonesha hali ilivyokuwa na ilivyo sasa kwa kipindi chote cha
miaka 50 ya Uhuru. Baadhi ya Halmashauri zimepiga hatua kubwa ya Maendeleo.
86
87
3.2.11. SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARA
UTANGULIZI:
Biashara ni nyanja muhimu kwani ndio njia rahisi ya kuwapatia wananchi
bidhaa/huduma ambazo hawawezi kuzizalisha wenyewe lakini ni muhimu kwa ajili ya
kukithi mahitaji yao ya kila siku. Kabla ya Uhuru shughuli za kibiashara katika Mkoa wa
Dodoma hazikuwa kubwa sana. Maduka mengi yaliyofunguliwa kipindi hicho yalikuwa
na bidhaa nyingi kutoka Ulaya na Asia kama vile Vitambaa kutoka Japani, Majembe ya
mkono kutoka Ujerumani na India, vyombo vya Chuma vya matumizi ya nyumbani
pamoja na vyakula vya mikebe kutoka Uingereza.
Katika miaka ya 1940 hadi 1961, baadhi ya Miji hususan Makao Makuu ya Wilaya
ilianza kukua kibiashara kutokana na kuongezeka kwa shughuli za kimaendeleo. Katika
kipindi hicho idadi ya watu ilianza kuongezeka, ujenzi wa vituo vya huduma kama Post,
Hospitali, Misikiti, Makanisa pamoja na Makumbusho ya Maabara ya shughuli za
Madini. Aidha vituo vya Stesheni ya Reli navyo vikaanza kukua kama vituo vya biashara
Hali ya Biashara/Viwanda:
Kabla na baada ya uhuru (miaka ya mwanzo ya uhuru) hali ya biashara ilikuwa duni na
viwanda katika Mkoa wa Dodoma havikuwepo. Kulikuwako na kiwanda kimoja tu
(kidogo) ambacho kilikuwa kinasindika zabibu kwa ajili ya kutengeneza mvinyo –
DOWICO. Bidhaa za kiwanda hiki hazikuwa za msingi kwa mahitaji ya wananchi.
Upatikanaji wa bidhaa haukuwa wa kurithisha kwani vituo vya usambazaji vilikuwa
vichache – maduka. Hata hivyo shughuli hizi zilikuwa zinafanywa na Wahindi na
Waarabu - wengi wao wakiwa katika Miji Mikuu ya Wilaya. Iliwalazimu wananchi
kusafiri hadi Makao Makuu ya Mkoa na Wilaya kutafuta bidhaa za viwandani ambazo
pia zilipatikana katika Miji ya Dar es Salaam, Tanga, Moshi na Arusha.
Shughuli za kibiashara zilizokuwa zikifanyika vijijini ni zile za uchuuzi zilizokuwa
zinafanyika katika maeneo machache – magulio/minada – sehemu kubwa ikifanywa na
Waarabu (Guoguo).
88
Baada ya Uhuru na Azimio:
Baada ya Uhuru hali ya biashara iliendelea kumilikiwa na Wahindi na Waarabu hadi pale
lilipotangazwa Azimio la Arusha, ambalo msingi wake ni kuweka njia zote kuu za
uchumi chini ya umma.
Sehemu kubwa ya biashara iliyokuwa ikiendeshwa na Wahindi na Waarabu
ilifungwa/ilidorora kwani wengi wao walikimbia nchi. Katika kutatua hali hii Serikali
ilianzisha taasisi mbali mbali zilizopewa jukumu la kutoa huduma kwa wananchi.
Baadhi ya taasisi hizo ni kampuni ya biashara ya Mkoa RTC ambayo ilipewa jukumu la
kusambaza biadhaa toka viwandani, Shirika la Usagishaji la Taifa - NMC ambalo
lilipewa jukumu la kusambaza bidhaa za kilimo; na mashirika ya maendeleo ya Wilaya
kama DODIDECO, MPWADECO na KODECO ambayo yalishughulika na kuuza bidhaa
mbalimbali. Wananchi nao walijiunga pamoja na kufungua maduka ya ujamaa/ushirika
ambayo yalikuwa na jukumu la kununua hidhaa toka RTC/NMC na kuwauzia wananchi
katika maeneo yao.
Taasisi hizi RTC na NMC zilikuwa na matawi yao katika kila Makao Makuu ya Wilaya
na katika maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa wananchi. Katika kuhakikisha kuwa
wananchi wanapata huduma, taasisi kama CASCO, CAPSCO, Zuzu Ceramic, Nyankali
Aggregate n.k zilianzishwa katika kuendeleza ujenzi wa Makao Makuu Dodoma chini ya
CDA.
Katika miaka ya 1980/1990 nyingi ya taasisi hizi zilikufa au ziliacha kutoa huduma
pengine ni kuingia kwa sera ya biashara huria na utandawazi ambapo watu binafsi
waliingia katika kutoa huduma hizi. Sura mpya ya biashara ilionekana pale Viwanda vya
Soda – Fahari Bottlers na Magodoro – Quality Foam Mattress na kiwanda cha kusaga
nafaka – Kizota Prime Products vilipoanzishwa – hali hii ilipanua wigo wa biashara na
wananchi wengi walipata ajira na hivyo kuongeza kipato chao cha kuboreka kimaisha.
Zana hii ya soko huu iliwezesha pia kupanuka kwa shughuli za kibiashara – maduka ya
jumla mengi yalianzishwa katika maeneo mengi ya Mkoa – na vituo vingi vya
usambazaji wa bidhaa za viwandani vilianzishwa. Hali kadhalika mazao mengi ya kilimo
na mifugo yalipata maeneo au soko kwa kupitia katika minada magulio na masoko
ambayo yameanzishwa katika maeneo mengi katika Wilaya za Mkoa wa Dodoma.
89
Wananchi wengi wameanzisha makampuni ya ujenzi ambayo yanashirikiana na Serikali
katika Nyanja ya ujenzi. Pia makampuni ya usafirishaji (kwa maana ya mabasi, malori,
daladala n.k.) yameanzishwa na yanafanya biashara ya kutoa huduma kwa wananchi kwa
ujumla.
Kwa ujumla katika kipindi hiki cha miaka hamsini (50) ya Uhuru kumekuwepo na
mabadiliko ya maendeleo makubwa kwa wananchi kwa maana ya biashara na viwanda
kwa wao wenyewe kuweza kufanya biashara, kutoa ajira hivyo kupata kipato ambacho
kimewawezesha kuboresha hali zao za maisha.
3.2.12. SEKTA YA MALIASILI NA UTALII
1.0. UTANGULIZI:
Sekta ya Maliasili inajumuisha sekta ndogo 5. Sekta ya mambo ya kale imebuniwa hivi
siku za karibuni lakini sekta zilizoendelezwa katika kipindi cha miaka hamsini ya Uhuru
ni misitu, nyuki, wanyama pori na Utalii. Sekta hizo ndogo ni Misitu, Nyuki,
Wanyamapori, Mambo ya Kale na Utalii. Sekta hizi zimeendelea kuchangia pato la taifa
lakini vile vile zimesaidia katika kutunza mazingira, kuhifadhi vyanzo vya maji na ardhi,
kuzuia mmomonyoko wa udongo, ufugaji nyuki na kutoa mali ghafi katika viwanda.
♦ Misitu:
Mkoa wa Dodoma una jumla ya kilomita za mraba 41,310. Kati ya hizo km2 11,206 ni
za misitu na vichaka hii ikiwa ni sawa na asilimia 27 (27%) ya eneo lote la Mkoa. Kati
ya eneo hili la misitu Mkoa una misitu kumi na tisa (19) iliyohifadhiwa kisheria yenye
ukubwa wa kilomita za mraba 1,563. Hii ni sawa na asilimia 13.9 (13.9%) ya eneo lote
la Mkoa. Miti aina ya miombo ndiyo inayopatikana zaidi katika Mkoa wa Dodoma.
Misitu hii imeendelea kuhifadhiwa katika kipindi cha miaka hamsini hata hivyo
kumekuwepo na changamoto nyingi zilizokuwepo na zinazoendelea kuwepo kuhusiana
na misitu hii ya hifadhi changamoto hizo ni pamoja na uvamiaji wa misitu kwa ajili ya
kilimo, ufugaji, nishati ya kuni na mkaa pamoja na makazi kutokana na ongezeko la
watu.
90
Upandaji wa miti: Miti imeendelea kupandwa kila mwaka na wadau mbalimbali
wakiwemo watu binafsi, shule za msingi na sekondari, taasisi za kidini na zisizo za kidini
na mashirika mbali mbali ya serikali na yasiyo ya serikali. Kumekuwa na ongezeko la
upandaji miti kila mwaka lakini upandaji miti umefikia wastani wa miti milioni tano
(5,000,000) kwa mwaka. Upandaji huu wa miti umetokana na uoteshaji miche ambayo
takribani kila wilaya huotesha miche isiyopungua milioni moja na laki tano (1,500,000)
miche hii vile vile huoteshwa na wadau mbalimbali ambayo kwa mwaka inaweza kufikia
miche milioni 9 (9,000,000)
Serikali imeanzisha miradi mingi ya hifadhi ya mazingira hapa nchini na Mkoa wa
Dodoma umepata bahati ya kuwa na Mradi wa Hifadhi Ardhi Dodoma (HADO)
Mradi ambao ulianzishwa mwaka 1973. Mradi huu umefanya kazi katika mkoa wote wa
Dodoma takribani katika kipindi cha miaka arobaini kwa kushirikisha wananchi Mradi
umefanya juhudi kubwa katika kuongoa ardhi iliyoharibika, kuzuia mmomonyoko wa
udongo, kurudisha uoto wa asili na kuhamisha mifugo katika maeneo yaliyokuwa
yameathirika zaidi; yote hii ni mafanikio ya sekta ya misitu katika kipindi cha miaka
hamsini ya Uhuru. Pamoja na mafanikio yote haya lakini bado kuna changamoto
zinazoukabili mradi huu. Ipo kasi kubwa ya uharibifu wa mazingira unaochangiwa na
shughuli za kilimo, ufugaji na uvunaji holela wa mazao ya misitu.
Katika kipindi cha hivi karibuni takribani miaka kumi iliyopita Mkoa wa Dodoma
umekuwa mojawapo ya Mikoa iliyopata bahati ya kuwa na maeneo yanayotarajiwa
kuwepo katika orodha ya Urithi wa Dunia (World Heritage Site). Maeneo hayo ni Misitu
ya Milima ya Wotta, Mafwemela na Mang’aliza (Rubeho Block) ambayo iko katika
Wilaya ya Mpwapwa. Misitu hii iko katika Milima ya Tao la Mashariki mwa Tanzania
(Tanzania Eastern Arc Mountains) yote hii ni muendelezo wa utunzaji na uhifadhi wa
misitu tangu kupatikana kwa uhuru miaka 50 iliyopita.
Vile vile serikali imeanzisha Mradi wa usimamizi shirikishi wa Misitu (Participatory
Forest Management-PFM) unaoendelea katika Wilaya za Kondoa na Mpwapwa na sasa
Wilaya za Chamwino na Kongwa. Mradi huu ni kwa ajili ya kuwashirikisha wananchi
katika usimamizi wa misitu hii yote ni mafanikio ya uhifadhi na matumizi endelevu ya
misitu katika kipindi cha miaka hamsini iliyopita.
91
♦ Ufugaji Nyuki:
Ufugaji nyuki ni utamaduni wa wenyeji wa mkoa wa Dodoma hata kabla ya uhuru,
ufugaji huu umeendelea hata baada ya uhuru. Kumekuwa na ongezeko la wafugaji wa
nyuki kutoka 200 hadi 4000 kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita. Na vilevile ufugaji
wa nyuki umekuwa wa kisasa zaidi kwa kutumia zana za kisasa zaidi ikiwemo mizinga
ya kisasa na vifaa vya kurinia asali
Ufugaji wa nyuki katika Mkoa wa Dodoma unafanyika hasa katika Wilaya za Kondoa,
Bahi na Chamwino. Ufugaji huu hufanywa na watu binafsi (kaya) ambao ni asilimia 10 –
12 (10% - 12%) ya wakazi wote wa Mkoa wa Dodoma. Ufugaji wa nyuki hutumia
mizinga ya kienyeji ambayo huzalisha kiwango cha asali kidogo kuanzia lita 2.5 – lita 20
kwa mwaka kutegemeana na hali ya hewa katika mwaka huo. Uzalishaji bora wa asali
na nta, umeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na mafunzo ya ufugaji
bora wa nyuki yanayoendelea kutolewa kwa wananchi pamoja na vifaa vya kisasa vya
ufugaji nyuki hasa mizinga. Kumekuwa na ongezeko la asali kutoka lita 5000 kwa
mwaka hadi lita 30000 na nta kutoka tani 3 hadi tani 9 katika kipindi cha miaka kumi
iliyopita
♦ Wanyamapori:
Mkoa wa Dodoma haukujaliwa sana kuwa na wanyama pori hata hivyo Mkoa wa
Dodoma una mapori ya akiba ya wanyama (Wild life Game Reserves) mawili (2) ya
Swagaswaga na Mkungunero yaliyoko katika Wilaya ya Kondoa yenye ukubwa wa
kilomita za mraba 710.
Mapori haya ndio yanayoendelezwa hadi sasa, Vilevile Katika Wilaya ya Mpwapwa kuna
pori tengefu la wanyamapori la Rudi (Rudi Game Controlled Area) lenye ukubwa wa
kilomita za mraba 1,364.5. Kumekuwa na changamoto kwenye mapori haya hasa uvamizi
kwa ajili ya makazi, uchimbaji wa madini na shughuli nyingine za kibinadamu.
92
♦ Mambo ya Kale:
Mambo ya kale ni sekta ndogo ambayo bado ni mpya katika sekta ya Maliasili
imebuniwa hivi karibuni pamoja na kwamba inayo mambo mengi ya kihistoria na Mkoa
wa Dodoma hauko nyuma katika mambo ya kale.
Mkoa una jumba la Makumbusho ya Madini, Jumba ambalo limebeba na linatunza
hazina kubwa ya historia ya madini ya Taifa letu la Tanzania na jumba pekee la
makumbusho ya madini hapa nchini. Jumba hili lilijengwa mnamo mwaka 1925 na
kuanza kutumika mwaka 1926 kwa kuhifadhi historia ya uvumbuzi wa tafiti mbalimbali
za madini na miamba. Mkoa wa Dodoma umeingia katika historia ya Urithi wa Dunia
(World Heritage Site) kupitia michoro ya mapango ya Kondoa Irangi yaliyoko wilayani
Kondoa. Vile vile mpango unafanywa kuingiza njia ya biashara ya utumwa na meno ya
tembo katika urithi wa dunia ambapo katika Mkoa wa Dodoma njia hii inapita katika
Wilaya ya Mpwapwa, na inasemekana Dr. David Livingstone alipita njia hiyo mwaka
1873 wakati wa harakati za kukomesha biashara ya utumwa.
♦ Utalii:
Mkoa wa Dodoma hauna vivutio vingi vya utalii, lakini maeneo haya ya wanyama pori,
michoro ya mapango ya Kondoa Irangi pamoja na Chemichemi ya maji ya moto iliyoko
Kondoa Mjini na sehemu zingine mbalimbali zimeendelea kuimarishwa na kuwa vivutio
vikubwa vya Utalii Mkoani Dodoma. Vile vile jengo la Bunge limekuwa mojawapo ya
vivutio vya utalii hapa katika Mkoa wa Dodoma
3.2.13. MAMLAKA YA USTAWISHAJI MAKAO MAKUU – CDA:
UTANGULIZI:
Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu ilianzisha mwaka 1973 kwa Tamko la Serikali
Na.230 baada ya Serikali kuamua kuhamisha Makao Makuu ya Nchi kutoka
Dar es Salaam kuja Dodoma. Mamlaka hii ilipewa jukumu ya kusimamia, kuratibu, na
kutekeleza shughuli za programu ya Ustawishaji wa Mji wa Dodoma ili ufae kuwa
Makao Makuu na kuratibu zoezi zima la kuhamisha Seikali Kuu na Taasisi zake zote toka
Dar es Salaam kuja Dodoma. Baadaye Serikali ilianzisha Wizara ya Ustawishaji Makao
Makuu mwaka 1976 ili kusimamia hasa utekelezaji wa Programu ya Ustawishaji wa
Maxkao Makuu.
93
Mpango kabambe wa Mji (Dodoma Moster Plan):
Kupitia Kampuni ya Canada iitwayo “Project Planning Associates” Mamlaka ya
Ustawishaji Makao Makuu iliandaa Mpango kabambe wa Mji mwaka 1976 na kufanyiwa
mapitio mwaka 1988.
Kutokana na mbadiliko mengi yaliyojitokeza tangu mwaka 1988, CDA ililazimika
kufanya tena mapitio ya mpango kabambe wa Mji kupitia Kampuni ya “Saman
Corporation” ya Korea ikishirikiana na Kampuni ya Wazawa ya “Tanzania Human
Setttlement Solutions” mwaka 2010 ili uweze kuendana na matakwa ya kiuchumi, kisiasa
na kijamii yaliyopo sasa.
Majukumu ya Malengo ya Taasisi:
Shughuli za Mamlaka ya Ustawishaji zimeelezwa katika Kufungu Na.4 cha CDA
“Establishement Order” ya mwaka 1873. Majukumu yake ni pamoja na
• Kupanga, kupima, kugawa na kumilikisha viwanja kwa matumizi tofauti kwa
wadau mbalimbali
• Kusanifu na kujenga miundombinu hususan Barabara, na Mifereji ya maji ya
mvua
• Kupitisha na kutoa vibali vya Ujenzi
• Kusimamia na kudhibiti uendelezaji wa Mji ili uwe katika Kiwango
kinachokubalika Kimipango Miji
• Kusimamia mazingira na madhari kwa kupanda miti
• Kuratibu Programu nzima ya uhamishaji Wizara na Idara za Serikali kutoa Dar es
Salaam kuja Dodoma.
Hali ya Uongozi na Utawala:
Tangu kuanzishwa kwake. CDA imekuwa ikiongozwa na Wakurugenzi Wakuu
wanaoteuliwa na Rais kwa nyakati tofauti.
(i) Mhe. Sir Clemence G. Kahama – 1973 – 1980
(ii) Bw. Joshua D. Minja – 1980 – 1987
(iii)Bw. George M. Mlinga – 1987 – 1990
(iv)Meja Jenerali (Mst) Muhidini M. Kimario – 1991 – 1996
(v) Bw. Evarist B. Kweba – 2001 – 2004
(vi)Eng. Martin L. Kitilla – 2007 hadi sasa
94
Mafanikio yaliyopatikana:
1. Kuandaa, kupima na kugawa maeneo mbalimbali ya Makazi, Biashara, Viwanda
na Taasisi mbalimbali. Maeneo ambayo yameshapangwa/kuboreshwa na
kugawiwa kwa wendelezaji hadi sasa ni Kikuyu, Nkuhungu, Chinangali, Area
“C” na “D” (Mlimwa), Chadulu, Ipagala na Ilazo. Maeneo mengine ni
Mwangaza, Kisasa, Mapinduzi (Makulu), Chidachi, Itega, Chang’ombe, Mnadani
Kusini, Miyuji Kusini, Mailimbili, Ostabei na Medeli.
2. Mamlaka imeandaa maeneo makubwa kwa ajili kuvutia wawekezaji wa ndani na
nje ya nchi. Maeneo hayo ni kwa ajili ya magorofa ya makazi (Apartments) na
biashara, taasisi na mahoteli katika maeneo yanayozunguka Chuo Kikuu cha
Dodoma ya Njedengwa, Iyumbu na Mkalama.
3. Mamlaka imeandaa na kupima maeneo ya Miganga, Mkonze, Mkalama, Nzuguni
na Ndachi ambayo yana karibu viwanja 20,000 kwa matumizi mchanganyiko ya
Makazi, Biashara, Taasisi na Viwanda vidogo.
4. Kuweka miundombinu ya Barabara kwa Kiwango cha changarawe katika maeneo
kadhaa yaliyopimwa na kugawiwa kwa waendelezaji. Maeneo hayo ni pamoja na
Kisasa, Mwangaza, Ilazo, Kikuyu na Ipagala.
5. Mamlaka imejenga barabara Kuu za eneo la Itega kwa Kiwango cha Lami.
6. Mamlaka imepanda miti katika maeneo mbalimbali ya Mji na kandokando mwa
barabara, kutunza misitu na bustani za miti na maua zikiwemo bustani za
Mashujaa na Nyerere Square.
Changamoto:
1. Mamlaka imekuwa ikipewa fedha kidogo ambazo hazikidhi majukumu yake. Hali hii
imesababisha mamlaka kushindwa kumudu majukumu yake.
2. Baadhi ya viwanja vilivyogawiwa kwa mfumo wa Uchangiaji gharama za upimaji,
umilikishaji na uwekaji wa Miundombinu, Wananchi wa kawaida wameulalamikia
kwa kuwa gharama ya viwanja huwa ni ya juu na wananchi wengi wa kipato cha
chini kushinda kulipia.
3. Kutokana na kutopimwa kwa viwanja vya kutosha, wimbi kubwa la Ujenzi holela
limejitokeza. Hali hii imesababishwa na ongezeko la idadi kubwa ya watu ambao
haliendani na idadi ya viwanja vinavyotolewa.
95
4. Serikali kushindwa kufidia maeneo ya upanuzi wa Mji kulingana na matakwa ya
Sheria za Ardhi na 4 na Na. 5 kumefanya zoezi la upangaji, upimaji, ugawaji na
ujenzi wa Miundombinu kwa maeneo ya upanuzi wa Mji kuwa ya gharama kubwa.
5. Mamlaka ya Vijiji ya kugawa na kusimamia Ardhi vilivyopewa na Serikali kumeleta
migogoro/migongano mingi na hivyo kuathiri utekelezaji wa majukumu ya CDA.
Matarajio ya Taasisi katika Miaka 50 ijayo:
Malengo ya ujumla ya Mamlaka ni kutayarisha Mkakati wa Kuharakisha Ustawishaji
Makao Makuu Dodoma unatekelezwa kwa vitendo kwa kutumia rasilimali za ndani
(maduhuli) na kutoka bajeti ya Serikali Kuu. Pia kuhakikisha kuwa azma ya Serikali
kuhusu Programu ya uhamishaji Wizara na Idara za Serikali kutoka Dar es Salaam kuja
Dodoma inatekelezwa katika kipindi cha miaka ishirini ijayo yaani mwaka 2012/2013
hadi 2031/2032.
Mwelekeo huu unahitaji Baraka, Nia na Mwowngozo kutoka Serikali Kuu kwa maeneo
ya Kimuundo, Kisera na Kisheria. Kutokana na matumizi ya ardhi yaliyopangwa katika
Mpango Kabambe wa mwaka 1976 na ule wa mapitio wa mwaka 1988 kuonekana
kutokidhi mahitaji makubwa ya ardhi yanayotokana na ongezeko kubwa la watu,
Mamlaka ipo katika hatua za mwisho za kutayarisha Mpango Kabambe mpya wa
kuuongoza Mji na ujenzi wa huduma za Jamii kwa miaka ishirini ijayo yaani 2011 hadi
2031.
3.2.14. VYUO VYA ELIMU YA JUU
1.0. CHUO CHA MIPANGO NA MAENDELEO VIJIJINI – IRDP
Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Dodoma kilianzishwa rasmi kama
taasisi chini ya sheria ya Bunge Na. 8 ya mwaka 1980. Sheria hiyo ilianzisha
chuo kikiwa ni kituo muhimu cha taifa cha kutoa mafunzo, kufanya utafiti, na
kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu katika mipango ya maendeleo vijijini.
Sheria hii ilianza kufanya kazi rasmi tarehe 1 Februari, 1979.
Chuo baada ya kuanzishwa kwake makao yake ya kwanza yalikuwa katika eneo
la Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Kitivo cha Morogoro (sasa – SUA). Mkuu wa
chuo akiwa Askofu Eliah Simon Chiwanga. Mwaka 1980 Chuo kilihamishiwa
96
Dodoma mjini katika majengo ya CCT-CTC, Jengo la kukodi la chimwaga na
shule ya msingi ya Mtekelezo (sasa - Central Secondary School). Katika mwaka
1984, aliyekuwa Mkuu wa Chuo Askofu Eliah Simon Chiwanga aliamua kujiunga
na kazi za kichungaji katika kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Mpwapwa.
Kutokana na hilo, Ndugu Constantine Mashenene Kazi aliteuliwa kuwa Mkuu
mpya wa chuo.
Mwaka 1985 Chuo kilihamishia ofisi zake kwenye majengo ambayo yalikuwa
yamejengwa kwa ajili ya ‘Vocational Training Centre” eneo la Area C (Sasa -
Kiwanja cha Ndege Shule ya Sekondari). Mwaka 1996 Ndugu Heslon K.L.
Mahimbo aliteuliwa kukaimu nafasi ya Mkuu wa Chuo baada ya Ndugu
Constantine Mashenene Kazi kuteuliwa kushika wadhifa wa Mkurugenzi wa
Idara ya Masuala ya Bunge na siasa katika ofisi ya Waziri Mkuu.
Chuo kilihamisha Makao yake kutoka Area C na kuhamia eneo la Mbwanga
kilipo sasa mwaka 1995. Mwaka 2003 Ndugu Constantine Silvinus Lifuliro
aliteuliwa kukaimu nafasi ya Mkuu wa Chuo na mwaka 2006 alithibitishwa rasmi
na serikali kuwa Mkuu wa Chuo.
Mafanikio yaliyo patikana hadi sasa
(i) Kuongezeka kwa idadi ya programu za mafunzo ya muda mrefu Kutoka
programu 2 mpaka 8 ( Stashahada za uzamili na cheti) ambazo ni:
• Cheti cha Mipango ya Maendeleo Vijijini.
• Stashahada katika Mipango ya Maendeleo.
• Shahada ya Kwanza katika Mipango ya Maendeleo ya Mikoa.
• Shahada ya Kwanza katika Mipango na Usimamizi wa Mazingira,
• Shahada ya Kwanza katika Mafunzo ya Idadi ya Watu na Mipango ya
Maendeleo.
• Shahada ya Kwanza katika Mafunzo na Fedha za Maendeleo na
Mipango ya Uwekezaji.
• Stashahada ya Uzamili katika Mipango ya Mikoa, na
• Stashahada ya Uzamili katika Mipango ya Mazingira.
97
Taaluma ya Mipango ya Maendeleo, Usimamizi wa Mazingira na masuala
ya Idadi ya Watu; Shahada ya mafunzo ya Fedha za Maendeleo na
Mipango ya Uwekezaji (Bachelor Degree in Development Finance and
Investment Planning) si tu ni muhimu kwa maendeleo endelevu bali pia
itatoa Wataalam wanaosaidia kwa kiasi kikubwa Serikali zetu za mitaa
ambako kwa sasa serikali inapelekea kiasi kikubwa sana cha fedha kwa
ajili ya shughuli za maendeleo.
(ii) Kuhusu eneo la Ushauri na Uelekezi, Chuo kimeendelea kufanya shughuli
za Ushauri na Uelekezi kwa wadau mbalimbali wa maendeleo,hususan,
Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na
watu binafsi. Pia tafiti kadhaa zenye lengo la kutatua matatizo yanayo
ikabili jamii zimefanyika na nyingine zinaendelea kufanywa.
(iii) Kuongezeka kwa ubora wa mafunzo yanayotolewa na chuo chetu;
Mafunzo yote yanayotolewa hapa chuoni hufuata mitaala inayolenga
umahili wa utendaji kazi katika fani husika (Competance Based Education
System) ambayo kwa kiwango kikubwa huzingatia mafunzo kwa vitendo
na ushirikishaji wa wanafunzi wakati wa kutoa mafunzo ya ndani na nje
ya darasa ili waweze kuelewa na kumudu zaidi mafunzo na kazi baada ya
kuhitimu mafunzo yao hapa chuoni. Mafunzo ya muda mfupi kwa wadau
yameongeza ujuzi na ufahamu kwa Viongozi na Maafisa Watendaji hali
ambayo inawezesha kuboresha utendaji wa kazi na utoaji wa huduma kwa
jamii katika maeneo yao ya kazi.
(iv) Kuongezeka kwa idadi ya wanachuo wanaojiunga na kuhitimu mafunzo
mbalimbali. Chuo kilipoanzishwa Mwaka 1979 kilikuwa na wanafunzi 22
wanaume 21 mwanawake 1 hivi sasa chuo kina wanafuzi 2844 wanaume
1687 wanawake 1157 Wahitimu katika chuo chetu kufikisha utaalam wa
Mipango ya Maendeleo Vijijini kwa kutoa wataalam mahiri wa ngazi
mbalimbali ambao wana uwezo wa kitaaluma wa kukabiliana na
changamoto zinazotokana na mabadiliko ya kiushindani katika dunia hii
ya utandawazi. Taaluma ya Mipango ya Maendeleo, Usimamizi wa
Mazingira na masuala ya Idadi ya Watu inayofundishwa na Chuo hiki kwa
98
watumishi wa Serikali na taasisi mbalimbali zenye dhamana ya shughuli
za maendeleo, imesaidia sana katika kuboresha uandaaji, utekelezaji na
usimamizi wa mipango ya maendeleo nchini na hivyo kusukuma mbele
maendeleo ya Taifa letu.
(v) Kukamilika kwa ujenzi wa majengo mbalimbali ikiwemo bweni la
Sumaye, maktaba, uzio kuzunguka Chuo; jengo la kwanza la taaluma,
jengo la ukumbi wa mikutano, na jengo la pili la taaluma lenye ghorofa
nane ambalo ujenzi wake unatarahiwa kubamilika mwezi septemba 2011.
Jengo hili la ghorofa nane litakuwa na Kumbi za mihadhara nne (4)
Vyumba vya madarasa nane (8) Chumba cha kompyuta kimoja (1) Ofisi
za Wahadhiri hamsini (50) Maktaba ndogo mbili (2) Vyumba vya mi
kutano vitatu (3).
(vi) Chuo kikisaidiwa na serikali kimejenga uwezo wa kufanya zaki zake kwa
weledi na ufanisi mkubwa kwa kuajiri wahadhiri na watumishi
waendeshaji na kuwaendeleza kiutendaji ili kukidhi mahitaji ya sasa na
yale yanayotarajiwa. Hadi sasa, Chuo kina jumla ya wahadhiri wapatao
88, ambao kati yao wahadhiri 9 wana shahada za Udaktari wa Falsafa na
wahadhiri 62 wana shahada za Uzamili. Wahadhiri 17 wana Shahada za
Kwanza na Stashahada za Uzamili. Hivi sasa, jumla ya wahadhiri 17
wanasomea shahada ya Udaktari wa Falsafa (uzamivu), 1 anasomea
shahada ya uzamili. Kwa upande wa wafanyakazi waendeshaji, jumla ya
wafanyakazi kumi (6) wanasomea kozi mbalimbaili. Kati yao (2)
wanasomea shahada za uzamili, (3) stashahada na wafanyakazi (1)
astashahada. Wahadhiri na wafanyakazi waendeshaji hawa wako katika
vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
(vii) Chuo kimeendelea kuendesha mafunzo ya muda mfupi, tafiti na kutoa
ushauri wa kitaalam kwa serikali na asasi mbalimbali zenye dhamana ya
maendeleo nchini. Shughuli hizi ni muhimu kwa sababu zimesaidia
kusambaza utaalam unaohitajika katika utekelezaji wa shughuli za
maendeleo nchini.
99
(viii) Kwa Msaada serikali ya Uholanzi kupitia Shirika la NUFFIC la na mradi
wa NICHE chuo kimeimarisha kitengo cha Rural Information Centre
(RIC) kuwa kituo na chanzo muhimu cha upatikanaji wa takwimu za
mipango ya maendeleo, hususani maendeleo vijijini.
(ix) Chuo pia kimeanzisha kijiji cha mfano (IRDP ‘model village’ –
Mpunguzi). Ambapo mafunzo mbalimbali yatolewayo na chuo
yanatarajiwa kufanyika kwa vitendo
(x) Chuo kimo katika haratati za kuanzisha kituo cha mafunzo katika kanda
ya ziwa mjini Mwanza. Kituo hiki kitaanza kutoa mafunzo mwaka wa
fedha wa 2011/2012
Changamoto zilizo jitokeza
Pamoja na mafanikio yaliyotajwa hapo juu chuo kinakabiliwa na changamoto
kubwa zifuatazo:
(i) Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu kukinzana na mitaala ya
vyuo vyenye mafunzo kwa vitendo kama chetu. Wakati mitaala hiyo
husika inaonyesha muda maalumu wa mafunzo kwa vitendo, Bodi hutoa
fedha kwa siku pungufu tofauti na siku zilizopendekezwa.
(ii) Kufuatana na Waraka wa Maendeleo ya Watumishi na.1 wa mwaka 2002
ambao ulielekeza kwamba muundo wa utumishi kwa Maafisa Mipango
ubadilishwe na kuwa muundo wa watumishi wa uchumi, hatua hii
imesababisha tuzo zinazotolewa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo
Vijijini kutojumuishwa katika kundi hilo la kada ya uchumi, na hivyo
kuleta wasiwasi kwa wahitimu wa Chuo Cha Mipango ya Maendeleo
Vijijini - Dodoma.
(iii) Kufuatia kuboresha kwa mitaala yetu, sasa chuo kinakabiliwa na ongezeko
kubwa la wahitaji wa mafunzo yanayotolewa hapa chuoni, ongezeko
ambalo hatuna uwezo nalo kutokana na ufinyu wa miundo mbinu.
(iv) Kupitia upya sheria ya uanzishwaji wa chuo ili kuendana na mabadiliko ya
kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni yalivyo sasa.
(v) Ushindani kutoka kwa vyuo au taasisi zinazotoa mafunzo ya kama yetu.
100
2.0. CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA KAMPASI YA DODOMA - CBE
Kampasi ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dodoma ni tawi la Chuo cha Elimu ya Biashara
Makao Makuu Dar es Salaam ambacho kilianzishwa mwaka 1965.
Wazo la kuanzishwa Chuo cha elimu ya Biashara lilitokanana mapendekezo ya Kamati
ya Menejimenti ya utafiti wa Mafunzo ambayo iliundwa na Serikali mwaka 1974 ili
kuipa serikali mwelekeo wa Mafunzo Kitaifa. Kamati ilipendekeza kwamba Chuo cha
Elimu ya Biashara kjenge Kampasi mbili nje ya Dar es Salaam katika Miji ya Dodoma na
Mbeya. Badala yake uamuzi ulifikiwa wa kushirikiana na Mpango wa Serikali wa
kujenga Makao Makuu Dodoma.
Kwa hiyo iliamliwa Kampasi ya Chuo cha Elimu ya Biashasra ijengwe Dodoma. Ujenzi
wa Chuo ulianza Juni 1980 kwa msaada wa Serikali ya Ujerumani kwa lengo la
kuchukua wanachuo 240. Chuo kilifunguliwa rasmi na Rais wa awamu ya kwanza wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mwalimu julius Kambarage Nyerere Oktoba
9, 1983 wakati wa sherehe za miaka kumi (10) ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma.
Chuo kilianza na wanachuo 80. Kampasi ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dodoma
inaongozwa na Makamu mkuu wa Chuo ambaye anawajibika kwa Mkuu wa Chuo cha
Elimu ya Biashara Makao Makuu Dar es Salaam.
Majukumu, Malengo na Mafanikio ya Chuo:
(i) Majukumu:
Majukumu ya Chuo tangu kuanzishwa kwake ni:
• Kutoa mafunzo ya Biashara na uendeshaji wa viwanda (Commercial and
Industrial Development/Management) katika nyanja (flelds of) za Uongozi wa
Biashara, Uhasibu, Masoko, Ununuzi na Ugavi na Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano
• Kufanya Utafiti na Ushauri mbalimbali katika tasnia ya Biashasra na
Ujasiriamali kwa Taasisi na wadau mbalimbali.
• Kuendesha mafunzo ya muda mfupi ya Biashara, Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano nk.
101
(ii) Malengo:
Kwa muda mrefu Chuo kimekuwa kinatoa mafunzo ya Cheti, Diploma na
Advance Diploma katika Nyanja zilizotajwa hapo juu. Lengo kubwa ni
kuwezesha kupatikana kwa wataalamu wa kutosha katika Nyanja zote zilizotajwa
hapo juu ili kutosheleza Soko la Ajira.
(iii) Mafanikio ya Chuo:
Yafuatayo ni mafanikio ya Chuo katika miaka nane (8) iliyopita:
• Idadi ya wanachuo imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka kutokana
na mwamko wa wazazi wa kusomesha watoto wao na pia kuanzishwa kwa
Bodi ya Mikopo. Takwimu zifuatazo zinathibitisha:
Jedwali Na. 29 Idadi ya Wanachuo 2002 hadi 2010 (CBE)
Mwaka wanaume Wanawake Jumla
2002/2003 247 138 385
2003/2004 272 172 444
2004/2005 335 205 540
2005/2006 684 362 1,046
2006/2007 1,054 595 1,649
2007/2008 1,479 971 2,450
2008/2009 1,102 767 1,869
2009/2010 1,569 1,056 2,325
• Chuo kinaendeshwa masomo ya asubuhi na jioni na kinatoa Mafunzo na
Ngazi za. Cheti (Certificate), Stashahada (Diploma) na Shahada (Degree)
katika fani za.
- Uongozi wa Biashara
- Uhasibu
- Menejimenti ya Masoko
- Menejimenti ya Ununuzi na Ugavi na
- Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Cheti za Stashahada tu)
102
• Kuanzia mwaka wa Masomo wa 2008/2009 Chuo kilianza kutoa Mafunzo
ya Shahada (Degree) katika fani ya Uhasibu. Katika mwaka wa masomo
wa 2009/2010 Chuo kilitoa Mafunzo ya Shahada katika fani za Uhasibu,
Uongozi wa Biashasra, Masoko na Ununuzi na Ugavi. Hii ina maana sasa
Mafunzo yatatolewa katika ngazi ya Cheti, Stashahada, Shahada na
Diploma ya Uzamili. Hapatakuwepo tena Stashahada za juu.
• Mfumo wa ufundishaji Masomo ambao Chuo kinautumia ni ule wa
Umilisi (Competence Based Learning) badala ya Mafunzo Nadharia
(Theoretical/Knowledge Based Learning). Mfumo huu wa ufundishaji
humpa mwanafunzi weledi mzuri wa yale anayofundishwa.
Imeelezwa hapo juu kwamba Chuo kimenza kutoa Mafunzo ya Shahada. Hii
haimaanishi kwamba sasa Chuo kimebadilika kuwa Chuo Kikuu. Kinaendelea
kuwa Chuo cha Elimu ya Juu (siyo Chuo kikuu) na kitaendelea kutoa Mafunzo ya
Umilisi.
Mahafali ya Chuo:
Mahafali (Graduation Ceremony) yalianza kutolewa hapa kwenye Kampasi
kuanzia mwaka 2008. Idadi ya Wahitimu ni kama ifuatayo:
Jedwali Na.30 Idadi ya Wahitimu 2008 hadi 2010 (CBE)
Mwaka Wahitimu
Cheti Stashahada Stashahada ya Juu Jumla
2008 106 325 332 763
2009 322 466 261 1,049
2010 585 380 261 1,226
Mafunzo ya Ujasiriamali:
Katika kuiunga mkono Serikali katika azima yake ya kupambana na umaskini,
Chuo kimeanzisha Mtaala wa Somo la ujasiriamali katika Kozi zote
zinazoendeshwa na Chuo. Hatua hii imechukuliwa ili kuwawezesha wahitimu wa
Kozi zote kuelewa dhana ya Ujasiriamali na kuwa tayari kwenda kujiajiri pindi
wamalizapo masomo na kuyatumia maarifa waliyoyapata katika kuboresha
shughuli zao badala ya kusubiri ajira katika Sekta rasmi.
103
Aidha Chuo kimeanzisha Kitengo cha Ujasiriamali ambacho kinatoa Mafunzo ya
muda mfupi na muda mrefu katika tasnia ya Ujasiriamali. Tunaamini hatua hii ni
mwelekeo stahiki wa kutekeleza azma ya MKUKUTA.
Changamoto:
• Uhaba wa Madarasa kuna uhaba mkubwa wa madarasa. Hali hii
imetokana na ongezeko la Wanachuo mwaka hadi mwaka kama
ilivyoelezwa hapo juu.
• Idadi kubwa ya Wanachuo ambao wanahitaji huduma ya malazi
imesababisha uhaba mkubwa wa hosteli kwa ajili ya malazi. Hosteli kumi
za Chuo zimeshindwa kukidhi mahitaji yamalazi na hivyo kulazimisha
Chuo kukodi nyumba za watu binafsi
• Idadi ya Wanachuo hailingani na ukubwa wa Maktaba iliyopo. Maktaba ni
ndogo kuliko idadi ya Wanachuo.
• Gharama za Ukarabati na Ukarafati wa Majengo ya chuo ambayo
yalijengwa miaka ya 1980 yamechakaa yanahitaji ukarabati. Gharama za
kufanya hivyo ni kubwa mno kulinganisha na mapato ya Kampasi. Aidha,
ukarabati mdogo mdogo ni aghali pia kutokana na vifaa visivyo na ubora
ambavyo viko madukani ambavyo hununuliwa na kutumika katika
ukarabati havidumu muda mrefu.
• Idadi ndogo ya Watumishi kwa mujibu wa Ikama ya Kampasi inatakiwa
kuajiri wafanyakazi wengi (Walimu na wasio Walimu) ili kukidhi mahitaji
ya uendeshaji wa majukumu ya Kampasi. Ajira inakuwa ngumu kwa kuwa
ni lazima kibali kipatikane kutoka Serikalini (Utumishi/Hazina). Hali hii
huathiri kwa kiasi kikubwa ufanisi wa majukumu na husababisha ajira za
Wakufunzi wa muda (Part-time Lectures).
104
3.0. CHUO KIKUU CHA DODOMA:
Historia fupi ya Chuo Kikuu cha Dodoma:
Chuo Kikuu cha Dodoma kilianzishwa rasmi tarehe 16 Februari 2007 siku ambayo Mhe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipowateua viongozi wakuu wa Chuo yaani
Mkuu wa Chuo, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Makamu Mkuu wa Chuo na Manaibu
wake wawili. Wazo la kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dodoma linatokana na ahadi
aliyoitoa mgombea wa Urais kupitia CCM Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika
mchakato wa Urais. Katika moja ya mikutano yake ya Kampeni alisema akichaguliwa
atajenga Chuo Kikuu chenye uwezo wa kudahili wanafunzi elfu arobaini.
Mchakato wa kuanzishwa Chuo Kikuu cha Dodoma ulianza rasmi mwaka 2006 ambapo
Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kuingia madarakani akaiagiza Wizara ya
Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia ya wakati huo kuanza utekelezaji wake. Wizara ya
Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia ikaunda kikosi kazi ambacho kilifanya upembuzi
yakinifu na kupendekeza kwa Serikali mahali pa kuanzishwa chuo hicho, jina la chuo na
miundombinu ya kuanzia shughuli zake.
Katika mchakato huo iliamriwa kuwa chuo kijengwe Dodoma, kiitwe Chuo Kikuu cha
Dodoma na Serikali ikatoa jengo Chimwaga, majengo yaJeshi ya Mkalama pamoja na
nyumba 155 zilizoko eneo la Kisasa kama miundombinu ya kuanzishia shughuli za Chuo.
Chuo Kikuu cha Dodoma kiliwapokea rasmi wanafunzi wanzilishi tarehe 10 Septemba
2007 na huo ndiyo ukawa mwanzo wa utimilifu wa ahadi aliyoitoa Mhe. Jakaya Mrisho
Kikwete ambaye katika historia ya Chuo tunamuita Muasisi wa Chuo Kikuu cha
Dodoma.
Muundo wa Chuo Kikuu cha Dodoma:
Chuo Kikuu cha Dodoma kinaundwa na Vyuo vya Kampasi sita ambavyo ni Sanaa
naSayansi za Jamii, Elimu, Afya, Sayansi Asilia na Hisabati, Sayansi za Ardhi na Sayansi
za Kompyuta, Habari na Mawasiliano. Vyuo vya Kampasi vinaundwa na Skuli pamoja na
idara za fani mbalimbali.
Majukumu ya Chuo na malengo yake:
Malengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma ni kuwa Chuo kikubwa katika Afrika Mashariki na
Kati chenye uwezo wa kudahili zaidi ya wanafunzi elfu arobaini na pia kitovu cha
teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika ukanda huo. Kama ilivyo katika Vyuo Vikuu
105
vingine majukumu ya Chuo Kikuu cha Dodoma ni kutoa mafunzo, kufanya utafiti na
kutoa huduma kwa jamii.
Sera na Sheria:
Chuo Kikuu cha Dodoma kimeanzishwa kutokana na Sera ya Elimu ya Juu ya mwaka
1999, Sheria mama ya Vyuo Vikuu na 7 ya mwaka 2005 pamoja na Hati Idhini ya Chuo
Kikuu cha Dodoma ya mwaka 2007. Katika utekelezaji wa shughuli za kila siku za
uendeshaji wa Chuo, sera na miongozo mbalimbali imeandaliwa ikiwemo sera ya utafiti,
sera ya ubora wa huduma, sera ya kutoa huduma kwa jamii, sera ya makazi, sera ya uajiri
na upandaji vyeo, sera ya maadili na nidhamu n.k.
Mabadiliko katika mfumo wa kiutawala:
Kama ilivyoelezwa hapo awali Chuo Kikuu cha Dodoma kinaundwa na vyuo sita vya
kampasi. Kutokana na uchanga wake, maamuzi mengi ya kiuendeshaji yalifanywa na
uongozi wa juu wa chuo. Hata hivyo kutokana na kasi ya kukua nakupanuka kwa chuo,
uongozi wa juu umekasimu madaraka kwa wakuu wa vyuo kwazile shughuli za kila siku
za uendeshaji kuanzia tarehe 1 Machi, 2011.
Maamuzi mtambuka kama vile taaluma, sera na miongozo mbalimbali, bajeti ya chuo,
ujenzi wa miundombinu, ajira, vitafanywa na uongozi wa juu na vyombo husika kama
vile Seneti, kamati ya Ajira, Kamati ya Miliki, Kamati ya Mipango na Fedha pamoja na
Baraza la Chuo.
Mafanikio yaliyopatikana:
Katika uhai wa miaka minne tangu kuanzishwa kwake, Chuo kimepata mafanikio
makubwa ya kujivunia. Pamoja na mambo mengine Chuo kimefanikiwa kufanya
yafuatayo:
(i) Kujenga miundombinu ya vyuo vinne yenye uwezo wa kutumiwa na
wanachuo elfu thelathini na sita.
(ii) Kimedahili wanafunzi 20,000 na hivyo kuwa Chuo kikubwa kuliko vyote
hapa nchini kwa vyuo vyenye mfumo wa bweni.
(iii) Kimeweza kutoa wahitimu wa kwanza 1,276
(iv) Kimetimiza masharti na kupata usajili kamili
106
Changamoto:
Chuo kimekabiliwa na changamoto nyingitangu kuanzishwa kwake. Zipo changamoto
zinazotokana na uchanga wake kama vile uhaba wa miundombinu, uhaba wa vifaa n.k.
lakini pia zipo changamoto zinazotokana na kasi ya ukuaji wa chuo kama vile uhaba wa
makazi ya wafanyakazi, raslimaliwatu, maji ya kukidhi mahitaji, miundombinu ya
majitaka. Changamoto kubwa inayokuzwa na uchanga wa chuo ni ufinyu wa bajeti na
vyanzo vichache vya mapato ya chuo.
Matarajio:
Chuo kina matarajio makubwa kama vile
• Kuwa chuo kikubwa Afrika Mashariki na Kati chenye uwezo wa kudahili
zaidi ya Wanachuo 40,000
• Kuwa kitivo cha teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa nchini na Afrika
Mashariki na Kati
• Kuchagiza kustawi na kukuwa kwa maendeleo ya jamii katika kanda ya kati
hususani Mji wa Dodoma.
3.2.15. SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI TUCTA:
Harakati za vyama vya Wafanyakazi Mkoani Dodoma zimekuwepo kabla ya mwaka
1960 katika kipindi cha miaka Hamsini ya Uhuru wa nchi yetu, mchango wa vyama vya
Wafanyakazi na Wafanyakazi wenyewe ni mkubwa:
(i) Wafanyakazi walisaidia sana chama cha TANU katika Harakati za kudai Uhuru
wa nchi yetu ambapo kupita mikutano ya wafanyakazi, kadi za uanachama wa
TANU zilisambazwa.
(ii) Hata baada ya kupata Uhuru, wafanyakazi walishiriki kikamilifu katika
kuchangia mapambano ya ukombozi wa Nchi za Afrika ambazo hazikuwa
Huru.
(iii) Wafanyakazi walichangia katika shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo
Ujenzi wa Ofisi za CCM Makao Makuu, Jengo la Chimwaga, Uwanja wa
Jamhuri na Minara ya kumbukumbu - Mnara wa UHURU, Mnara wa
INDEPENDENCE SQUARE na Mnara wa Mashujaa. Wafanyakazi waliweza
kuchangia pia katika ujenzi wa shule, vituo vya Afya na Zahanati na
wanaendelea hadi sasa.
107
Haya yote yametekelezwa katika kipindi chote tangu tulipo;ata Uhuru wetu. Baada ya
mwaka 1996, vyama vingi huru vya wafanyakazi vilianzishwa. Hapa Dodoma vyama
vinane vilianzishwa na Idadi hiyo imekuwa ikiongezeka. Vyama hivyo ni TUGHE,
TUICO, CHODAWU, TALGWU, RAAWU, CWT, TAMICO COTWU (T),
TEWUTA, TUPSE na TASIWU.
Vyama vyote hivi vinaendelea kufanya kazi zao chini ya Shirikisho la Wafanyakazi
Tanzania TUCTA. Pia vyama hivi vinashirikiana na vyama ambavyo siyo wanachama
wa Shirikisho la TUCTA.
3.2.16. SHIRIKA LA UTANGAZAJI TANZANIA TBC KANDA YA KATI DODOMA
TBC Kanda ya Kati inajumuisha Mikoa ya Dodoma na Singida. Katika Mikoa yote
miwili kwa sasa kuna vituo vya kurushia matangazo ya Redio na Televisheni. Matangazo
ya Redio Dodoma ndiyo matangazo ya siku nyingi tangu mwaka 1988 kutokea katika
kituo cha kurushia matangazo kilichoko katika Kijiji cha Mundemu Wilaya ya Bahi kwa
kutumia mtambo wa masafa ya kati Medium Wave mita bendi 497, 603 KHz pamoja na
mtambo mdogo wa kurushia matangazo uliopo Studio ya Mjini Dodoma.
Matangazo ya Redio katika mawimbi ya FM; 87.7 MHz TBC Taifa na 90.4 MHz TBC
FM pamoja na matangazo ya Televisheni Chaneli 8, 207 MHz ni hatua ya maendeleo
iliyofikiwa mwaka 2004 kwa Televisheni na 2007 kwa Redio za FM kituo cha Image
kilichopo Dodoma Mjini. Kwa kituo kipya kabisa cha kisasa cha Singida kilichopo eneo
la Mikumbi katika Manispaa ya Singida, matangazo ya Televisheni Chaneli 7, 191.25
MHz, na Redio TBC Taifa 96.6 na TBC FM 94.6 MHz Mkoani Singida yalianza
mwishoni mwa mwaka wa fedha wa 2009/2010.
Kanda ya Kati kiutendaji inao watayarishaji wa vipindi, waandishi wa habari, mafundi na
watendaji wa vitengo vingine vya Utawala.
Kabla ya kuanza kwa matangazo ya Redio na Televisheni mikoa ya Singida na Dodoma
kama ilivyokuwa mikoa mingi ya Tanzania Bara kwa sehemu kubwa ya utawala baada ya
uhuru wakati wa awamu ya kwanza ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere ilikuwa
inahudumiwa na waandishi wa habari waliokuwa wakiandika habari na kutuma Makao
Makuu wakati huo ya Radio Tanzania ambako zilikuwa zikitangazwa kutokea Dar es
salaam. Kwa upande wa vipindi vya Redio watayarishaji wa vipindi walikuwa wakisafiri
108
kutoka Dar es salaam kuja Mikoani kukusanya taarifa mbalimbali na kurudi nazo Makao
Makuu kwa ajili ya kuzitangaza katika vipindi mbalimbali.
Mabadiliko yaliyotokea baadaye kwa kufungwa mitambo ya kurushia matangazo pamoja
na Studio ya Redio yaliwezesha kuongezwa kwa wafanyakazi wa kutayarisha na
kuvitangaza vipindi vinavyotayarishwa Dodoma.
Hivi sasa vipindi vya mikoa ya Singida na Dodoma vinaweza kutayarishwa na
kutangazwa kutokea Dodoma. Kwa upande wa Studio ya Radio Kanda ya Kati Dodoma
muda maalum umetengwa wa kuanzia saa 5.00 asubuhi hadi saa 7.00 mchana kurusha
vipindi vilivyotayarishwa Dodoma vyenye kuonyesha sura ya Kanda ya Kati iwe katika
kupasha habari, kuelimisha au kuburudisha.
Aidha kupitia studio ya Radio Dodoma, TBC Taifa inaweza kujiunga moja kwa moja na
studio hiyo kwa vipindi vinavyotoka Dodoma. Mfano wa vipindi hivyo ni Leo Katika
Bunge, Ugua Pole na vipindi vingine maalum. Kwa upande wa matukio ya kila siku ya
habari mikoa yote miwili Singida na Dodoma imeongezewa nguvu kwa kuletwa
waandishi wa habari wenye vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi ambavyo vina uwezo wa
kutuma habari muda mfupi tu baada ya tukio kutokea. Kuwepo kwa waandishi
waliopatiwa mafunzo na vifaa vyenye kutumia teknolojia ya kisasa kumeifanya TBC siyo
tu kwa Kanda ya Kati lakini kwa maeneo yote nchini kuwa ni chombo cha utangazaji
chenye kutumainiwa na watazamaji wa televisheni na wasikilizaji wa Redio za TBC.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, makao yake ni Dodoma hiyo nayo ni
changamoto nyingine kwa TBC kwamba mkutano wa Bunge umekuwa ni moja ya
matukio yake muhimu katika shughuli za uandishi wa habari na utangazaji. Matangazo
ya kutoka Bungeni kupitia Televisheni hivi sasa yote yanarushwa moja kwa moja wakati
Bunge linapoendelea na mikutano yake na upande wa Redio sehemu kubwa ya
matangazo yake pia yanarusha moja kwa moja vipindi vya Bunge na kuvirudia vipindi
vya majadiliano usiku.
TBC Kanda ya Kati ni moja ya matawi ya TBC Makao Makuu. Kwa maana hiyo kazi
zote zinazofanywa na watendaji wa TBC walioko Dodoma na Singida ni utekelezaji
wa malengo na shabaha nzima ya TBC kwa nchi nzima.
109
HISTORIA YA TBC
Shirika la Utangazaji Tanzania (The Tanzania Broadcasting Corporation-TBC) ni
chombo cha umma kilichoundwa chini ya sheria ya Mashirika ya Umma ya mwaka 1992,
sura ya 257 (The Public Corporations Act, Cap. 257 R.E 2002) sheria ya Utangazaji ya
mwaka 1993, Sura ya 306 (Broadcasting Services Act, Cap. 306. R.E. 2002).
TBC imeundwa kuwa chombo cha Utangazaji cha Umma (Public Service Broadcaster-
PSB) kama ilivyo kwa vyombo vingine vya Utangazaji vya Umma. Kwa mujibu wa
sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano ya mwaka 2003 (The Tanzania Communication
Regulatory Authority Act, No. 12 , 2003) TBC ina mamlaka ya kutoa huduma za
utangazaji wa aina zifuatazo:-
1. Utangazaji kwa umma (Public Broadcasting);
2. Utangazaji wa Biashara (Commercial Broadcasting);
3. Utangazaji wa Kijamii (Community Broadcasting);
4. Huduma nyingine ya utangazaji kama Waziri wa Habari atakavyoamua {kifungu 32
(2)}
Utangazaji katika Tanzania Bara ulianza mwaka 1951 kwa majaribio mjini Dar es salaam
kwa chombo kilichoitwa “Sauti ya Dar es salaam”. Chombo hiki kilikuwa chini ya Idara
ya Huduma za Jamii. Mwaka 1955 chombo hiki kilibadilishwa jina na kuitwa “Sauti ya
Tanzania” (Tanganyika Broadcasting Services) kikitumia mitambo yenye nguvu ya
“Short Wave” iliyoweza kusikika karibu nchi nzima, kabla ya Julai 1, 1956 kubadilishwa
na kuitwa Tanganyika Broadcasting Corporation-TBC kwa mujibu wa sheria ya
Tanganyika Broadcasting Ordinance sura ya 370 (wakati huo).
RADIO TANZANIA DAR ES SALAAM
Mnamo mwaka 1965, serikali iliamua kuchukua uendeshaji wa chombo hiki na kukifanya
Idara katika Wizara ya habari na Utalii. Chombo hiki kilibadilishwa jina na kuitwa Radio
Tanzania Dar es salaam RTD kwa mujibu wa sheria namba 11 ya mwaka 1965.
Majukumu ya chombo hiki yalikuwa yakibadilika kila hatua ya mabadiliko
110
ilivyojitokeza. Tangu ukoloni hadi uhuru. Kilikuwa ni chombo cha utekelezaji wa sera,
siasa na taratibu za serikali iliyopo madarakani. Kutoka wakati huo mpaka mwaka 1993,
vyombo vya Utangazaji vilikuwa ama vinamilikiwa au kudhibitiwa na serikali.Kipindi
cha baada ya uhuru itakumbukwa kuwa serikali ilirithi mifumo mingi ya kikoloni na
ilikuwa na kazi kubwa ya kujenga utaifa, uzalendo, umoja na mshikamano wa
Watanzania. Vyombo vya utangazaji na hasa Redio ya serikali iliifanya kazi hiyo kwa
ufanisi mkubwa.
Mwishoni mwa miaka ya 1980, kulitokea mabadiliko makubwa ya mifumo ya siasa na
uchumi duniani. Kambi ya nchi zilizokuwa zinafuata mfumo wa siasa na uchumi wa
Ujamaa zilianza kusambaratika na nchi hizo kuanza kufuata siasa ya uchumi wa soko
huria ambao udhibiti wa serikali katika uchumi na mfumo wa udhibiti wa siasa kupitia
chama kimoja viliondoka. Hali hii ilizikumba pia nchi changa, Tanzania ikiwemo.
Kutokana na kuondoka kwa udhibiti wa dola katika uchumi na siasa, wananchi walipata
fursa zaidi ya kupata habari kuhusu masuala mengi na kuwa na uhuru wa kuanzisha
vyombo vya habari vya binafsi. Mfumo wa sheria nao ilibidi ubadilike kuendana na hali
halisi. Na kwa upande wa utangazaji Sheria ya Utangazaji, sura 306 ilitungwa na kuunda
chombo cha usimamizi katika utangazaji (Tume ya Utangazaji).
Kuingia kwa utandawazi mwishoni mwa miaka ya 1990, kulileta mabadiliko zaidi ya
kisheria ili kuruhusu ushindani zaidi kwani kulifanya milango ya uchumi kuachwa wazi
zaidi katika juhudi za kuifanya dunia kuwa kijiji kimoja. Kwa upande wa habari
ilitungwa sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano ya mwaka 2003. Hii iliunganisha Tume ya
Mawasiliano (Tanzania Communication Commission) na Tume ya Utangazaji (Tanzania
Broadcasting Commission) na kuunda Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano (TCRA).
TAASISI YA UTANGAZAJI TANZANIA
Taasisi ya Utangazaji Tanzania (Tanzania Broadcasting Services) kilikuwa chombo cha
utangazaji cha umma kilichoundwa chini ya Sheria ya Mashirika ya Umma na Sheria ya
Utangazaji chini ya Tangazo la Serikali namba 239 la mwaka 2002 {The Tanzania
Broadcasting services (Taasisi ya Utangazaji-TUT) (Establishment), Order 2002}. TUT
lilikuwa shirika la umma lililoundwa kwa ajili ya kufanya utangazaji wa umma (PSB).
111
Lilikuwa muunganiko wa iliyokuwa Radio Tanzania Dar es salaam (RTD) na iliyokuwa
Televisheni ya Taifa (TVT) ambavyo vilikuwa vyombo vya utangazaji vya dola (State
Broadcasters). TUT ilianza kazi rasmi mwezi Julai 2004.
SHIRIKA LA UTANGAZAJI TANZANIA (TBC)
TBC imeanzishwa kwa mujibu wa kifungu namba 4 cha sheria ya mashirika ya umma
kinachompa Rais mamlaka ya kuanzisha Mashirika ya umma kwa amri itakayotolewa
kupitia Gazeti la Serikali (Government Gazette) kwa ajili ya kazi au malengo maalum.
TBC pia imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Utangazaji ya mwaka 1993 ambayo
katika kifungu cha 4 inaainisha kuwa waziri wa Habari anaweza kufanya shughuli za
Utangazaji nchini zitakazokuwa zinajulikana kama Tanzania Broadcasting Services kwa
ajili ya kutoa elimu, burudani, na habari kwa wasikilizaji na watazamaji nchini, nje ya
nchi (pale anapoona inafaa) na kuweka vituo mbalimbali vya utangazaji nchini. Kifungu
kinaeleza wazi kwamba kazi hii ya utangazaji itafanywa na matawi mawili ya utangazaji-
RTD na TVT {kifungu 4(2)}. TBC pia imeainishwa katika sehemu ya tano ya sheria ya
Mamlaka ya mawasiliano ikieleza pia majukumu yake kama PSB. Hivi ni vifungu pia
vilivyoanzisha TUT. Kupitia kifungu namba 4 cha sura 257, Rais alitoa amri ya
uanzishwaji wa TBC kupitia tangazo la serikali namba 186 la 2007 {The Tanzania
Broadcasting corporation (Shirika la Utangazaji Tanzania-TBC) (Establishment) Order
2007}.
CHANZO CHA MABADILIKO
Baada ya kutathmini utendaji wa TUT kwa miaka miwili ya utendaji wake, Bodi ya
Wakurugenzi ya TUT ilibaini mapungufu kadha yaliyokuwa yakisababisha kushindwa
kutimiza malengo na majukumu yake. Matatizo hayo yalikuwa ya ndani na nje. Hivyo
Bodi iliamua kuwa yalitakiwa mabadiliko makubwa na ya haraka kuweza kurekebisha
hali hiyo. Mabadiliko hayo ilikuwa lazima yaanzie katika mabadiliko ya sheria.
Yalilenga hasa kuionesha TUT waziwazi kama Shirika la umma lililo na hadhi yake ya
kisheria na kuainisha wazi kazi yake kama chombo cha utangazaji cha umma chenye
jukumu la kutangaza kwa jamii zote na kuainisha uhusiano wake na serikali katika
utekelezaji wa jukumu lake hilo.
112
Maeneo muhimu yaliyofanyiwa mabadiliko ni pamoja na Jina. Jina la Taasisi ya
Utangazaji Tanzania lilikuwa halieleweki vizuri na lilikuwa haliendani na maana halisi
na kazi za chombo husika. Ilionekana kama Taasisi tu ya serikali na sio chombo huru cha
umma kinachotakiwa kuwajibika kwa umma. Maana ya jina hilo ilikuwa haieleweki kwa
umma, serikali na hata wafanyakazi wenyewe. Ndipo Bodi ilipoaumua kuchagua jina la
Shirika la Utangazaji Tanzania,ambalo kwa kiasi kikubwa limeondoa utata.
Tangazo namba 239 la 2002 halikuainisha wazi kuwa TUT ina uwezo wa kuingia katika
mikataba, kushtaki au kushtakiwa yenyewe, uwezo wa kukopa kwa kuweka rehani mali
zake na kuwa na uwezo wa kuuza na kununua mali kwa jina lake. Kifungu hicho
kimeongezwa katika Tangazo namba 186 la 2007 (kifungu 3(2)).
TBC KAMA SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA UMMA
Ripoti mojawapo ya Shirika la Umoja wa Mataifa la UNESCO inaelezea Shirika la
Utangazaji la umma kama chombo ambacho hakiambatani na ushawishi wa kibiashara au
ule wa nguvu za dola na kwamba lengo kubwa la chombo hiki ni kutoa huduma sawa
kwa umma wote iwe ni kwa kuwafahamisha, kuwaelimisha ama kuwaburudisha. Tafsiri
ya UNESCO inaeleza kuwa Shirika la Utangazaji la umma ni chombo ambacho raia wote
wa nchi husika hukubalika na kuwa sawa. Ni chombo kinachotumikia raia wote bila
kujali hali zao za kijamii, kisiasa ama kiuchumi. Ni chombo cha upeo wa juu, chenye
uwezo wa kutosha na kilicho huru. Kwa tafsiri hiyo utaona kwamba chombo hiki ni
muhimu sana katika nchi inayozingatia utawala wa kidemokrasia.
Unapotafakari historia na maendeleo ya siasa (hususani ukombozi wa nchi yetu,
ukombozi wa nchi jirani, kuingia kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa), uchumi, ulinzi
na usalama wa nchi hii, umoja, amani na mshikamano wa Watanzania, maendeleo na
changamoto katika maisha ya jamii katika afya, elimu, kilimo, ujasiriamali, michezo,
utamaduni nakadhalika huwezi kusahau mchango wa Radio Tanzania Dar es salaam,
Televisheni ya Taifa, Taasisi ya Utangazaji Tanzania na sasa TBC katika kupasha habari,
kuelimisha na kuburudisha.
113
MATARAJIO
Ni shabaha ya TBC kuifanya Kanda ya Kati kuwa kituo chake cha utangazaji cha pili
kwa ukubwa baada ya Dar es salaam. Hatua hiyo maana yake ni kuongeza vitendea kazi
vyenye kutumia teknolojia ya kisasa pamoja na watendaji ili kazi ya kutayarisha vipindi
na habari za redio na televisheni ziweze kufanyika kwa ukamilifu. Huduma hiyo ya
utangazaji itakapowezekana itakuwa ya manufaa pia kwa mikoa jirani ikizingatiwa kuwa
Dodoma ni katikati ya nchi.
114
SURA YA NNE
4.0. SERA NA SHERIA ZILIZOKUWEPO TANGU 1961 HADI SASA
4.1. Sera ya Vijiji vya Ujamaa:
Mwaka 1969, kupitia Waraka wa Rais kumbukumbu Na. SHC. C. 180/1 wa tarehe 20
Machi 1969, Serikali ilianzisha Vijiji vya Ujamaa ambapo wananchi walitakiwa kuishi
kwa pamoja na kufanya kazi pamoja kwa faida ya wote. Mfano huu wa maisha ulikuwa
na lengo la kuwawezesha wananchi wote kupata huduma za Kijamii kama vile Afya,
Elimu, Maji na Barabara: Suala hili lilikaziwa na Sheria ya Vijiji Na.7 ya mwaka 1982.
4.2. Azimio la Arusha:
Mnamo tarehe 05 Februari, 1967 Serikali ilitangaza kuanzishwa kwa Azimio la Arusha
kwa lengo la kuwajenga watanzania katika misingi ya Ubinadamu na Usawa. Azimio la
Arusha liliweka pia miiko ya Uongozi ambayo iliwakataza viongozi kujilimbikizia mali,
kutoa au kupokea Rushwa; Kuanzishwa kwa Azimio la Arusha kulifuatiwa na
kutaifishwa kwa mali binafsi na kuanzishwa kwa mashirika ya Umma.
4.3. Jeshi la Kujenga Taifa:
Katika kujenga uzalendo, Serikali ilitunga Sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa Na:16 ya
mwaka 1964. Chini ya Sheria hii, wananchi na viongozi walitakiwa kuhudhuria mafunzo
ya Jeshi la Kujenga Taifa ambako huko walipatiwa mafunzo na mbinu za Uzalendo,
Moyo wa kutetea na kulinda nchi yako; Mbali ya viongozi wa Kitaifa, vijana kutoka
Vyuo mbalimbali na shule za Sekondari waliendelea kuhudhuria mafunzo hayo kwa
vipindi mbalimbali.
4.4. Mabaraza ya Wafanyakazi:
Tangazo la Rais Namba 1, la mwaka 1970 lilianzisha Mabaraza ya Wafanyakazi sehemu
za kazi waraka huo wenye kumbukumbu Namba SHC/C.180/1/1102 wa tarehe 10
Februari, 1970 ulitoa maelekezo ya ushirikishwaji wa wafanyakazi katika maamuzi
muhimu ya utoaji huduma na uzalishaji sehemu za kazi. Matawi ya Mabaraza ya
Wafanyakazi yalianzishwa katika sehemu mbalimbali za kazi.
115
4.5. Madaraka Mikoani:
Mwaka 1972 Serikali ilianzisha Mfumo wa Madaraka Mikoani kwa kuanzisha Kurugenzi
za Maendeleo za Mikoa na kuvunja Halmashauri za Wilaya na Miji. Katika mfumo huo,
Mkuu wa Mkoa alikuwa ni Kiongozi wa Serikali akisaidiwa na Mkurugenzi wa
Maendeleo wa Mkoa (RDD). Katika ngazi ya Wilaya Mkuu wa Wilaya alikuwa ni
Kiongozi wa Serikali akisaidiwa na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Wilaya (DDD).
4.6. Sera yaTaifa yasArdhi – 1995
Sera yaTaifa ya Ardhi iliidhinishwa na Seriali mwaka 1995 kwa madhumuni ya
kutambua HAKI ya kila raia kumiliki ardhi kwa matumizi mbalimbali na kwamba Ardhi
yote ya Tanzania ni mali ya Umma, chini ya Udhamini wa Rais kwa niaba ya Raia wote.
4.7. Sera ya Maendeleo ya Mtoto - 1996:
Sera ya Maendeleo ya Mtoto Tanzania ya mwaka 1996 ililenga kuelimisha jamii kuelewa
haki za msingi za Mtoto.
4.8. Sheria ya Ardhi Na. 4 na 5 za 1999
Sheria hizi zimeanzishwa ili kukidhi ongezeko kubwa la idadi ya watu na mifugo pamoja
na mahitaji ya matumzi na namna ya kumiliki na kusimamia aina zote za ardhi ya
kawaida, Ardhi ya Vijij na Ardhi ya Hifadhi.
4.9. Sera ya Menejimenti na Ajira – 1999:
Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma ya mwaka 1999 ilikuwa na
lengo la kuboresha huduma zitolewazo na Serikali kupitia Utumishi unaozingatia sifa na
usimamizi unaopima matokeo ya kazi.
4.10. Sera ya Maendeleo ya Wanawake – 2003:
Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2003 ililenga kusawazisha tofauti
zilizopo baina ya Wanawake na Wanaume ili kuweka mazingira mazuri yatakayowezesha
wote kutekeleza majukumu yao katika kujiletea maendeleo na kuondoa umasikini kwa
kuzingatia mahitaji ya Kijinsia.
4.11. Sera ya Maendeleo Vijijini – 2003:
Sera ya Maendeleo Vijijini (Rural Development Policy) ya mwaka 2003 ililenga
kuongeza fursa na upatikanaji wa Huduma za Kiuchumi na kuhakikisha kunakuwepo na
Utawala Bora.
116
4.12. Sera ya Taifa ya Biashara – 2003:
Sera ya Taifa ya Biashara (National Trade Policy) ya mwaka 2003 ilikuwa na lengo la
kuongeza ufanisi na kupanua wigo wa mahusiano ya uzalishaji wa ndani na kuimarisha
Biashara ya nje kama mkakati wa kuongeza kasi ya ukuaji wa Kiuchumi na Maendeleo.
4.13. Sera ya Taifa ya Umwagiliaji – 2010:
Sera ya Taifa ya Umwagiliaji (National Irrigation Policy) ya mwaka 2010 imelenga
kuhakikisha upatikanaji endelevu wa maji ya umwagiliaji yatayoleta manufaa katika
uzalishaji wa mazao ambayo yatachangia katika kuwa na uhakika wa chakula na
kupunguza umasikini.
4.14. Sera ya Elimu na Mafunzo – 1995:
Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 ililenga kuboresha na kuimarisha elimu
itolewayo katika ngazi zote ili iendane na maendeleo ya Kijamii nchini.
4.15. Sera ya Misitu – 1953:
Sera ya Misitu ya mwaka 1953 na kufanyiwa marekebisho mwaka 1963 na 1998 zote hizi
zilikuwa na lengo na kuwa na matumizi endelevu ya Misitu. Sera hii ilienda sambamba
na Sera ya mazingira ya mwaka 2004 ambayo ilieleza juu ya Hifadhi endelevu ya
Rasilimali.
4.16. Sera ya Maendeleo ya Jamii – 1996:
Lengo la Sera ya Maendeleo ya Jamii ya mwaka 1996 ilikuwa na lengo la kuwawezesha
wananchi mmoja mmoja au kikundi kuchangia zaidi katika azma ya kujitegemea katika
ngazi za familia na hatimaye Taifa kwa ujumla wake.
4.17. Sera ya Maji ya mwaka 1971 - 1991:
Sera hii ililenga kuwapatia wananchi wote maji safi na salama katika umbali usiozidi
mita 400 kutoka katika makazi yao. Chini ya Sera hii Serikali ilikuwa ndiye mwekezaji
pekee, mtekelezaji na mwendeshaji wa miradi ya maji vijijini na mijini.
4.18. Sera ya maji ya mwaka 2002:
Leongo kubwa la Sera hii ni kuhakikisha kwamba wananchi wanahusishwa katika
kupanga, kujenga na kuendesha miradi ya maji wao wenyewe, tofauti na ilivyokuwa
katika sera ya awali. Majukumu ya Serikali yalibadilika kutoka kwenye Serikali kuwa
mtoa huduma na kubaki na majukumu ya uratibu, utungaji wa sera namiongozo na
udhibiti.
117
4.19. Sheria Na.25 ya Elimu – 1978:
Katika sheria hii mambo kadhaa ya Elimu yalitajwa ikiwamo, fursa ya Elimu kwa wote,
kuundwa kwa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), kurudisha mitihani ya kidato cha
Pili (Form Two) kwa shule za Sekondari na Darasa la Saba (STD VII) kwa shule za
Msingi. Sheria hii pia iliruhusu mfumo wa uendeshaji wa shule na vyuo kupitia Bodi za
shule na vyuo.
4.20. Sheria ya Elimu – 1962:
Baada ya kupata Uhuru, Serikali ya Tanganyika ilipitisha Sheria ya Elimu ya mwaka
1962 ambayo iliondoa ubaguzi aina yoyote katika utoaji wa Elimu kubadili mfumo wa
mihutasari, lugha ya kufundishia na mitihani. Pia Sheria hii iliwapa wazalendo madaraka
ya uongozi katika ngazi zote za Elimu nchini.
4.21. Sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Na. 11 ya 2007:
Kabla ya kutungwa kwa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007,
kulikuwepo na Sheria mbalimbali zilizotungwa na Serikali ya Tanzania ili Kuzuia na
Kupambana na Rushwa. Sheria hizo ni pamoja na Sheria ya Kuzuia Rushwa (Sura ya
400) na Sheria ya Kuzuia Rushwa ya mwaka 1971.
4.22. Sheria Na. 7 ya mwaka 1982
Hii ni Sheria ya Serikali za Mitaa Halmashauri za Wilaya ambayo inatoa mwongozo wa
kuendesha mamlaka za Serikali za Mitaa katika Halmashasuri za Wilaya.
4.23. Sheria Na. 8 ya mwaka 1982:
Hii ni Sheria ya Serikali za Mitaa Halmashauri za Miji ambayo inatoa mwongozo wa
kuendesha mamlaka za Serikali za Mitaa katika Halmashasuri za Miji.
4.24. Sheria Na. 9 ya mwaka 1982
Hii ni Sheria yas Fedha ya Serikali za Mitaa ambayo inatoa mwongozo wa usimamizi wa
fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
4.25. Sheria Na. 2 ya mwaka 2002 ya Programu ya Huduma kwa Jamii
Lengo la Sheria hii ni kupnguza msongamano usio wa lazima kwa wafungwa Magerzani.
118
4.26. Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa:
Sheria Na. 4 ya mwaka 1979 na Sheria Na.11 ya mwaka 1984 zimetungwa kwa lengo la
kusimamia Chaguzi mbalimbali zinazofanyika katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
4.27. Sheria ya Manunuzi Na. 21 ya 2004
Sheria hii ilitungwa kwa madhumuni ya kutoa mwongozo wa kufanya manunuzi ya vifaa
na huduma katika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa.
119
SURA YA TANO
5.0. MABADILIKO NA MATUKIO MAKUU KATIKA MFUMO WA KISIASA,
KIULINZI, KIUTAWALA, KITEKNOLOJIA, KIUCHUMI NA KIJAMII
5.1. Kujengwa kwa kambi ya Wapigania Uhuru Kongwa:
Mwaka 1964, Kambi ya Wapigania Uhuru kutoka nchi za Kusini mwa Afrika
ilijengwa katika Wilaya ndogo ya Kongwa. Vyama vya ukombozi zilizohusika
katika kuleta wapigania Uhuru wake ni FRELIMO (Msumbiji); MPLA (Angola),
SWAPO (Namibia), PAC na ANC (Afrika Kusini) na FROLIZI (Zimbabwe).
5.2. Kuanzishwa kwa Kilimo cha Zabibu Dodoma:
Historia ya zao la Zabibu ni ndefu katika Mkoa wa Dodoma kwani inasemekana
ya kwamba mwanzoni mwa miaka ya 1950 Mapadri wa Kikatoliki walipanda Mti
wa kwanza huko Kondoa wakitumia Miti kutoka Italia. Askofu wa Bihawana
alianzisha majaribio ya Kilimo cha Zabibu kunako mwaka 1955 katika eneo hilo.
Aidha Mkuu wa Magereza nchini Tanzania (kwa wakati huo) Bwana O. K.
Rugimbana aliamua kufanywe majaribio ya kilimo cha Zabibu kwenye Gereza la
Isanga.
Mwanzoni mwa mwaka 1965, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw. J. B.
M. Mwakangale aliunda Kamati ya watu 12 ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya
Bwana H. Taratibu akishauriwa na Afisa Kilimo wa Wilaya Bwana N. Magohe ili
kuona njia za kuwawezesha wakulima kuanzisha kilimo cha Zabibu.
Mwaka huo 1965, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere alipotembelea Dodoma alitangaza kuwa zao la Zabibu ndilo
litakuwa zao Kuu la Biashara na Uchumi kwa Mkoa wa Dodoma. Hili ni tukio
muhimu lililoendeleza Kilimo cha Zabibu na Kiwanda cha kutengeneza Mvinyo
kikajengwa na Wamisionari, kikaendeshwa na Waingereza kabla ya kukabidhiwa
kwa National Milling Cooperation ingawa baadaye kiwanda hicho kilikufa
kutokana na uongozi mbovu.
120
5.3. Kujengwa kwa Handaki la Kihistoria Kongwa:
Mwaka 1968 wapigania Uhuru waliokuwa katika Kambi ya Kongwa walijenga
Handaki ambalo lilitumiwa na Rais wa kwanza wa Msumbiji Hayati Samora
Machel kama Ofisi yake. Handaki hilo lilijengwa na Mzee Mabaya ambaye
alikuwa ni raia wa Afrika Kusini na lilikuwa na urefu upatao mita 150 na kina
kipatacho mita 4.
5.4. Operesheni Dodoma:
Operesheni hii ilianza Juni, 1971 kwa lengo la kubomoa makazi ya zamani ya
kuishi mmoja mmoja na kujikusanya pamoja katika sehemu maalum zilizopimwa
kwa kuanzisha Vijiji vya Ujamaa. Jumla ya Vijiji 190 vilianzishwa ambapo
Kilimo cha Sesa na Mashamba ya Ujamaa vilianzishwa ikiwa ni hatua ya
maendeleo ya Vijiji hivyo.
5.5. Kuanzishwa kwa Mradi wa Hifadhi Ardhi Dodoma - HADO:
Mradi wa Hifadhi Ardhi Dodoma ulianzishwa mwaka 1973 katika Mkoa wa
Dodoma ili kukabiliana na ongezeko la mmomonyoko wa udongo uliokuwa
umeathiri mazingira ya Mkoa. Wilaya zilizohusika katika Programu hii ni
Kondoa, Mpwapwa na Dodoma Vijijini.
Kwa kuwa Wilaya ya Kondoa ilikuwa imeathirika vibaya kuliko Wilaya zingine,
basi Makao Makuu ya Mradi wa HADO yaliwekwa Kondoa. Lengo Kuu la mradi
huu lilikuwa kuzuia uendelezaji wa mmomonyoko wa udongo kwa kutumia
mbinu za Kitaalamu ili ardhi hiyo iweze kuongolewa na kutumika kwa uzalishaji
mali.
5.6. Kuanzishwa kwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu - CDA - 1973:
Mji wa Dodoma ulianzishwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) ili
uweze kuendelea kwa kasi na kwa mpangilio. Mwaka 1973, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitangaza Rasmi
kuanzishwa kwa CDA.
Waziri wa kwanza wa Ustawishaji Makao Makuu (Ofisi ya Rais) alikuwa Mhe.
Adamu Sapi Mkwawa (ambaye sasa ni marehemu) na Mkurugenzi Mkuu wa
kwanza wa CDA alikuwa Mhe. Clement George Kahama.
121
Mwaka 1976 Mpango wa Makao Makuu Dodoma (Dodoma Master Plan)
uliobuniwa na kuandaliwa na Kampuni ya Project Planning Associates ya Canada
na Wataalam Wazalendo wa Tanzania, ulikamilika na kuidhinishwa na Serikali.
5.7. Dodoma kuwa Makao Makuu ya CCM:
Tarehe 05 Novemba, 1976 kilifanyika kikao cha pamoja kati ya TANU na ASP
ambapo kilipokea mapendekezo ya Tume ya watu 20. Katika kikao hicho,
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitangaza kuwa jina la Chama kipya ni
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM). Ilikubalika Chama kipya kizinduliwe rasmi
tarehe 05 Februari, 1977 na kutangazwa DODOMA kuwa Makao Makuu ya
Chama.
5.8. Kuanzishwa kwa Ikulu ndogo ya Chamwino:
Baada ya kupitishwa kwa Dodoma kuwa Makao makuu ya Chama na Serikali
mwaka 1973, ujenzi wa Ikulu ndogo ya Chamwino ulianza. Ujenzi huo
ulikamilika na kukabidhiwa kwa Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere tarehe 05
Febreuari, 1981 wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka mine ya CCM.
5.9. Bunge kuhamishia shughuli zake Dodoma:
Dodoma ilianza kupata hadhi ya kuwa Mwenyeji wa Bunge la Tanzania kwa
mikutano ya kawaida isipokuwa Bunge la Bajeti mwaka 1981 shughuli za Bunge
zilikuwa zikifanyika katika ukumbi wa CCM Makao Makuu ambao sasa ni Tawi
la Benki ya NMB mwaka 1991 shughuli za Bunge zilihamishiwa katika Ukumbi
wa Pius Msekwa.
Mnamo mwaka 1995, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Benjamini William Mkapa aliamua kuhamishia shughuli zote za Bunge
Mjini Dodoma ambapo mwaka 2005 ulifanyika ujenzi wa Jengo jipya la Bunge
Mjini Dodoma.
5.10. Mvua za El-Nino:
Mwishoni mwa mwaka 1997, Mvua kubwa za El-Nino zilinyesha Mkoani
Dodoma na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya Barabara, Madaraja,
nyumba pamoja na mashamba ya mazao mbalimbali.
122
5.11. Ofisi ya TAMISEMI Kuhamia Dodoma
Mwaka 1998, Rais wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa alianzisha
Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na kutangaza kuwa Makao
makuu ya Wizara hiyo yatakuwa Dodoma.
5.12. Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru:
Mwaka 1999 mbio za Mwenge wa Uhuru zilihitimishwa Mkoani Dodoma katika
uwanja wa Jamhuri. Katika sherehe hizo Mgeni Rasmi alikuwa Mhe. Benjamin
William Mkapa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
5.13. Ajali ya Treni ya Abiria:
Treni ya Abiria ilipata ajali katikati ya eneo la Stesheni ya Msagali na Igadu
Wilayani Mpwapwa tarehe 24 Juni, 2002. Katika ajali hiyo watu 288 walipoteza
maisha na wengine kujeruhiwa. Maiti 200 walizotambuliwa na kuchukuliwa na
ndugu zao, Maiti 88 ambao hawakutambuliwa walizikwa katika makaburi ya
Mailimbili Dodoma Mjini tarehe 27 Juni, 2002.
5.14. Kuzinduliwa kwa Machinjio ya kisasa ya Dodoma:
Machinjio ya kisasa ya Dodoma iliyopo eneo la Kizota katika Manispaa ya
Dodoma yaliwekewa jiwe la Msingi tarehe 28 Julai, 2003 na Mhe. Rais Benjamin
William Mkapa na ilizinduliwa rasmi mwezi Agosti na Mhe. Dr. Shukuru J.
Kawambwa Waziri wa Mifugo. Mnamo Agosti 2005 Machinjio hiyo ilikabidhiwa
rasmi Serikalini na Mkandarasi aliyekuwa anajenga.
5.15. Mlipuko wa Homa ya Bonde la Ufa (RVF)
Mwanzoni mwa mwaka 2007 Mkoa wa Dodoma ulikumbwa na mlipuko wa homa
ya Bonde la Ufa (RVF). Hadi tarehe 02/05/2007 tukio la mwisho wa upande wa
mifugo liliporipotiwa, vijiji 93 vyenye ng’ombe 202,436, Mbuzi 83,097 na
Kondoo 38,098 vilikuwa vimetoa taarifa ya matukio yaliyoashiria RVF, ng’ombe
2,562, Mbuzi 3,600 na Kondoo 1,322 waliripotiwa kutupa mimba kutokana na
RVF. Aidha ng’obme 588, Mbuzi 1,074 na Kondoo 442 walikufa kwa dalili za
RVF, Ugonjwa huu ulidhibitiwa ilipofika katikati ya mwezi Juni 2007.
123
5.16. Kuzinduliwa kwa Chuo Kikuu cha Dodoma (Dodoma University)
Chuo Kikuu cha Dodoma kilianzishwa rasmi tarehe 16 Februari 2007 siku
ambayo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipowateua viongozi
wakuu wa Chuo yaani Mkuu wa Chuo, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Makamu
Mkuu wa Chuo na Manaibu wake wawili tarehe 10 Septemba, 2007 wanafunzi
wazilishi walipokelewa.
5.17. Kuungua kwa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa:
Tarehe 28 Agosti 2010, Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma liliteketea kwa
moto uliotokea majira ya Saa 4.00 usiku. Jengo, Samani na Nyaraka mbalimbali
vyote viliteketea kwa moto. Chanzo cha moto huo kinasadikiwa ni hitilafu ya
Umeme.
124
SURA YA SITA
6.0. CHANGAMOTO NA MATARAJIO YA BAADAYE
6.1. Changamoto zilizojitokeza
Pamoja na mafanikio haya ambayo Mkoa umeweza kuyapata katika kipindi cha
miaka 50 ya UHURU, Pia unakabiliwa na changamoto zifuatazo:
• Upungufu wa Watumishi katika baadhi ya Sekta kama Elimu, Afya,
Kilimo, Mifugo.
• Ukosefu wa Soko la ndani la uhakika kwa ajili ya mazao ya kilimo na
mifugo. Kwa mfano hakuna viwanda vya usindikaji wa Nyanya, Maziwa,
Nyama, Ngozi nk.
• Ufinyu wa Bajeti unasababisha baadhi ya Sekta kutotengewa fedha za
kutosha kutekeleza mipango iliyowekwa. Kwa upande mwingine fedha
kuchelewa kutoka HAZINA na hivyo kuathiri ratiba za utekelezaji.
• Maslahi na mazingira duni ya baadhi ya watumishi kama vile, mishahara
midogo, ukosefu wa nyumba za watumishi, ukosefu wa vitendea kazi.
Haya yote yamekuwa yakiathiri utendaji wa kazi kutokana na kushuka
kwa ari ya kufanya kazi miongoni mwa watumishi.
• Matumizi mabaya ya maliasili kama vile ukataji miti ovyo, kilimo
kisichofuata kanuni bora ufugaji na ulishaji mifugo unaozidi uwezo wa
malisho, uchomaji moto ovyo na uharibifu wa vyanzo vya maji.
• Kuanzishwa kwa Sekretarieti ya Ajira kumesababisha ugumu wa kupata
watumishi wa kada kama za Maafisa Watendaji wa Kata, Maafisa
Watendaji wa Vijiji, Wahudumu na madereva. Hii inatokana na mchakato
wa Ajira kufanywa bila mtu kujua atapangwa Mkoa au Wilaya gani.
Hivyo anapofaulu na kupangiwa sehemu yenye mazingira asiyoyazoea
huripoti na kuondoka.
125
• Hali ya ukame inayotokea mara kwa mara imekuwa na athari katika
uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo na hivyo kuathiri ukuaji wa
uchumi na ustawi wa wananchi wa Mkoa wa Dodoma. Mkoa umekuwa
ukipata mvua chini ya milimita 400 ambayo hazitoshelezi kustawisha
mazao na kusababisha uzalishaji duni wa mazao ya kilimo, ukosefu wa
malisho ya mifugo na maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu na
wanyama.
• Uwezo mdogo wa Mamlaka ya Serikali za mitaa katika ukusanyaji wa
mapato ya ndani umekuwa ukiathiri utekelezaji wa baadhi ya majukumu
ya mamlaka hizo.
• Mfumo wa utoaji wa Huduma za kijamii kama vile Afya, Elimu na Maji
haujakidhi mahitaji kutokana na ongezeko la idadi ya watu na bajeti finyu
• Ufanisi wa Sera. Sera nyingi zimeandaliwa katika kutoa mwongozo wa
utekelezaji wa masuala muhimu ya Kitaifa. Hata hivyo ufanisi wa Sera
hizo unaskuwa siyo wa kuridhisha kutokana na kukabiliwa na changamoto
za upatikanaji wa rasimaliwatu katika ngazi mbalimbali, uwezo wa
kifedha pamoja na namna tunavyoweka vipaumbele;
6.2. MATARAJIO YA BAADAYE ( the way forward)
• Katika miaka 50 ijayo Mkoa wa Dodoma unatarajia kujitosheleza kwa
chakula na kupnguza umasikini wa kipato kwa wananchi wake.
• Kuendelea kuzisimamia mamlaka za Serikali za Mitaa ili ziweze kutoa
huduma bora za Jamii ikiwemo Elimu na Afya.
• Kusimamia mamlaka mbalimbali zinazotoa huduma za maji ili
kuhakikisha kuwa kunakuwepo upatikanaji wa maji safi nasalama kwa
watu wote kwakuandaa nakutekeleza mipango shirikishi yausimamizi
nauendelezaji wa rasilimali za maji.
• Kujenga uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea kwa kusimamia
utekelezaji wa shughuli za Kilimo, Mifugo, Miundombinu ya barabara
pamoja na matumizi sahihi ya raslimali za Taifa.
126
7.0. REJEA MBALIMBALI (REFERENCES)
1. Sura ya Dodoma Mamlaka ya Makao Makuu Tanzania “Publishing
House – Dar es Salaam Toleo la Pili 1980
2. Historia, Mila na Desturi za Wagogo Mathias E. Mnyampala – East
African Literature Bureau toleo la Pili 1971
3. National capital Master Plan Dodoma – TanzaniaCapital Development
Authority Tanzania and Project Planning Associates Limited Canadaz
May 1976
4. Gazeti la Nchi yetu Tanzania - Toleo Na. 40 Mei 1967
5. Gazeti la Nchi yetu Tanzania - Toleo Na. 94 Novembe 1971
6. 2002 Population and Housing census General Report. Central census
Office National Bureau of statistics presidents Office – Planning and
Privatization 2003
7. Nyerere J. K. UJAMAA,OUP,DAR ES SALAAM (1968)
8. PRIMARY SCHOOL HANDBOOK,No1 (std 1-iv) Department of
EducatioDar Es Salaam
9. MWONGOZO WA ELIMU YA WATU WAZIMA (1980) Wizara ya
Elimu ya Taifa, Dar es Salaam,
10. The Effectveness of Public Policies in Tanzania - Final Report -
Vol.I.August, 2010Economic and social Research Foundation ESRF
Dar es Salaam
Subscribe to:
Posts (Atom)
Duh! Tumeshiba kuelewa ..inatakiwa namna hii mtu huulizi swali..kazi nzuri bigup
ReplyDeleteNimefurahi sana kuipata historian hii nzuri ya mkoa was dodoma
ReplyDeleteNimefurahi sana kuipata historian hii nzuri ya mkoa was dodoma
ReplyDeleteDuh ngoj niwaze Kwanza
ReplyDelete